Tujuzane mbinu chafu zinazotumiwa na baadhi ya wafanyabiashara

namvumi king

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
734
1,000
1. Kuna baadhi ya wauza mikate wanatabia ya kupunguza zile slesi katika mkate..

Alafu wanazikusanya kupata mkate Mwingine, ngumu sana kulingudua ilo maana watu hawana muda wa kuhesabu slesi za mkate

2. Jamaa zetu wauza viberit nao wanafanya mchezo kama wauza mikate

Wanapunguza zile njiti alafu wanapata kiberiti kipya, yaani apo anapata Faida ya ziada

3. Kwenye mafuta ya kupikia, wanaifungua galoni wanapunguza mafuta kisha wanaibonyeza pembeni nafasi ya mafuta waliyoyatoa hewa inakaaa...galoni inasoma lita 5 kumbe ni lita 4 na ukiicheki chupa ya galoni ina dimpoz...watu ni wahuni sanaaa....hahahahhaaaa

4. Kuna mbinu moja matata sana katika mzani yaan unakuta mzani unawekwa upande wa fen ule ambao umewekwa unga au chochote kinachopimwa ile fen unakuta inazunguka kwa kasi sana unazani kakuzidishia bizaa kumbe upepo wa fen tuwe makini hapo

5. K/koo wanatabia ya kuipaka nyanya mafuta ikipigwa na taa ile ya jion inang'aa hatari ukichunguza vzr utakuta mbovu

6. Ukinunua sosej, ndizi au nyama choma ukaletewa imekatwakatwa tyr, jua kuna vipande vishaibiwa. Ni rahisi kujua ktk sosej na ndizi maana zile ncha mbili za sosej au ndizi huenda usione moja wapo ktk vile vipande. Nyama choma huwezi jua ila mishkaki omba uletewe na vijiti vyake.

7. Michele wa quality moja ambao unaoaswa kuuzwa Tsh 1,900 kwa kilo unagawanyishwa magunia mawili tofauti .gunia moja unaambiwa kg 1 ni 1900 na jingine kg 1 ni 2200.... Wengi wetu tunakimbilia wa 2,200 kwa kuamini ndio Bora.. unapigwa ukicheka hapo

8. Huku kwetu sabuni za kupima wanachanganya na unga kidogo,unanunua kilo ya sabuni haina povu halafu unaweza shangaa nusu nzima umeimaliza kwa nguo tano tu.
 
reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,740
2,000
Kuna vitu vingine wanajitia tuu nuksi kuiba, sasa unaiba slesi moja moja ya mkate au njiti ya hicho kibiriti , mpaka unaze kibiriti kingine ni lini? hio sh hamsini itakupeleka wapi...?
Khaa Huo mda si bora ungeutumia kuombea taifa..

Mi nahisi hata dhambi kuna za jumla na rejareja, haiwezekani Mwenzako Aibe kodi za watanzania wote na Mil 50 za kila kijiji, wewe uibe njiti ya kiberiti halafu muwekewe kwenye pipa moja...

Aaaaah hata huyo shetani Hio roho hana, na ukizingatia alianza kua Malaika kabla ya kuasi....
Ukiona hivyo wewe sio mtenda dhambi, ni uroho tuu, kuna mijitu ina dhambi zao banaa.
 
Msonjo Khan

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
558
1,000
Maghamashi kwenye biashara ni mengi mno, na hii inatokana na baadhi ya wafanya biashara wenye tamaa.

Hii ya mwisho ya kutia unga kwenye sabuni imenishangaza, sasa hiyo sabuni si itakuwa inachafua nguo au? maana unga hauyayuki kama sabuni.
 
jacana

JF-Expert Member
May 24, 2020
448
500
10/ wafanyabiasha waotumia mizan hasa hii ya mawe na sahani

sasa ujanja upo hivi mazani huwekewa jiwe la 100g ili kubalace na sahani sasa muuzaji huondoa 100g, hapo akishaondoa uzito wote hubaki kwa mteja.mfano labda unanunua Michele 1000g yeye atakupimia 800g
 
Christine1

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
14,280
2,000
Maghamashi kwenye biashara ni mengi mno, na hii inatokana na baadhi ya wafanya biashara wenye tamaa.

Hii ya mwisho ya kutia unga kwenye sabuni imenishangaza, sasa hiyo sabuni si itakuwa inachafua nguo au? maana unga hauyayuki kama sabuni.
Inawezekana,ndo maana sijawahi zielewa sabuni za kupima za unga! Km chokaa hivi,sabuni nyingi haina povu!

Bora foma,omo,Aerial,toss....za zamani
 
Madame B

Verified Member
Apr 9, 2012
28,815
2,000
1. Kuna baadhi ya wauza mikate wanatabia ya kupunguza zile slesi katika mkate..

Alafu wanazikusanya kupata mkate Mwingine, ngumu sana kulingudua ilo maana watu hawana muda wa kuhesabu slesi za mkate

2. Jamaa zetu wauva viberit nao wanafanya mchezo kama wauza mikate

Wanapunguza zile njiti alafu wanapata kiberiti kipya, yan apo anapata Faida ya ziada

3. Kwenye mafuta ya kupikia, wanaifungua galoni wanapunguza mafuta kisha wanaibonyeza pembeni nafasi ya mafuta waliyoyatoa hewa inakaaa...galoni inasoma lita 5 kumbe ni lita 4 na ukiicheki chupa ya galoni ina dimpoz...watu ni wahuni sanaaa....hahahahhaaaa

4. Kuna mbinu moja matata sana katika mzani yaan unakuta mzani unawekwa upande wa fen ule ambao umewekwa unga au chochote kinachopimwa ile fen unakuta inazunguka kwa kasi sana unazani kakuzidishia bizaa kumbe upepo wa fen tuwe makini hapo

5. K/koo wanatabia ya kuipaka nyanya mafuta ikipigwa na taa ile ya jion inang'aa hatari ukichunguza vzr utakuta mbovu

6. Ukinunua sosej, ndizi au nyama choma ukaletewa imekatwakatwa tyr, jua kuna vipande vishaibiwa. Ni rahisi kujua ktk sosej na ndizi maana zile ncha mbili za sosej au ndizi huenda usione moja wapo ktk vile vipande. Nyama choma huwezi jua ila mishkaki omba uletewe na vijiti vyake.

7. Michele wa quality moja ambao unaoaswa kuuzwa Tsh 1,900 kwa kilo unagawanyishwa magunia mawili tofauti .gunia moja unaambiwa kg 1 ni 1900 na jingine kg 1 ni 2200.... Wengi wetu tunakimbilia wa 2,200 kwa kuamini ndio Bora.. unapigwa ukicheka hapo

8. Huku kwetu sabuni za kupima wanachanganya na unga kidogo,unanunua kilo ya sabuni haina povu halafu unaweza shangaa nusu nzima umeimaliza kwa nguo tano tu.
Namba 8 ni kweli kabisa
Kuna sabuni (sitaitaja jina) ukinunua, ukiiweka kwenye maji unaona kabisa ungaunga juu, sabuni ya 500 ila ukiiyeyusha unafua mfuo mmoja tu!!
Hii ni kwa sisi wa uswazi, nyie wa kishua hamtaelewa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom