Tujuzane: Mfahamu Eli Cohen jasusi hodari wa Israeli nchini Syria

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
7,905
13,348
TUJUZANE: MFAHAMU Eli Cohen JASUSI HODARI WA ISRAELI NCHINI SYRIA

Na Mgeni wa Jiji

Eli Cohen ni jina lenye heshima ndani ya shirika la kijasusi Israel 'MOSSAD'. Uzalendo, kipaji na uwezo mkubwa wa kujifunza na kukumbuka mambo ni vitu vinavyoaminika kuwa silaha kuu ya jasusi huyu. Eli Cohen ni nani?, kwanini anakumbukwa nchini Israeli?, ni zipi kazi alizowahi kufanya?, Je sasa yupo wapi?.

Haya ni baadhi ya maswali nitakayoyajibu ndani ya makala hii yenye lengo moja kuu kuelimishana historia ya dunia.

Baada ya Israeli kuanza kujitafutia utawala wake binafsi mataifa mengi kama si yote ya kiarabu yalitangaza uadui na Israeli. Ni kuanzia hapo Israeli ilipoona umuhimu wa kupandikiza kizazi kipya cha majasusi wa taifa hilo dogo lililozungukwa na maadui. Kutokana na udogo wake kijiografia na wingi wa maadui Israeli iliamini kuwa taarifa ni silaha.

Katika kipindi hicho ndipo kijana wa kiyahudi aliyeishi huko Misri na familia yake iliyohama kutoka Syria Eli Cohen alichipukia kama jasusi wa Israeli ndani ya mataifa ya kaskazini mwa Afrika hususa Misri na Syria. Akiwa mahiri katika upigaji picha, kumbukumbu ya mambo, sayansi ya silaha na mahiri wa lugha. Moja ya kazi za mwanzo za Eli Cohen ilikuwa ni kuwatoroshea Israeli wayahudi walioishi Misri kazi aliyoifanya kwa mafanikio makubwa yaliyolipelekea shirika la ujasusi wa kijeshi Israeli kumuangalia kwa ukaribu mkubwa jasusi huyu kijana.

Eli Cohen alipewa mafunzo mengi zaidi ya kijasusi ikiwa ni kumuandaa kwa ajili ya kazi hatari nchini Syria. Alijifunza aya zote muhimu za kitabu tukufu cha Quran, sala muhimu kwa kila muislamu, tamaduni za jamii ya Syria pamoja na siasa ya taifa hilo. Miaka ya 1960s tayari Eli Cohen alikuwa miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa kisyria walioaminiwa na viongozi wa kisiasa na kijeshi hadi kufikia hatua ya kuchangia mawazo katika mikakati ya kisiasa na kijeshi hususa ile ya kuliteketeza taifa adui wa nchi za uarabi, Israeli.

Akiwa Syria Eli Cohen alijulikana kama Kamel Amin Sabet, msyria aliyekulia nchini Argentina. Ikumbukwe kuwa kipindi hicho 1960s Argentina ilikuwa ndio kimbilio la raia wengi wa Syria na ndipo walipokutana wasyria wakajadili hali ya taifa lao nyumbani.

La Casa Arabe ni sehemu iliyomjengea ukaribu mkubwa na watu maarufu wa Syria, akijinasibu kama mfanyabiashara, miongoni mwa watu hao ni aliyekuja kuwa kiongozi wa chama cha BAF aliyemtambulisha Cohen kwenye jamii ya watu maarufu wa Syria.

Akiwa mjini Damascas Cohen alifanikiwa kujenga urafiki na maofisa wa jeshi la Syria waliomuamini hadi kufikia hatua ya kumuonesha makombora ya taifa hilo. 1963 rafiki mkubwa wa Cohen, General Amin El hatha alifanikiwa kuwa raisi wa Syria. Cohen alizidi kuwa na nguvu nchini Syria hadi kufikia hatua ya kupendekezwa kuwa waziri wa ulinzi wa taifa ilo.

Ni kutokana na ukaribu wake na viongozi wa kisiasa na kijeshi wa Syria Cohen alifanikiwa kuujua mpango wa Syria kuzuia maji ya mto Jordan yasifike Israeli kwa kujenga mabwawa makubwa. Coheni alilitaarifu taifa lake Israeli na bila kuchelewa Israeli ililipua maeneo ya Syria yaliyotengwa kwa ajili ya mabwawa hayo.

Eli Cohen aliweza kupeleka taarifa nyingi za kijeshi za Syria kwa Israeli

1965 jasusi Eli Cohen aliingia matatani, ikiwa ni muda mchache baada ya kutokea Israeli, Cohen akiwa katika majukumu yake ya kijasusi, akituma ujumbe wa siri Israeli kwa njia ya radio, kikosi cha Kupambana na ujasusi Syria kikitumia vifaa vya kunasa mawasiliano kutoka Urusi walifanikiwa kumnasa Cohen akiwa ndani ya nyumba yake iliyokuwa jirani kabisa na kambi kubwa ya jeshi akituma mawasiliano. Cohen alikamatwa na kufanyiwa upekuzi ndipo hapo Eli Cohen alipogundulika kama jasusi wa Israeli, Cohen alishitakiwa na kuhukumiwa kifo kwa kunyongwa hadharani mwezi wa 5 wa mwaka 1965.

Taarifa za mwisho alizotuma nyumbani Israeli ndizo zilizofanikisha Israeli kuudhibiti upande wa Gullan upande hatari zaidi kwa ulinzi na usalama wa taifa hilo dogo lililozingirwa na maadui, hadi sasa watalii wanaotembelea Gullan hupewa historia ya jasusi huyu na mchango wake kwa Israeli.

Yapo mengi yaliyofanywa na jasusi huyu kwa taifa lake la Israeli aliyeishi na maadui wa taifa lake kama miongoni mwao kushiriki mikakati mbali mbali dhidi ya taifa lake na kisha kuidhibiti mikakati hiyo kwa kutumia mawasiliano ya radio.
186B6123-672F-4460-B543-F4DD6A7AB40B-3575-000003B170B18AD3.jpg
 
Yeah in an intelligent world he deserves to receive such a honor. Many of us don't real understand what it takes to be a patriotic to our country.. Will come back soon with more elaborations on the matter
 
TUJUZANE: MFAHAMU Eli Cohen JASUSI HODARI WA ISRAELI NCHINI SYRIA

Na Mgeni wa Jiji

Eli Cohen ni jina lenye heshima ndani ya shirika la kijasusi Israel 'MOSSAD'. Uzalendo, kipaji na uwezo mkubwa wa kujifunza na kukumbuka mambo ni vitu vinavyoaminika kuwa silaha kuu ya jasusi huyu. Eli Cohen ni nani?, kwanini anakumbukwa nchini Israeli?, ni zipi kazi alizowahi kufanya?, Je sasa yupo wapi?.

Haya ni baadhi ya maswali nitakayoyajibu ndani ya makala hii yenye lengo moja kuu kuelimishana historia ya dunia.

Baada ya Israeli kuanza kujitafutia utawala wake binafsi mataifa mengi kama si yote ya kiarabu yalitangaza uadui na Israeli. Ni kuanzia hapo Israeli ilipoona umuhimu wa kupandikiza kizazi kipya cha majasusi wa taifa hilo dogo lililozungukwa na maadui. Kutokana na udogo wake kijiografia na wingi wa maadui Israeli iliamini kuwa taarifa ni silaha.

Katika kipindi hicho ndipo kijana wa kiyahudi aliyeishi huko Misri na familia yake iliyohama kutoka Syria Eli Cohen alichipukia kama jasusi wa Israeli ndani ya mataifa ya kaskazini mwa Afrika hususa Misri na Syria. Akiwa mahiri katika upigaji picha, kumbukumbu ya mambo, sayansi ya silaha na mahiri wa lugha. Moja ya kazi za mwanzo za Eli Cohen ilikuwa ni kuwatoroshea Israeli wayahudi walioishi Misri kazi aliyoifanya kwa mafanikio makubwa yaliyolipelekea shirika la ujasusi wa kijeshi Israeli kumuangalia kwa ukaribu mkubwa jasusi huyu kijana.

Eli Cohen alipewa mafunzo mengi zaidi ya kijasusi ikiwa ni kumuandaa kwa ajili ya kazi hatari nchini Syria. Alijifunza aya zote muhimu za kitabu tukufu cha Quran, sala muhimu kwa kila muislamu, tamaduni za jamii ya Syria pamoja na siasa ya taifa hilo. Miaka ya 1960s tayari Eli Cohen alikuwa miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa kisyria walioaminiwa na viongozi wa kisiasa na kijeshi hadi kufikia hatua ya kuchangia mawazo katika mikakati ya kisiasa na kijeshi hususa ile ya kuliteketeza taifa adui wa nchi za uarabi, Israeli.

Akiwa Syria Eli Cohen alijulikana kama Kamel Amin Sabet, msyria aliyekulia nchini Argentina. Ikumbukwe kuwa kipindi hicho 1960s Argentina ilikuwa ndio kimbilio la raia wengi wa Syria na ndipo walipokutana wasyria wakajadili hali ya taifa lao nyumbani.

La Casa Arabe ni sehemu iliyomjengea ukaribu mkubwa na watu maarufu wa Syria, akijinasibu kama mfanyabiashara, miongoni mwa watu hao ni aliyekuja kuwa kiongozi wa chama cha BAF aliyemtambulisha Cohen kwenye jamii ya watu maarufu wa Syria.

Akiwa mjini Damascas Cohen alifanikiwa kujenga urafiki na maofisa wa jeshi la Syria waliomuamini hadi kufikia hatua ya kumuonesha makombora ya taifa hilo. 1963 rafiki mkubwa wa Cohen, General Amin El hatha alifanikiwa kuwa raisi wa Syria. Cohen alizidi kuwa na nguvu nchini Syria hadi kufikia hatua ya kupendekezwa kuwa waziri wa ulinzi wa taifa ilo.

Ni kutokana na ukaribu wake na viongozi wa kisiasa na kijeshi wa Syria Cohen alifanikiwa kuujua mpango wa Syria kuzuia maji ya mto Jordan yasifike Israeli kwa kujenga mabwawa makubwa. Coheni alilitaarifu taifa lake Israeli na bila kuchelewa Israeli ililipua maeneo ya Syria yaliyotengwa kwa ajili ya mabwawa hayo.

Eli Cohen aliweza kupeleka taarifa nyingi za kijeshi za Syria kwa Israeli

1965 jasusi Eli Cohen aliingia matatani, ikiwa ni muda mchache baada ya kutokea Israeli, Cohen akiwa katika majukumu yake ya kijasusi, akituma ujumbe wa siri Israeli kwa njia ya radio, kikosi cha Kupambana na ujasusi Syria kikitumia vifaa vya kunasa mawasiliano kutoka Urusi walifanikiwa kumnasa Cohen akiwa ndani ya nyumba yake iliyokuwa jirani kabisa na kambi kubwa ya jeshi akituma mawasiliano. Cohen alikamatwa na kufanyiwa upekuzi ndipo hapo Eli Cohen alipogundulika kama jasusi wa Israeli, Cohen alishitakiwa na kuhukumiwa kifo kwa kunyongwa hadharani mwezi wa 5 wa mwaka 1965.

Taarifa za mwisho alizotuma nyumbani Israeli ndizo zilizofanikisha Israeli kuudhibiti upande wa Gullan upande hatari zaidi kwa ulinzi na usalama wa taifa hilo dogo lililozingirwa na maadui, hadi sasa watalii wanaotembelea Gullan hupewa historia ya jasusi huyu na mchango wake kwa Israeli.

Yapo mengi yaliyofanywa na jasusi huyu kwa taifa lake la Israeli aliyeishi na maadui wa taifa lake kama miongoni mwao kushiriki mikakati mbali mbali dhidi ya taifa lake na kisha kuidhibiti mikakati hiyo kwa kutumia mawasiliano ya radio.View attachment 580111
Nataka kujua hawa majasusi wanapeleka vp taarifa kwa mataifa yao mpaka inakuwa siri waliomzunguka inakuwa ngumu kuwajua?? Na hata kama wakijua tayar wanakua wmechelewa kama walivyo chelewa kwa huyo jasus

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walikuwa wanatumia radio wengi wao, ila taarifa zilienda kwa mfumo wa code. Ila kuna baadhi walitumia njia ya kusafirisha nyaraka kawaida kama vifurushi. Mf. John Walker
 
Hivi yossi Cohen dir wa mossad anamahusiano yoyote na elli Cohen!

Ova
 
TUJUZANE: MFAHAMU Eli Cohen JASUSI HODARI WA ISRAELI NCHINI SYRIA

Na Mgeni wa Jiji

Eli Cohen ni jina lenye heshima ndani ya shirika la kijasusi Israel 'MOSSAD'. Uzalendo, kipaji na uwezo mkubwa wa kujifunza na kukumbuka mambo ni vitu vinavyoaminika kuwa silaha kuu ya jasusi huyu. Eli Cohen ni nani?, kwanini anakumbukwa nchini Israeli?, ni zipi kazi alizowahi kufanya?, Je sasa yupo wapi?.

Haya ni baadhi ya maswali nitakayoyajibu ndani ya makala hii yenye lengo moja kuu kuelimishana historia ya dunia.

Baada ya Israeli kuanza kujitafutia utawala wake binafsi mataifa mengi kama si yote ya kiarabu yalitangaza uadui na Israeli. Ni kuanzia hapo Israeli ilipoona umuhimu wa kupandikiza kizazi kipya cha majasusi wa taifa hilo dogo lililozungukwa na maadui. Kutokana na udogo wake kijiografia na wingi wa maadui Israeli iliamini kuwa taarifa ni silaha.

Katika kipindi hicho ndipo kijana wa kiyahudi aliyeishi huko Misri na familia yake iliyohama kutoka Syria Eli Cohen alichipukia kama jasusi wa Israeli ndani ya mataifa ya kaskazini mwa Afrika hususa Misri na Syria. Akiwa mahiri katika upigaji picha, kumbukumbu ya mambo, sayansi ya silaha na mahiri wa lugha. Moja ya kazi za mwanzo za Eli Cohen ilikuwa ni kuwatoroshea Israeli wayahudi walioishi Misri kazi aliyoifanya kwa mafanikio makubwa yaliyolipelekea shirika la ujasusi wa kijeshi Israeli kumuangalia kwa ukaribu mkubwa jasusi huyu kijana.

Eli Cohen alipewa mafunzo mengi zaidi ya kijasusi ikiwa ni kumuandaa kwa ajili ya kazi hatari nchini Syria. Alijifunza aya zote muhimu za kitabu tukufu cha Quran, sala muhimu kwa kila muislamu, tamaduni za jamii ya Syria pamoja na siasa ya taifa hilo. Miaka ya 1960s tayari Eli Cohen alikuwa miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa kisyria walioaminiwa na viongozi wa kisiasa na kijeshi hadi kufikia hatua ya kuchangia mawazo katika mikakati ya kisiasa na kijeshi hususa ile ya kuliteketeza taifa adui wa nchi za uarabi, Israeli.

Akiwa Syria Eli Cohen alijulikana kama Kamel Amin Sabet, msyria aliyekulia nchini Argentina. Ikumbukwe kuwa kipindi hicho 1960s Argentina ilikuwa ndio kimbilio la raia wengi wa Syria na ndipo walipokutana wasyria wakajadili hali ya taifa lao nyumbani.

La Casa Arabe ni sehemu iliyomjengea ukaribu mkubwa na watu maarufu wa Syria, akijinasibu kama mfanyabiashara, miongoni mwa watu hao ni aliyekuja kuwa kiongozi wa chama cha BAF aliyemtambulisha Cohen kwenye jamii ya watu maarufu wa Syria.

Akiwa mjini Damascas Cohen alifanikiwa kujenga urafiki na maofisa wa jeshi la Syria waliomuamini hadi kufikia hatua ya kumuonesha makombora ya taifa hilo. 1963 rafiki mkubwa wa Cohen, General Amin El hatha alifanikiwa kuwa raisi wa Syria. Cohen alizidi kuwa na nguvu nchini Syria hadi kufikia hatua ya kupendekezwa kuwa waziri wa ulinzi wa taifa ilo.

Ni kutokana na ukaribu wake na viongozi wa kisiasa na kijeshi wa Syria Cohen alifanikiwa kuujua mpango wa Syria kuzuia maji ya mto Jordan yasifike Israeli kwa kujenga mabwawa makubwa. Coheni alilitaarifu taifa lake Israeli na bila kuchelewa Israeli ililipua maeneo ya Syria yaliyotengwa kwa ajili ya mabwawa hayo.

Eli Cohen aliweza kupeleka taarifa nyingi za kijeshi za Syria kwa Israeli

1965 jasusi Eli Cohen aliingia matatani, ikiwa ni muda mchache baada ya kutokea Israeli, Cohen akiwa katika majukumu yake ya kijasusi, akituma ujumbe wa siri Israeli kwa njia ya radio, kikosi cha Kupambana na ujasusi Syria kikitumia vifaa vya kunasa mawasiliano kutoka Urusi walifanikiwa kumnasa Cohen akiwa ndani ya nyumba yake iliyokuwa jirani kabisa na kambi kubwa ya jeshi akituma mawasiliano. Cohen alikamatwa na kufanyiwa upekuzi ndipo hapo Eli Cohen alipogundulika kama jasusi wa Israeli, Cohen alishitakiwa na kuhukumiwa kifo kwa kunyongwa hadharani mwezi wa 5 wa mwaka 1965.

Taarifa za mwisho alizotuma nyumbani Israeli ndizo zilizofanikisha Israeli kuudhibiti upande wa Gullan upande hatari zaidi kwa ulinzi na usalama wa taifa hilo dogo lililozingirwa na maadui, hadi sasa watalii wanaotembelea Gullan hupewa historia ya jasusi huyu na mchango wake kwa Israeli.

Yapo mengi yaliyofanywa na jasusi huyu kwa taifa lake la Israeli aliyeishi na maadui wa taifa lake kama miongoni mwao kushiriki mikakati mbali mbali dhidi ya taifa lake na kisha kuidhibiti mikakati hiyo kwa kutumia mawasiliano ya radio.View attachment 580111
Alitengenezewa movie iliitwa "the impossible Spy"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom