Tukazanie Sheria za kulinda Maadili sio za kuwaadhibu wavunja Maadili

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,489
40,991
Kuna watu wanafoka kuhusu mambo yasiyopendeza, mambo yasiyo ya kimaadili, mambo ya dhambi. Na kwao fikra zao ni kuwa kukiwa na adhabu kali mambo hayo yataisha.

Niwaulizeni, Kuna nchi yoyote inayoruhusu ujambazi? Kuna nchi isiyo na sheria kali dhidi ya majambazi? Je, kutokana na sheria hizo, ujambazi umeisha?

Kuna nchi inaruhusu mauaji? Pamoja na sheria kali dhidi ya wauaji, mauaji yamekoma?

Kuna nchi ambayo ina katiba inayoruhusu viongozi au Serikali kuwaua wanaowahoji au wapinzani wao wa kisiasa? Wasiojulikana waliruhusiwa na sheria yoyote? Akina Lisu walitwangwa risasi na wasitaka kuhojiwa, kulikuwa na sheria inayoruhusu kufanya hivyo?

Tangu sheria ya Mungu ije Duniani, maovu yamekoma?

Sheria inatusaidia tu kuyajua yaliyokatazwa, na kujenga woga. Lakini kwa mhalifu, sheria haifanyi moyo wake ubadilike bali anakuwa tu mwoga, na akipata mazingira ya usiri, atatenda uovu wake.

Tunafahamu hata baadhi ya viongozi wetu walivyo wevi na wala rushwa licha ya mambo hayo kuzuiwa na katiba na sheria zetu mbalimbali, tena wanaapa na kuapa, lakini wakiwa wakiwa kwenye mazingira yanayoweza kutekeleza uovu wao, wanafanya, tena kwa kufuru, kwa sababu uovu ni asilia yao, upo katika maisha na nafsi zao. Sheria na hata nafasi zao za uongozi hazijaweza kuwabadilisha chochote. Kinachobadilika ni mara ya kwanza walikuwa wevi wavaa tshirt, sasa ni wevi wavaa suti.

Tatizo ambalo watu wamekuwa wakiliongelea sana sasa hivi la ushoga, haliwezi kuondolewa kwa sheria za kuwaadhibu mashoga bali kwa sheria na miongozi inayozuia utengenezaji wa mashoga. Na hata tukifanya hayo, tutapunguza, lakini hatuwezi kujidanganya kuwa hatutakuwa na shoga hata mmoja.

Leo hii, hata kama Serijali ikatangaza kuwa ushoga ni halali Tanzania, usitegemee kuwa wale ambao siyo mashoga watabadilika na kuwa mashoga. Haiwezi kutokea. Kitakachotokea ni wale ambao tayari ni mashoga, watafanya mambo yao kwa uhuru, lakini siyo sheria ndiyo itakayokuwa imewafanya kuwa mashoga.

Kama tunataka kuondokana na tabia hizi chafu, ni lazima kukazania kwenye malezi. Mtu ambaye amekuwa shoga tangu akiwa mdogo, yupo shuleni, hutaweza kumbadilisha kwa sheria akiwa mtu mzima. Na hata kwenye malezi, siyo lazima na haifai kuwatamkia watoto neno hili kila mara. Neno linalotamkwa kila mara, hata kwa ubaya baadaye huonekana la kawaida, na watu wengine hasa watoto kwenye umri fulani hupenda kujaribu kitu kinachokatazwa kila mara.

Jambo la muhimu ni malezi ya watoto na kuwajengea mazingira yanayozuia wao kuwa katika mazingira ya kujifunza uchafu huo wakiwa majumbani, na zaidi wakiwa mashuleni, hasa kwenye umri mdogo.

Kuna matukio kadhaa ambayo yamewahi kuripotiwa katika baadhi ya shule, hasa za msingi, watoto wadogo kufanyiwa uchafu wa aina mbalimbali na walimu wao, ikihusisha kuwashika maeneo yao ya siri, kuwaingilia kinyume cha maumbile na kuwaingilia kwa njia za kawaida (kisheria ni ubakaji). Sasa kunapokuwa na tishio la kuwajengea watoto tabia hizi mbaya, Serikali kwa kupitia Wizara ya Elimu na Wizara ya Watoto ije na mwongozo juu ya mahusiano ya walimu na watoto.

Mapendekezo:

1) Madarasa yote, ofisi za Walimu na kumbi, kuwekwe CCTV camera.

2) Mwalimu asiruhusiwe kukutana na mwanafunzi yeyote nje ya maeneo ya wazi ya mazingira ya shule (nje ya majengo), madarasani na ofisini.

3) Mwalimu asiruhusiwe kukutana na mwanafunzi yeyote katika eneo lolote, na mwanafunzi mmoja akiwa pekee yake. Lazima akutane nao katika makundi.

4) Mwalimu atakayepatikana kumtendea uchafu mtoto yeyote, afungwe maisha.

5) Shule ambayo mwalimu au walimu wake watathibitika kuwafanyia uchafu wanafunzi wao, itangazwe wazi kwenye vyombo vya umma, na hiyo shule ipigwe faini kubwa kwa kushindwa kufuatilia tabia za walimu wake.

6) Wakaguzi wa Elimu, miongoni mwa kazi zao, ihusishwe kupitia taarifa zote zilizopatikana kwenye CCTV, na zile zinazoashiria mapungufu ya maadili kwa walimu zifikishwe kwa wamiliki wa shule na Serikalini kwaajili ya kuchukua hatua.

KUMBUKA
Asiye shoga, hawezi kuwa shoga kwa sababu kuna nchi fulani inaruhusu ushoga. Halikadhalika, aliye shoga hawezi kuacha kuwa shoga kwa sababu kuna sheria kali dhidi ya ushoga, atakachofanya ni kutenda mambo yake kwa kificho zaidi, lakini siyo kuacha.
 
Huwezi kulinda maadili bila kuwaadhibu wavunja-maadili. Kujenga maadili na kuadhibu ni sawa kabisa na pande mbili za jero.
 
Kama tunataka kuondokana na tabia hizi chafu, ni lazima kukazania kwenye malezi. Mtu ambaye amekuwa shoga tangu akiwa mdogo, yupo shuleni, hutaweza kumbadilisha kwa sheria akiwa mtu mzima. Na hata kwenye malezi, siyo lazima na haifai kuwatamkia watoto neno hili kila mara. Neno linalotamkwa kila mara, hata kwa ubaya baadaye huonekana la kawaida, na watu wengine hasa watoto kwenye umri fulani hupenda kujaribu kitu kinachokatazwa kila mara.
Naunga mkono hoja, prevention is better than cure!.
P
 
Sheria za maadili zipo.

Ila uadilifu wa kweli unapatikana au unatokana na mafundisho ya kiroho,

Hofu juu ya Mungu ndio chanzo kikuu Cha uadilifu kwa binaadamu, ndipo Sheria zinafuata.

Katika ulimwengu wa sasa tunaona wasomi; Maprofesa na madokta walio bobea lakini hawana hofu ya Mungu ni hatari sana.

Sio tu kuwa na Sheria bali tukitaka kutengeneza watu waadilifu basi tuanze kuwaomba viongozi wa dini watengeneze watu waadilifu hapo tutakuwa tumezuia zaidi.
 
Tatizo lipo kwenye nafsi
Tatizo lipo ndani
Tatizo lipo rohani mwa watu
Kuna msemo unasema 'bloodily fool' maana yake upumbavu unakuwa kwenye blood mainstream
Mtoto amezaliwa mwizi since day One ataacha kuiba akiwa mzee??
 
Kuna watu wanafoka kuhusu mambo yasiyopendeza, mambo yasiyo ya kimaadili, mambo ya dhambi. Na kwao fikra zao ni kuwa kukiwa na adhabu kali mambo hayo yataisha.

Niwaulizeni, Kuna nchi yoyote inayoruhusu ujambazi? Kuna nchi isiyo na sheria kali dhidi ya majambazi? Je, kutokana na sheria hizo, ujambazi umeisha?

Kuna nchi inaruhusu mauaji? Pamoja na sheria kali dhidi ya wauaji, mauaji yamekoma?

Kuna nchi ambayo ina katiba inayoruhusu viongozi au Serikali kuwaua wanaowahoji au wapinzani wao wa kisiasa? Wasiojulikana waliruhusiwa na sheria yoyote? Akina Lisu walitwangwa risasi na wasitaka kuhojiwa, kulikuwa na sheria inayoruhusu kufanya hivyo?

Tangu sheria ya Mungu ije Duniani, maovu yamekoma?

Sheria inatusaidia tu kuyajua yaliyokatazwa, na kujenga woga. Lakini kwa mhalifu, sheria haifanyi moyo wake ubadilike bali anakuwa tu mwoga, na akipata mazingira ya usiri, atatenda uovu wake.

Tunafahamu hata baadhi ya viongozi wetu walivyo wevi na wala rushwa licha ya mambo hayo kuzuiwa na katiba na sheria zetu mbalimbali, tena wanaapa na kuapa, lakini wakiwa wakiwa kwenye mazingira yanayoweza kutekeleza uovu wao, wanafanya, tena kwa kufuru, kwa sababu uovu ni asilia yao, upo katika maisha na nafsi zao. Sheria na hata nafasi zao za uongozi hazijaweza kuwabadilisha chochote. Kinachobadilika ni mara ya kwanza walikuwa wevi wavaa tshirt, sasa ni wevi wavaa suti.

Tatizo ambalo watu wamekuwa wakiliongelea sana sasa hivi la ushoga, haliwezi kuondolewa kwa sheria za kuwaadhibu mashoga bali kwa sheria na miongozi inayozuia utengenezaji wa mashoga. Na hata tukifanya hayo, tutapunguza, lakini hatuwezi kujidanganya kuwa hatutakuwa na shoga hata mmoja.

Leo hii, hata kama Serijali ikatangaza kuwa ushoga ni halali Tanzania, usitegemee kuwa wale ambao siyo mashoga watabadilika na kuwa mashoga. Haiwezi kutokea. Kitakachotokea ni wale ambao tayari ni mashoga, watafanya mambo yao kwa uhuru, lakini siyo sheria ndiyo itakayokuwa imewafanya kuwa mashoga.

Kama tunataka kuondokana na tabia hizi chafu, ni lazima kukazania kwenye malezi. Mtu ambaye amekuwa shoga tangu akiwa mdogo, yupo shuleni, hutaweza kumbadilisha kwa sheria akiwa mtu mzima. Na hata kwenye malezi, siyo lazima na haifai kuwatamkia watoto neno hili kila mara. Neno linalotamkwa kila mara, hata kwa ubaya baadaye huonekana la kawaida, na watu wengine hasa watoto kwenye umri fulani hupenda kujaribu kitu kinachokatazwa kila mara.

Jambo la muhimu ni malezi ya watoto na kuwajengea mazingira yanayozuia wao kuwa katika mazingira ya kujifunza uchafu huo wakiwa majumbani, na zaidi wakiwa mashuleni, hasa kwenye umri mdogo.

Kuna matukio kadhaa ambayo yamewahi kuripotiwa katika baadhi ya shule, hasa za msingi, watoto wadogo kufanyiwa uchafu wa aina mbalimbali na walimu wao, ikihusisha kuwashika maeneo yao ya siri, kuwaingilia kinyume cha maumbile na kuwaingilia kwa njia za kawaida (kisheria ni ubakaji). Sasa kunapokuwa na tishio la kuwajengea watoto tabia hizi mbaya, Serikali kwa kupitia Wizara ya Elimu na Wizara ya Watoto ije na mwongozo juu ya mahusiano ya walimu na watoto.

Mapendekezo:

1) Madarasa yote, ofisi za Walimu na kumbi, kuwekwe CCTV camera.

2) Mwalimu asiruhusiwe kukutana na mwanafunzi yeyote nje ya maeneo ya wazi ya mazingira ya shule (nje ya majengo), madarasani na ofisini.

3) Mwalimu asiruhusiwe kukutana na mwanafunzi yeyote katika eneo lolote, na mwanafunzi mmoja akiwa pekee yake. Lazima akutane nao katika makundi.

4) Mwalimu atakayepatikana kumtendea uchafu mtoto yeyote, afungwe maisha.

5) Shule ambayo mwalimu au walimu wake watathibitika kuwafanyia uchafu wanafunzi wao, itangazwe wazi kwenye vyombo vya umma, na hiyo shule ipigwe faini kubwa kwa kushindwa kufuatilia tabia za walimu wake.

6) Wakaguzi wa Elimu, miongoni mwa kazi zao, ihusishwe kupitia taarifa zote zilizopatikana kwenye CCTV, na zile zinazoashiria mapungufu ya maadili kwa walimu zifikishwe kwa wamiliki wa shule na Serikalini kwaajili ya kuchukua hatua.

KUMBUKA
Asiye shoga, hawezi kuwa shoga kwa sababu kuna nchi fulani inaruhusu ushoga. Halikadhalika, aliye shoga hawezi kuacha kuwa shoga kwa sababu kuna sheria kali dhidi ya ushoga, atakachofanya ni kutenda mambo yake kwa kificho zaidi, lakini siyo kuacha.
Mkuu, Hongera sana kwa kulitolea ufadanuzi makini suala hili. Hili jambo la mashoga lipo kitambo sana, toka wakati wa Sodoma na Gomola lakini halikupata airtime kama wakati huu. Najaribu kutafuta nini kimejiri hadi ushoga leo ni HABARI na huko nyuma ingawa lilikuwepo lakini haikuwa HABARI. Jiwe limedondokea wapi??
 
Back
Top Bottom