Tujuzane kuhusu AC je ni kweli zinanyonya umeme hadi unit 35 kwa siku?

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,626
Leo tupeane ujuzi kuhusu AC aka viyoyozi je ni kweli huwa zinatumia unit hadi 35 hadi 40 kwa zikiwasha masaa 24?

Wenye AC mje mtupe ushuhuda huwa mnatumia vipi na huwa inatumia units ngapi kwa siku maana maneno ni mengi sana.

Najua wapo wengi tu wanatamani kuwa na AC ndani lakini tatizo ndo hilo kwamba wanaogopa gharama au hawajapata kufaham vizuri kuhusu AC.

Naombeni tujuzane.

AC yako unawasha kwa muda gani na huwa inakula units ngapi kila siku.

Gharama zake, ubora, nk.

Karibuni sana.
 
AC sema zipo za ukubwa na aina mbalimbali. Kuna izi "power efficiency" inaweza kula units kidogo. Sasa itategemeana na vingi:

(1) umewasha masaa mangapi?
(2) joto unalotaka ishushe na hali ya hewa ya nje maana AC zikifika muda flan uwa zinajizima. Sasa kama nje joto 35 degrees wewe umeweka ifikishe 17 hapo kuzima sahau.
(3) size ya room
(4) aina, hali ya uchakavu, .. ya AC



Mi iyo takataka sinunui kamwe labda nidake Air cooler. Ila kwa Dar aircooler sio effective coz Humidity ni kubwa inafaa sana Dodoma uko na miko ilio mbali na Dar.

Yote 9 kumi aisee maisha magumu wazee, jumlisha na hii corona na siasa hizi dah hafu unakuta mtu haunywi pombe. Unapataje usingizi?
 
Braza units 30 per day!? Kwa AC moja? Acha masikhara hayo. Unajua hivi vifaa vya umeme huwa vinapimwa utumizi wake wa umeme kwa Watts. Ac inategemea na ukubwa wake wa watts

Nb Unit 1 ni sawa na Watts 1000.
Ukiwa na vitu vyenye watts 1000 ukaviwasha kwa muda wa saa moja utakuwa umetumia units ngapi?
 
Leo tupeane ujuzi kuhusu AC aka viyoyozi jee ni kweli huwa zinatumia unit hadi 35 hadi 40 kwa zikiwasha masaa 24?

Wenye AC mje mtupe ushuhuda huwa mnatumia vipi na huwa inatumia units ngapi kwa siku maana maneno ni mengi sana

Najua wapo wengi tu wanatamani kuwa na AC ndani lakini tatizo ndo hilo kwamba wanaogopa gharama au hawajapata kufaham vizuri kuhusu AC

Naombeni tujuzane

AC yako unawasha kwa muda gani na huwa inakula units ngapi kila siku

Gharama zake, ubora, nk

Karibuni sana
Unit 35 - 40 inawezekana sana ila sasa matumizi haya sio kwa AC 1 ni kama kwenye hotels ambako kuna rooms nyingi ndio matumizi hayo yanawezekana ila kwa matumizi ya nyumbani hasa kama ac ni moja basi unaweza kutumia unit 3 tu mpaka 4 inategemea na AC yako
 
AC inayokula Units 35-40 kwa siku haipo dunia hii, hata zikiwa 3 units 40 hazigongi, unless iwe ni very old, yaani units 1200 kwa Mwezi????

Huyo aliekuambia kakutisha tuu ili mtaani aonekane kafunga yeye tuu.
Labda kama anafanya na recycling ya vyuma
 
Back
Top Bottom