Tujuzane mitaa hatari na salama katika miji mbalimbali hapa nchini

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,388
24,947
Habari wakuu...

Kutokana na hali ya usalama kwa ujumla wake hapa nchini kuna wakati tunajikuta tunakuwa katika maeneo tofauti tofauti katika harakati nzima za kimaisha na kutafuta riziki zetu kila iitwapo leo.

Wakati mwingine tumekuwa tunakatiza mitaa ambayo siyo salama kwa sababu ya ugeni au kutojua historia ya eneo hilo na hatimaye kuangukia mikononi mwa wahalifu, wezi, majambazi au vibaka na wakati mwingine tunaporwa mali hata kutolewa UHAI.

Cha kushangaza sana hata vyombo vya dola saa nyingine vinaogopa maeneo hayo hasa nyakati za usiku.

Kupitia huu uzi tusaidiane hapa kujua sehemu zile korofi au vijiwe vya wahalifu ambapo itatusaidia kuyaepuka maeneo hayo vilevile kuvisaidia vyombo vya dola kufuatilia na kuwakamata wahalifu.

Pia tusishau kujuzana mitaa salama ambapo muda wowote hasa nyakati za usiku ni ngumu kukumbwa na tatizo la uhalifu.

Ni vyema ukataja mkoa, wilaya ama kijiji husika.

Karibuni...
 
Back
Top Bottom