Habari za muda huu wachakalikaji?
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza hapo juu, sisi kama watafutaji na wafanyabiashara wa mafuta ya kupima na kuwauzia wakaanga mihogo, samaki, chipsi na wengine wanaoyatumia kwa sana tunafeli kutokana na bei za mafuta kuwa juu sana na kupelekea kuwapandishia hao akina baba na mama zetu wanaoyahitaji sana kitu kinachopelekea kutopata faida au kula hasara moja kwa moja.
Huku kwetu Kimara dumu moja la lita 20 sasa hivi ni 60,000 Mpaka 57,000. Madukani reja reja kwa lita ni 3,500. Bei hii ni kubwa sana kwa muuza mihogo na chipsi.
Karibuni tujuzane bei za huko kwenu bei za mafuta kwa jumla na rejareja.
Karibuni ndugu zangu.