Tukiachana na viongozi wa kitaifa..je ni raia wangapi wakifa hutangazwa msiba wa Kitaifa.?

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,312
Kulingana mkanganyiko unaoendelea juu ajali iliyochukua maisha ya watoto wetu pamoja na walimu wao.

Wengine wakishauri huu msiba uwe wa Kitaifa kwa maana Jumatatu iwe siku ya mapumziko kuomboleza huu msiba.

Wengine wakihoji mbona huko nyuma kuliwahi kutokea ajali zilizochukua roho nyingi zaidi lakini hakukuwa na kelele kuwa uwe msiba wa Kitaifa.

Naomba ufafanuzi kujua ni watu wangapi wakifa au ni utaratibu gani hutumika ili Taifa liomboleze kitaifa kwa raia wa kawaida...?
 
Wataalamu wa itifaki za majanga hampo..!
 
Mkuu hebu tupe mfano wa ajali iliyouwa watu wengi na serikali haikuupa uzito matukio hayo.
 
Nchi zinazothamini wqtoto Leo ungekuwa ni msib Wa taiga..ika si kwa taiga letu..mwenyezi Mungu awape heri wadogo zetu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu ni ajali nyingi zimetokea hapo katikati bara na visiwani....lakini ninayoikumbuka ni ile ya Majinja pale Mafinga iliua zaidi ya watu 50....
Kama hatukuwa na utamaduni wa kuwaenzi wafu na matukio makubwa kama haya basi tuanze na hili la Arusha si vibaya.
 
Swali linabaki palepale je watu wangapi wakifa serikali inaweza kutangaza maombolezo ya kitaifa.?
 
Nchi zinazothamini wqtoto Leo ungekuwa ni msib Wa taiga..ika si kwa taiga letu..mwenyezi Mungu awape heri wadogo zetu
Wewe hebu toka huko ukisema kitu sema nchi fulani walifariki watoto kadhaa ikafanyika hivi kwa maana nyingine with evidence. Yaani Ushiriki/juhudi zote za serekali unaziona bure kweli 'Mwenye hasidi siko zote hana sababu'!( tafuta mswahili akufafanulie maana yake)
 
Msiba w kitaifa ni upi? Ni kweli kuna mkanganyiko kwenye hili. Labda serikali ina miongozo yake au inategemea nani yuko madarakani? Kwa hili la Arusha kwa mfano sijasikia bendera yetu inarukaje, nilidhani kwa misiba ya kitaifa bendera huruka nusu mlingoti kwa siku tajwa.
 
Kulingana mkanganyiko unaoendelea juu ajali iliyochukua maisha ya watoto wetu pamoja na walimu wao.

Wengine wakishauri huu msiba uwe wa Kitaifa kwa maana Jumatatu iwe siku ya mapumziko kuomboleza huu msiba.

Wengine wakihoji mbona huko nyuma kuliwahi kutokea ajali zilizochukua roho nyingi zaidi lakini hakukuwa na kelele kuwa uwe msiba wa Kitaifa.

Naomba ufafanuzi kujua ni watu wangapi wakifa au ni utaratibu gani hutumika ili Taifa liomboleze kitaifa kwa raia wa kawaida...?
Mkuu, nini maana ya msiba wa Kitaifa, binafsi najua kitendo cha Makamu wa Rais kuongoza wakazi wa Arusha kuaga miili ya watoto wetu wapendwa, tayari ni ngazi ya Kitaifa na Seriklai imeshiriki kikamilifu. Tatizo naloona hapa kwa baadhi yetu ni "uzembe/uvivu", wanataka itangazwe siku ya maombolezo ambayo itaambatana na kutoenda kazini ili walale nyumbani.
 
Idawa kila nafsi ya mwanadamu ina thamani sawa sawa na ya mwingine yeyote awe rais, mbunge, waziri, mkulima, mfugaji, mwanafunzi nk.

Ni suala la hekima na utu tu kwa kiongozi/viongozi badala ya sheria..... hivyo ilistahili na ilipaswa kuwa kufikia sasa hivi Serikali iwe imeandaa utaratibu na kuuweka bayana + eneo la kuwazika watoto wetu wale na kujenga mnara wa kumbukumbu.
 
Mkuu, nini maana ya msiba wa Kitaifa, binafsi najua kitendo cha Makamu wa Rais kuongoza wakazi wa Arusha kuaga miili ya watoto wetu wapendwa, tayari ni ngazi ya Kitaifa na Seriklai imeshiriki kikamilifu. Tatizo naloona hapa kwa baadhi yetu ni "uzembe/uvivu", wanataka itangazwe siku ya maombolezo ambayo itaambatana na kutoenda kazini ili walale nyumbani.
Umemaliza yooote, big up.
 
Sidhani kama siku za maombolezo lazima watu wasiende kazini. Naamini kunakuwa na urushaji wa bendera nusu (I stand to be corrected). Kumbukumbu yangu ya msiba wa EMS (Sokoine) na (JKN) Nyerere tulikuwa na siku za kuomboleza ambazo hazikuwa public holidays. Kwani hao viongozi wakuu wameongoza misiba mingapi, je ilikuwa ya kitaifa?
 
Msiba w kitaifa ni upi? Ni kweli kuna mkanganyiko kwenye hili. Labda serikali ina miongozo yake au inategemea nani yuko madarakani? Kwa hili la Arusha kwa mfano sijasikia bendera yetu inarukaje, nilidhani kwa misiba ya kitaifa bendera huruka nusu mlingoti kwa siku tajwa.
Word!
 
Back
Top Bottom