Tujuzane Restaurant za Dar zenye chakula na mazingira mazuri

Dharra

JF-Expert Member
Jun 23, 2017
1,661
2,930
Wakuu habari za siku ya leo.

Mimi hupenda sana siku za sikukuu ama baadhi ya weekend mida ya jioni nikiwa peke yangu kupata chakula katika migahawa mizuri na bora. Sehemu ninazopendelea sana ni pamoja na sea cliff (ile restaurant ipo location poa sana) na sometimes wanakuwa na live band pale, roof top restaurants za African Hotel, Holiday inn na Harbor view na zingine.

Kwa ambao wako na experiance tupeane info, ni wapi pengine kunakuwa na good food pamoja na friendly environment kwa mida ya Jioni?
 
Tupe na gharama za misosi huko ulikopita ili ttuvunje vibubu na sisi tukaoshe macho na kubadili menu

wala haitishi sana mkuu. Unavuta pizza yako unashushia na kitu Tuna salad na icecream la kokonoto. Buku 30 tu una enjoy
 
biriani wapi linapatikana kwa maeneo ya kariakoo

Sent using Jamii Forums mobile app
Biriani huwa ijumaa mkuu, chef pride lumumba au opposite na st Bernard hospital kuna nyumba zile za zamani wanapika hapo tamu sana, au mtaa wa livingstone na udoe kuna hotel ya wasomali tena wachagua kukaa chini kuufinya au kukaa kwenye kiti.
 
Nishaurini jamani. Bajeti yangu maximum 18,000 nataka nimtoe dinner girlfriend wangu weekend ijayo. Sijui niende restaurant gani.
 
Back
Top Bottom