Tukiacha ushabiki wa kivyama na Unafiki, Hoja ya Spika haijajibiwa

Tukiacha ushabiki wa kivyama na kujipendekeza (unafiki), Licha ya kila mtu kujitokeza kujaribu kujibu hoja ya Spika Ndugai ama kuizungumzia hoja hiyo, na hata Serikali (Rais) ameitisha mkutano wa kidola nikidhani anajibu hoja, badala yake wamejikuta wanamjadili Ndugai ama kumdhihaki ama kumdhalilisha tu, hoja ya Spika Job Ndugai haijajibiwa hata chembe, na ina nguvu kubwa. Hoja ya Ndugai si kwamba ina nguvu za kitaasisi tu, bali ni hoja inayohatarisha madaraka ya Rais, kwasababu kuu mbili,

Mosi: Liko kundi kubwa la Watanzania waliopewa jina la masikini na utawala wa John Magufuli, wakaaminishwa kuwa Rais Magufuli alikataa kukopa popote duniani tangu aingie madarakani hadi anafariki, na kwamba aliwagomea wazungu kwakuwa ni mabeberu waliotaka kupora raslimali zetu. Hawa waliaminishwa ujinga kuwa miradi yote nchini inajengwa kwa pesa yetu wenyewe.

Hili kundi utaliambia nini leo ukianza kukopa kwa uwazi na kutangaza hivi kila mkopo, bila kwanza kulipa elimu kuwa Magufuli katika utawala wake alikopa kimyakimya mikopo mikubwa ya kibiashara iliyovunja rekodi ya mikopo nchini? Kosa kubwa ambalo Rais Samia alifahya ni pale alipoingia madarakani akataka kuwawin makundi yote masikini na wenye akili, akasema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Ni wazi hili kundi la masikini litamuunga mkono mtu yoyote atakayekosoa mikopo yenu.

Pili: Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 63(2) nanukuu; Ibara ya 63 (2) "Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwaniaba ya wananchi, kuisimamia na KUISHAURI Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii."

Kwa ibara hii ya 63 (2), Spika Ndugai ametimiza wajibu wa kikatiba wa Bunge katika kuishauri serikali, Kwamaoni yangu Spika hajakosea chochote katika kauli yake kuhusu serikali kuacha kukopa. Ametimiza matakwa ya kikatiba kama mkuu wa muhimili,

Ukiacha wajibu wa kibunge kama Spika, Job Ndugai kama rais wa Tanzania ametumia ibara ya 18 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa maoni yake. Ni sheria ipi Tanzania inayomzuia mtu kutoa maoni yake, ama kukosoa serikali?

Na Yericko Nyerere

View attachment 2069920
View attachment 2069921
Huyu yericho kama kawaida ni mpotoshaji wa ukweli. Inaelekea ndio biashara yake kuna watu wanamlipa.
Kwanza hakuna kundi lililoaminishwa magufuli hakopi. Magufuli alikua na miradi ya kimkakati ambayo wakopeshaji hawako tayari kukukopesha wanaona ni ya kujikomboa kiuchumi. Walipoona tunaanza na hela zetu wenyewe ndio yakajitokeza mabenki tukakopa kwao.
Tofauti na magufuli samia anakopa ovyo bila mkakati. Anakopa ovyo hadi hela za kujenga madarasa kitu wakati wa magufuli tunafanya wenyewe. Chini ya magufuli alijenga moyo wa kujitegemea kwa kuhakikisha anakata unyonyaji wa wawekezaji na kuhakikisha kodi inalipwa. Chini ya samia ni kurukia mikopo yoyote akioneshwa na mabeberu.
Muelekeo tutakopa hadi hela ya kula sikukuu na kushona nguo za sikukuu toka ubeberuni chini ya samia😂
 
SIYO KWELI KWAMBA RAIS SAMIA ANAKOPA BILA MIKAKATI. Tujaribu kuwa waungwana kidogo hata kama hatumpendi kiongozi wetu au chama chake. Kwa mfano, mkopo wa UVIKO-19 fedha zimepelekwa kwenye Halmashauri kujenga madarasa (nani alipendezwa kuona watoto wetu walivyojazana madarasani achia mbali kukaa chini, upungufu wa vyoo n.k.), vituo vya afya, barabara vijijini. Kuboresha elimu, afya na miundombinu ya vijijini siyo mkakati kweli, labda mimi nina uelewa mdogo kwenye dhana nzima ya mikakati ya maendeleo. Tutafakari tafadhali
 
Back
Top Bottom