Tukiacha siasa shule za kata kuwa kama St. Francis Girls Mbeya

Ualimu ukiwekewa mazingira mazuri na mafao.mazuri automatically wenye sifa bora watakimbilia huko; automatically wenye sifa dhaifu watajikuta wanatafuta kazi nyingine za kufanya. Serikali iweke minimum wage ualimu sekondari kwa mfano iwe TZS 2.5 m/= uone kama the best hawajelekea ualimu. Tatizo lililopo ni mazingira na mishahara duni.
mtu apige div1 pts 7 akimbilie ajira ya ualimu ambayo anaearn hardly laki 3 kwa mwezi? Ni chizi pekee ndio atapenda ualimu.
 
Umoengea point sana...

Hua wanachukua watoto ambao wana uelewa wa hali ya juu sana pekee... hawachukui wenye uelewa hafifu hata siku moja...

Wangekua wanachukua watoto wamatabaka yote mpaka zero zingekuwepo...

Cc: mahondaw
Wivu tu.
 
Ndio capacity ya facilities zao ulitaka wafanyeje labda?
Wafanye rondom selection Ili Kila mtu awe na chance sio kufanya mchujo kàma usaili wa kazi
Hapo ndio tutajua kama waalimu wao au mazingira ya kujifunzia ndio yataleta hizo single digits zote kiufupi haiwezekani

Ndio maana hata shule za serikali zilixofanya vizuri na kutoa watoto walioongoza nazo ni walewale kwenye matokeo ya darasa la saba wanachukua top ten Kila mkoa kwa jinsia zote afu wanawapanga shule za nzumbe,ilboru Tabora girls nk nk
Baada ya hapo wanachagua daraja linalofuata wanawapeleka bweni wao wanaita shule za kitaifa za bweni kawaida then grade 3 na vilaza wengine wanabaki shule za kata

Kwa hiyo kwa mantiki hii lazima kutakuwa na ufaulu tofauti hata mm nilichaguliwa kwa mazingira hayo hayo afu kipindi hicho mkifika sekondari wanawapanga tena kwenye madaraja A Hadi D nk nk kulingana na ufaulu na matokeo ya kidato cha pili
 
Kati ya hao wanafunzi 90 huenda tusipate "mjasiriamali" hata mmoja. Mjasiriamali ni mtu anayewekeza muda na nguvu zake kutatua tatizo au matatizo fulani ndani ya jamii yake.

Naijua vema elimu yao hao watu. Darasani A+ ila nje ya darasa zero kabisa. Zero socialization, zero maarifa binafsi, zero everything isipokuwa principles za vitabuni. Sana sana asilimia kubwa hapo wataishia kuajiriwa (siwaombei hivyo ila ndiyo ukweli mchungu).

Siungi mkono watu wa ufaulu fulani kwenda kusomea fani fulani. Mfano; wasiofaulu vizuri kwenda ualimu au upolisi. Kinyume chake pia siyo sahihi. Kusema waliofaulu sana ndiyo wakawe walimu!

Kigezo cha kwanza kiwe passion. Mtu achague mwenyewe nini afanye (ilimradi awe na vigezo vingine) vya msingi.
Naunga mkono hoja, Mimi kwa Tz wala sibabaiki na hizi sijui A+ maana inabidi tuambiwe hata wale wa mwanzo wako wapi, wanafanya nini, elimu yetu hii ya ufaulu kwa wingi haina faida katika hali halisi. Juzi nilikuwa namsikia yule tajiri Musk sijui anasema watoto wake kafungua shule yake ya family anawafundisha masomo yote ila kikubwa problem solving, mbona wenzetu huko majuu vijana wakitoka wanabuni biashara mpya sio kuigana. ikotokea mtu kaiga basi anaboresha zaidi sio copy paste.
 
Na muwaambie mapema hao vipanga wenu huu ni ukweli mchungu Ili waje kupata status kitaa ni lazima wapate pesa vinginevyo watadharirika
Pili wao kama vipanga kazi yao ni kuwatumikia na kutumikishwa na wasio vipanga,Ili ushinde ubunge lazima pesa unless ubebwe kwa nguvu la sivyo utadharirika
 
ST. Francis Girls secondary school Mbeya ina Division one za point saba 80 kati ya wanafunzi 90 darasani, Kumi waliobaki wana diviosion one ya point nane na tisa

Kwa ufupi shule za wakatoliki hasa hawa masister ni shida ni balaaa

Darasa nzima linapiga Single digit yaani division one ya point saba mpaka tisa

Nasikia hata ile Canossa ni shule ya masister wa kikatoliki sina hakika bali imetoa mwanafunzi bora wa kike

Huu ni muda wa serikali kuchukua wenye ufaulu mkubwa na kwenda kufundisha shule za kata

Wanafunzi waliofauli vizuri kidato cha nne na sita walazimishwe kwenda kusomea ualimu

Hata ikiwezekana kwa viboko naunga mkono hoja
Mbona wewe hawakukulazimisha?
 
Naunga mkono hoja, Mimi kwa Tz wala sibabaiki na hizi sijui A+ maana inabidi tuambiwe hata wale wa mwanzo wako wapi, wanafanya nini, elimu yetu hii ya ufaulu kwa wingi haina faida katika hali halisi. Juzi nilikuwa namsikia yule tajiri Musk sijui anasema watoto wake kafungua shule yake ya family anawafundisha masomo yote ila kikubwa problem solving, mbona wenzetu huko majuu vijana wakitoka wanabuni biashara mpya sio kuigana. ikotokea mtu kaiga basi anaboresha zaidi sio copy paste.
Kwa jinsi elimu ya bongo ilivyo ngumu ukiona mwanafunzi "ana akili sana darasani" ujue kuna vitu vingi sana vya nje ya darasa anavitoa sadaka ili apate huo muda wa kuwa kipanga. Ndiyo sababu ukifuatilia utagundua kuwa "vipanga" wengi huishia kuajiriwa na "vilaza".
 
Na muwaambie mapema hao vipanga wenu huu ni ukweli mchungu Ili waje kupata status kitaa ni lazima wapate pesa vinginevyo watadharirika
Pili wao kama vipanga kazi yao ni kuwatumikia na kutumikishwa na wasio vipanga,Ili ushinde ubunge lazima pesa unless ubebwe kwa nguvu la sivyo utadharirika
Ukweli mchungu huu. Mgumu sana kumeza.
 
Wanachuja watoto wanaoingia pale kwa mtihani wa Interview waliouandaa wenyewe na wana viwango vyao vya ufaulu sasa ulitakaje mzee, wachukue wanafunzi bila kuwapima? Hakuna shule inafanya hivyo..naijua hiyo shule ndani njee acha tu, zungumzia discipline pia ni nguzo ya ufaulishaji watoto wanaopikwa pale wana discipline ya kutosha
Ila wakirudi kitaa uuuwi, mwendo wa vimini🤔🤔, hafu Yana shape aisee ....
 
Wanachuja watoto wanaoingia pale kwa mtihani wa Interview waliouandaa wenyewe na wana viwango vyao vya ufaulu sasa ulitakaje mzee, wachukue wanafunzi bila kuwapima? Hakuna shule inafanya hivyo..naijua hiyo shule ndani njee acha tu, zungumzia discipline pia ni nguzo ya ufaulishaji watoto wanaopikwa pale wana discipline ya kutosha
Naona unapatetea ila kiukweli wanachukua watt walio tayari na uwezo wao mkuu. Kama unasemea discipline mbona wasichukue wale Wa mwisho mwisho afu wakawape ivyo discipline unayosemea.
Kuna shule zinaendaga kuwafuta wale kumi bora kitaifa wasomee kwao bure ili wake kuongoza kwa six ili wawape sifa kwa mashule yao mkuu. Wawavute wengine ili wawapige
 
Kipindi nimeenda advance tulipangiwa na watoto kutoka hyo st fransis na marian girl's wote walikuwa na division one za nane, na tulipokuwa tubafanya mitihani walikuwa wanakuwa wa mwisho darasani na division three Hadi Necta. So kwangu hzo shule nyingi ni spoon feeding pia elimu ya saa inahitaji ubunifu na ku solve changamoto za kimazingira kuliko kupata ma A yote KWA ku cremisha
 
Wazee wa sembe na nyara za serikali au siyo.
Usikariri kuwa lazima wafanye hizo mambo mkuu ujiridhishe kwa hali uliyo nayo.
Mbona wapo wanaofanya halali na wanatoboa ama umekaririshwa.
You're just looking reasons to justify your condition. Mana binadamu hajawahi kubali kushindwa kwa hali aliyo nayo. Wengine tunasingizia kuwa hatuna network Mara serikali sijui haitoi ajira.ila muda huo huo wapo wanaotoboa huku umekaa na hali yako iyo .
 
Wewe unawafahamu vema. Wengi wanajidai hawaoni hili. Shule za serikali hazichuji wanaojiunga ila hizi sijui sent nani, nao wakianza kuchukua bila kuchuja, watu watabaki midomo wazi.
Serikali inatoa huduma KWA jamii hzo st nini sijui wako kibiashara zaidi
 
Kipindi nimeenda advance tulipangiwa na watoto kutoka hyo st fransis na marian girl's wote walikuwa na division one za nane, na tulipokuwa tubafanya mitihani walikuwa wanakuwa wa mwisho darasani na division three Hadi Necta. So kwangu hzo shule nyingi ni spoon feeding pia elimu ya saa inahitaji ubunifu na ku solve changamoto za kimazingira kuliko kupata ma A yote KWA ku cremisha
Ukimuozesha spoon feeding hatajua kunitafutia. Lazima MTT azoee kukomaa alone since at early ages hii mentality naipenda
 
Back
Top Bottom