Tukaribishe makundi mengine ya uwekezaji katika Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,604
8,743
Mradi wa Bagamoyo ni drama za ajabu sana huwezi kupata faida kwenye mkataba kama unaongea na mwekezaji mmoja tu. Kama China na Oman wanajua wako peke yao serikali itakuwa kwenye wakati mgumu sana kuweza kujadili mkataba mzuri. Hivyo ushauri wangu ni kutangaza upya uwekezaji maana siku hizi wawekezaji wameongezeka sana

1. G7 nchi tajiri kuliko zote Duniani wameamua kuanzisha shirika la uwekezaji kushindana na China

2. Tunawa kukopesha na kufanya wenyewe bila masharti

Kitu kingine hii bandari haijitaji ukubwa kana kwamba hatuna bandari nyingine maaneo hayo hivyo gharama za mradi zinaweza kupungua sana kama tukigawa mizigo kati ya hizi bandari mbili chini ya serikali yaani ni kama stendi ndogo na kubwa kutokana na ukubwa wa mizigo.

Hakuna sababu ya kukuza mradi sana wakati tayari tuna bandari na reli dar hii iwe ya meli kubwa tu tutashangaa gharama zitashuka sana na tunaweza kukopa wenyewe. Uwekezaji mkubwa uwe kwenye industry park.

Kwenye hii park tusikubali china wawe pakee maana tunaweza kuwa na uwekezaji wa nchi za ulaya tukiweka uendeshaji wa china pekee watakuwa wana block hizi kampuni.
 
Mkuu huo mkataba wewe Binafsi umewahi kuuona na kuusoma?

Maana Mara nyingi linapo kuja suala la kujadiri Bandari ya Bagamoyo watu hutumia hisia zaidi sio kwa wanaopinga tu bali hata kwa wanao sapoti.
 
Mradi wa bagamoyo ilikuwa tuujenge kwa pesa yetu wenyewe kwa serikali kujenga bandari na makampuni binafsi kujenga miundombinu inayoendana na uwekezaji wa hiyo bandari.
 
Mkuu huo mkataba wewe Binafsi umewahi kuuona na kuusoma?

Maana Mara nyingi linapo kuja suala la kujadiri Bandari ya Bagamoyo watu hutumia hisia zaidi sio kwa wanaopinga tu bali hata kwa wanao sapoti.

Binafsi nadhani Watz tuna experience mbaya ya muda mrefu ya mikataba na wawekezaji.

Sidhani kama kuna mkataba ktk mradi ambao wawekezaji wanamiliki 100% of the shares utakaowaridhisha Watz.

..Ni afadhali TPA wawe na shares angalau 40% ktk two way ownership, au 30% ktk three way ownership, ili kuzuia kuibiwa na kujenga imani ya wananchi ktk mradi.

Cc Nguruvi3
 
Pengine ma Chadema yanaamini kua wao ni chama cha siasa cha upinzani lkn ukweli Mbowe Zitto ni Mkono wa Kushoto wa Mafisadi yalioko ndani ya CCM...Mbowe Zitto,JPM alikata Mirija yao kama ilivyokua kwa Mafisadi wengine,lkn kwasasa wote wanakula Pamoja,Nyumbu wameachiwa kelele tu
 
Back
Top Bottom