Tukiacha siasa shule za kata kuwa kama St. Francis Girls Mbeya

seedfarm

Senior Member
Feb 9, 2020
123
1,000
ST. Francis Girls secondary school Mbeya ina Division one za point saba 80 kati ya wanafunzi 90 darasani, Kumi waliobaki wana diviosion one ya point nane na tisa

Kwa ufupi shule za wakatoliki hasa hawa masister ni shida ni balaaa

Darasa nzima linapiga Single digit yaani division one ya point saba mpaka tisa

Nasikia hata ile Canossa ni shule ya masister wa kikatoliki sina hakika bali imetoa mwanafunzi bora wa kike.

Huu ni muda wa serikali kuchukua wenye ufaulu mkubwa na kwenda kufundisha shule za kata

Wanafunzi waliofauli vizuri kidato cha nne na sita walazimishwe kwenda kusomea ualimu

Hata ikiwezekana kwa viboko naunga mkono hoja
 

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,300
2,000
Mkuu wana ccm wengi tuna Division one za point saba

Sasa wewe kama ulishindwa kupata point saba tatizo ni kichwa chako


Tatizo ni kichwa, Narudia tena tatizo ni kichwa chako

Unakula maembe unategemea point saba

Tatizo lishe ya utotoni,
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,413
2,000
Ualimu ukiwekewa mazingira mazuri na mafao.mazuri automatically wenye sifa bora watakimbilia huko; automatically wenye sifa dhaifu watajikuta wanatafuta kazi nyingine za kufanya. Serikali iweke minimum wage ualimu sekondari kwa mfano iwe TZS 2.5 m/= uone kama the best hawajelekea ualimu. Tatizo lililopo ni mazingira na mishahara duni.
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,626
2,000
Elimu ya msingi ijumushe o level sekondari baada ya hapo 70% waende vyuo vya ufundi 30% Alevel then 20%:Diploma na 10% vyuo vikuu.
 

Mbeya City Spurs I

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
276
1,000
Kati ya hao wanafunzi 90 huenda tusipate "mjasiriamali" hata mmoja. Mjasiriamali ni mtu anayewekeza muda na nguvu zake kutatua tatizo au matatizo fulani ndani ya jamii yake.

Naijua vema elimu yao hao watu. Darasani A+ ila nje ya darasa zero kabisa. Zero socialization, zero maarifa binafsi, zero everything isipokuwa principles za vitabuni. Sana sana asilimia kubwa hapo wataishia kuajiriwa (siwaombei hivyo ila ndiyo ukweli mchungu).

Siungi mkono watu wa ufaulu fulani kwenda kusomea fani fulani. Mfano; wasiofaulu vizuri kwenda ualimu au upolisi. Kinyume chake pia siyo sahihi. Kusema waliofaulu sana ndiyo wakawe walimu!

Kigezo cha kwanza kiwe passion. Mtu achague mwenyewe nini afanye (ilimradi awe na vigezo vingine) vya msingi.
 

keisangora

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
1,596
2,000
Huwa wanawachuja wanachukua tu cream tu hapo shuleni kwao.

Hebu wachukue wanafunzi bila ya kuwachuja kwa mitihani afu tuone kama wataweza kupata Hayo matokeo.

Hii MIE hainishtui ni sawa unachukua matajiri wenye dola bilioni moja plus unawapatia nchi yao. Hapo unategemea nini hivi jamani.
Yaani Hao madada wakatoliki wasichuje watoto wanaoenda huko shuleni kwao tuwaone walivyo wababe Wa kuwafundisha Hayo watt sasa.

Yaani hill hata halinitishi MIE najua wanachuja sana tena sana.

Mwalimu mzuri anafundisha kilaza mpaka anaelewa na kufaulu kwa alama za juu kabisa
 

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
1,664
2,000
ST. Francis Girls secondary school Mbeya ina Division one za point saba 80 kati ya wanafunzi 90 darasani, Kumi waliobaki wana diviosion one ya point nane na tisa..
sio rahisi, St. Fransic wanafanya biashara ya huduma, ambapo wamewekeza pesa nyingi ili wapate faida. Wakati shule za kataa hawafanyi biashara bali wanatoa huduma ya bure. Kwa hiyo hilo swala haliwezekani
 

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,300
2,000
Division one yako ya 7 imekusaidia nn, au una Chet chenye dvsn one siyo kichwa kilichopata dvsn one maana unalalamika mno inaonekana dvsn zero wanakukimbiza kwenye real life la kitaa
Mimi furaha yangu na kukimbiza kwangu ni pale Chadema inaposhindwa uchaguzi

Mimi nikiona Chadema wanapata taabu na kutaabika kwa kutandikwa mabomu na fimbo ndio furaha yangu na kukimbiza kwangu

Wewe kilaza unadhani bila Division one kali JPM angesoma udsm

Nyie wenye division 2 mpaka 4 ndio janga la Taifa

Nikisikia Chadema imepata hata kura moja huwa naumia sana sana na kuona kila mtu amenizidi maisha

Uchaguzi wa mwaka jana mmebaki Facebook na Twittet tu hapo nina furaha isiyo na kifani na ninatembea kifua mbeleeeeeeeeee na kupeperusha bendera ya ccm uwanjani kwangu

Kwa akili hizi hakika mtaishia kulia lia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom