nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
[h=2][/h]Ijumaa, Agosti 17, 2012 10:03 Na Balinagwe Mwambungu
IMERIPOTIWA kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapendekeza kuanzishwa kwa Baraza la Seneti ambali litakuwa na marais wastaafu na wajumbe wengine wa kuchaguliwa. Taarifa hio zikiwanukuu baadhi ya wanumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Halmshauri Kuu (NEC) ya CCM, zilieleza kwamba imependekezwa kwamaba mfumo wa sasa wa Bunge ufumuliwe na badala yake kuwe na Mabaraza MawiliBunge na Seneti.
Sababu ya kutaka kulifumua Bunge, hazikuelezwa na sababu za kutaka liwepo Baraza la Seneti hazina mashiko. Inaelezwa kwamba siku za usoni taifa litakuwa na marais wengi wastaafu, hivyo liundiwe Baraza la Seneti, ambamo wataingia kwa kuwa walikuwa marais, lakini pia inapendekezwa kwamba watachakuwamo wajumbe wengine wa kuchaguliwa.
Inaelezwa kwamba nchi kuwa na mabaraza mawili si jambo jambo geni na inatolewa mfano wa Marekani na Uingerezaambako kuna Baraza la Wawakilishi (House of Representatives) na Senatena Uingereza ambako kuna House of Commons na House of Lords. Mfumo huu haukubuniwa kwa sababu ya kutaka kukidhi matakwa ya kundi fulani, bali imetokana na historia ya nchi hizo.
Lakini si nchi hizo mbili zenye mfumo huu wa kuwa na mabunge mawili. Nigeria ina Baraza la Seneti, India ina mabaraza mawili ukiachia mbali mabunge ya majimbo. Kuundwa kwa mabaraza hayo kulitokana na sababu maalumu zilizosabisha kuwapo kwa mabaraza hayo.
Tuchukue mfano wa Marekani ili kuelezea dhana ya mabaraza mawili vizuri. Baraza la Wawakishi mara nyingine huitwa Congress, wajumbe wake huchaguliwa kutoka kila jimbo kufuatana na wingi wa watu. Hawa huchaguliwa kila baada ya miaka miwili (mid-term elections).
Kwahiyo, jimbo moja lenye watu wengi linaweza likawa na wawakilishi zaidi ya mmoja. Jimbo la California ndilo lenye watu wengi zaidi na lina Wawakilishi 53, kati ya wawakilishi 435. Na Baraza la Seneti (Upper House), lina maseneta 100, wawiwili kutoka kila jimbo (state) wanatumikia kwa muda wa miaka sita. Marekani ina jumla ya majimbo 48.
Kwa upande wa Uingereza, kutokana na historia yake kwamba ilitawaliwa kifalme, kulitokea mapinduzi na makabwela (common people) wakaunda Bunge lao (House of Commons) watawala wakabaki na Bunge na House of Lords. Wajumbe wake ni wateule wa kifalme.
Ni sababu zipi ambazo CCM wanataka kujenga mabaraza ya kitabaka ambayo nchi yetu ilikwisha yakataa kabla na baada ya uhuru? Kwamba kutakuwa na marais wengi wastaafu kwahiyo tuwaundie baraza, hapana. Tukitaka kupunguza idadi ya marais wastaafu, ama tuongeze umri si kupunguza, kama kigezo cha mtu kugombea urais ili kupunguza gharama za marais wastaafu au tuongeze muda wa kushika madarakabadala ya miaka mitano, tufanye minane (8), ili kumpa muda wa kutosha kutekeleza aliyokusudia kufanya, hata kama atakuwa rais wa muhula mmoja.
Kwanza, katika mfumo wa sasa wa vyama vingi, tukiwapeleka marais wastaafu bungeni, wataumbuka. Maseneta wenzao watawabwatukia na kuwakosoa kutokana na mambo ambayo hawakuyasimamia vizuri. Hadhi ya urais itakuwa wapi? Tukifanya hivyo tutakuwa hatuwatendei haki. CCM walisema wanakusudia kuwaengua marais wastaafu na kuwaundia Baraza la Ushauri la CCM, hapana shaka wameona kuwa ni kuongeza gharama, sasa wanataka gharama hizi wazibebe walipa kodi. Hapana.
Itakuwa busara kama itaamuliwa kwamba tuwe na mabaraza matatuBaraza la Wawakilishi (Zanzibar), Bunge la Tanganyika na Bunge la Muungano ambalo litakuwa na idadi ndogo wa wawakilishimmoja kutoka kila mkoa na watashughulikia mambo ya Muungano tu.
Viongozi wastaafu, wako juu ya Bunge au Baraza la Wawakilishii. Rais yeyote, ikiwa anataka, anaweza kuomba ushauri juu ya jambo lolote kutoka kwa viongozi wastaafu kuanzia wakuu wa wilaya, mikoa, mawaziri, mawaziri wakuu na marais na sio kuwaundia baraza maalumu.
Dhana ya kutaka Katiba mpya itamke idadi ya Wabunge ni njema, lakini pia itamke idadi ya Wizara, ili rais asiweze kuwapa vyeo marafiki, kama ilivyotokea kwa wanamtandao.
Katiba vile vile itamke kipindi cha uongozi wa kitaifa, lakini isimzuie mwakilishi wa wananchi kuchaguliwa tena na tena kama kazi yake ni nzuri na ikiwa wananchi waliomchagua, wanaona bado anafaa kuwa mwakilishi wao.
Kutamka kipindi cha ubunge, ni kuwanyanganya wananchi haki yao ya kumchagua mwakilishi wanaye mpenda. Na kama Bunge kila mara linakuwa na kuwa wabunge wengi wapya halinogi, kwa sababu wabunge wapya kwa kipindi fulani, watakuwa wanajifunza kutoka kwa wabunge wakongwe.
Katiba pia isitamke umri wa mgombea ubunge au uwakilishi, kwa kuwa miaka ya mtu kupiga kura ni 18, lakini iweke ukomo wa umri wa wawakilishi wetu nchi za nje. Katika vipindi viwili tumeshuhudia watu waliostaafu utumishi kutokana na umri, wanateuliwa kuwa mabalozi wetu nchi za nje. Lakini itapendeza pia kama Katiba itambana rais na kutamka kwamba idadi ya mabalozi wanasiasa, iwe ni nusu ya watumishi kutoka serikalini.
Aidha, Katiba mpya pia itamke kwamba wakuu wa majeshi na vyombo vya Ulinzi na Usalama, majaji wastaafu, hawataruhusiwa kugombea urais. Wakitaka kugombea wafanye hivyo kabla ya kustaafu kwa maana ya kwamba itabidi wajiudhuru nyadhifa zao.
Katiba mpya itamke uwepo wa majimbo (hivi sasa mikoa) ambao yataongozwa na magavana wa kuchaguliwa. Hawa watabuni mipango ya maendeleo ya majimbo yao, watasimamia utawala na watakuwa na Mamlaka ya Kodi (TRA) itakusanya kodi ya mkoa. Hazina Kuu itakuwa inagawiwa sehemu ya mapato toka kila mkoa kutokana na ukubwa wa mapato. Katiba mpya iwe ufunguo wa maendeleo ya wananchi badala ya kuwakikwazo. Hivi sasa sehemu kubwa ya fedha inayohitajiwa kwa ajili ya maendeleo, inatoka Hazina. Tujifunze toka India.
Katiba mpya itamke kutakuwa na aina moja tu ya uwakilishiuwakilishi wa kuchaguliwa. Hii itakuwa imefuta ubaguzi wa kijinsiakuipendelea jinsia moja kwa kuipa nafasi maalumu.
Katiba itamke rasmi kwamba uchaguzi wowote, katika ngazi zote, ikiwa ni pamoja na ule wa rais, unaweza kupingwa mahakamani, isipokuwa uwekewe utaratibu maalumu kuepusha nchi kuingia katika mgogoro wa muda mrefu.
Hitimisho. Viongozi wetu wasiendelee kuigawa nchi katika vipandevipande kwa kukidhi matakawa ya kisiasa. Sehemu kubwa ya bajeti yetutakriban asilimia-----inatumikakwa mambo ya utawala na asilimia tu ndio bajeti ya maendeleo. Wakati umefika sasa kufanya mageuzi ya
na kuubadili mfumo wa sasa, ili nchi yetu ipate kusonga mbele kiuchumi, kijamii na kimaendeleo. Tuondokane na mfumo unaowatumikisha wananchi, tuingie katika mfumo unaowatumikia wananchi. Tutapiga hatua kubwa mbele.