Tujuzane kidogo, Uchawi una nafasi gani katika biashara

Job Richard

JF-Expert Member
Feb 8, 2013
3,865
2,176
Biashara nyingi uchawi unahusika kwa namna moja au nyingine majuzi katika tafuta yangu ujuzi ili nizame kwenye kisima hiki cha biashara nikaishiwa nguvu kitendo cha kuambiwa ni lazima uende kidogo kwa babu avute wateja hizi imani zipoje

Makazini uchawi, Biashara uchawi ina maana kazi na biashara haiendi bila uchawi ndugu yangu work mate kafungua bucha fasta kwa mganga eti zindiko na kukwepa chuma ulete why Tanzania au hata Bakhressa pale alipofika ametumia hizi nguvu za kichawi tujuzane najua mpo kama huyu jamaangu

Labda nipo usingizini acha niendelee kulala
 
Km unataka kufungua biashara Tandale kwa tumbo na uswahil haswa ww fungua tu hiyo biashara alafu jion piga mahesabu uone km yatakuja sawa ndo utajua inanafasi gani uchawi

Mkuu kila mmoja na njia zake za kufikia mafanikio km vp ikiwa muislam
Mwite sheikh apige kisomo anza biashara km mkristo piga dua anza kazi km uko uswahilini usijiangaishe mtafute kalumanzila aeke mambo sawa
 
Sirdirashy,

duuuuh sasa mimi sehemu yangu ya biashara ninapotaka kufungua eneo la msikiti nami mkiristo NILIKUWA NJE NA HII IMANI NGOJA NIKALIOMBEE maana hizi imani zetu sasa
kwani huyo chuma ulete anakuibiaje akati hesabu zako unaijua umepata shilingi ngapi NAKUMBUKA MWAKA JUZI JAMAA ALIKIMBIA GENGE LAKE AKIDAI ANAIBIWA NA CHUMA ULETE MIMI NILIMWAMBIA tatizo lipo kwake kwenye matumizi huenda anatumia sana pesa ya biashara katika matumiz binafsi lakini sio uswazi kule
 
Km unataka kufungua biashara Tandale kwa tumbo na uswahil haswa ww fungua tu hiyo biashara alafu jion piga mahesabu uone km yatakuja sawa ndo utajua inanafasi gani uchawi

Mkuu kila mmoja na njia zake za kufikia mafanikio km vp ikiwa muislam
Mwite sheikh apige kisomo anza biashara km mkristo piga dua anza kazi km uko uswahilini usijiangaishe mtafute kalumanzila aeke mambo sawa

Biashara nyingi uchawi unahusika kwa namna moja au nyingine MAJUZI KATIKA TAFUTA YANGU UJUZI ILI NIZAME KWENYE KISIMA HIKI CHA BIASHARA nikaishiwa nguvu kitendo cha kuambiwa ni lazima uende kidogo kwa babu avute wateja HIZI IMANI ZIPOJE

MAKAZINI UCHAWI
BIASHARA UCHAWI ina maana kazi na biashara haiendi bila uchawi NDUGU YANGU WORK MATE KAFUNGUA BUCHA fasta kwa mganga eti zindiko na kukwepa chuma ulete why TZ au hata Bakhressa pale alipofika ametumia hizi nguvu za kichawi TUJUZANE NAJUA MPO kama huyu jamaangu

LABDA NIPO USINGIZINI ACHA NIENDELEE KULALA

Mkuu biashara na uchawi ni vitu viwili visivyohusiana kabisa kwa 100%. Biashara ni bidii yako na commitment yako. uchawi hausaidii biashara ikuwe au kuongeza mauzo. Maombi yako na imani yako katika biashara yako ndio siri ya mafaniakio yako. Sio uchawi. Mchawi na yeye anafanya biashara tu anataka uende kwake na yeye apate hela. Kabla hujaenda kwa mchawi jiulize kwa nini mchawi anaishi maisha ya kifukara na anakwambie wewe utakiwa tajili, kwani yeye hataji kuwa tajili?.......
Ushauri- Fanya biashara yako kwa bidii zote na muombe Mungu utafanikiwa tu, achana na imani hizo potofu.
 
Kaka,

1. Mtegemee Mwenyezi Mungu. Yeye ndio amekuumba wewe na ndio pekee wa kukuongoza kwenye mafanikio.
2. Hangaika. Waarabu wana msemo wao, "Manijtahada, Wajada" yaani mwenye kujitahidi hufanikiwa. Kama unaona hupati mafanikio ongeza jitihada na tafuta marafiki waliofanikiwa wakusaidie kimawazo.
3. 10X biashara yako. Kama unafanya biashara ambayo watu wengine wanafanya. Jiulize swali lifuatayo, "Nifanye kitu gani niwe bora Mara 10 kuliko washindani wangu?". Ukishapata jibu fanya hivyo.

Uchawi upo lakini haina nguvu kama unavyofikiria. Ingekuwa inayo basi kwa uchawi wetu wakiTanzania tungekuwa tushashinda Africa Cup. Ajabu nikuwa hata kuingia hatuingia.

Focus kwenye kuchapa kazi na achana na mambo haya. Yatakuumiza kichwa na kuuwa malengo yako.

Good Luck!
 
kama uchawi ungekuwa unalipa tungekuwa nchi amabyo ingeongoza kwa uchumi nadhani ni Nigeria kwa dunia nzima muhimu ni juhudi na maarifa usiamke baada ya wateja kuamka amka kabla ya wateja kuamka , chunga kauri za kufunga biashara yako mfano "mteja anauliza una sabuni ya Ayu ? wewe unamjibu mbona zimeacha kutumika miaka mingi sasa hapo unaua biashara yako.
 
Jajojo,

asante mkuu wewe naona upo upande wangu nami siviamini hivi vitu lakini cha kushangaza nimeshuhudia na kusimuliwa biashara nyingi zinaendeshwa kwa ushirikina na mwanzoni nikajua labda hawa wasiosoma ndo wanaongoza enzi za utoto maana nakumbuka kuna jamaa mbeya home alikuwa na mashine ikasadikiwa kamuua mtu ili amzindike KO NIMEKUWA NIKIJIULIZA KUNA UHUSIANO GANI WA BIASHARA NA UCHAWI kama haitoshi kuna eneo iringa makambako nikaambiwa pale wote wamezindika maduka yao bila kufanya hivo hupati mteja kariakoo ivo ivo utaona mwenzio anauza wote bidhaa sawa watu wote wanakimbilia kwake eti anaweka dawa ya kuvuta wateja JE UMEWAHI SIKIA HAYA AU JAPO KUWAHOJI WAFANYABIASHARA WACHACHE
 
kama uchawi ungekuwa unalipa tungekuwa nchi amabyo ingeongoza kwa uchumi nadhani ni Nigeria kwa dunia nzima muhimu ni juhudi na maarifa usiamke baada ya wateja kuamka amka kabla ya wateja kuamka , chunga kauri za kufunga biashara yako mfano "mteja anauliza una sabuni ya Ayu ? wewe unamjibu mbona zimeacha kutumika miaka mingi sasa hapo unaua biashara yako.

KABISA mkuu lakini wapo wenzetu hapa bongo wanaamini hayo no biashara bila mganga kuhusika
 
Dr. Said,


asante mkuu upo sawa ingawa hii imani imeua sana utendaji wetu maana wengi wameegemea huko badala ya kuwaza kusonga mbele kibiashara hapo bold NDIPO TATIZO LILIPO USINGEKUWA NA NGUVU WASINGEKUWA WANAENDA KUUTAFUTA
 
Wengi wanadai kuwa waganga wanaweza kutambika sehemu ya biashara yako na kuifanya upate wateja mimi siko simo huko......nakuja kwa upande wako je hiyo sehemu unayotaka kuzama kibiashara umeshajiuliza ni wachawi wangapi wametoka hapo?hapa namaanisha wafanyabiashara waliowahi kuleta waganga kuwatambikia?unafikiri hiyo sehemu(ardhi)imetamkiwa vitu vingapi ambavyo vilizoea kuabudiwa?..ushauri wangu kabla hata hujaingiza mzigo sehemu husika mtangulize kiongozi wako wa kiroho unayemuamini au kama wewe ni muumini mzuri ambaye umesimama tambika kwa DAMU YA YESU hakuna mchawi wala shetani atakayeisogelea biashara yako,otherwise utaishia kugombana na wafanyakazi wako na hutopata muafaka.
Nawasilisha
 
asante mkuu upo sawa ingawa hii imani imeua sana utendaji wetu maana wengi wameegemea huko badala ya kuwaza kusonga mbele kibiashara hapo bold NDIPO TATIZO LILIPO USINGEKUWA NA NGUVU WASINGEKUWA WANAENDA KUUTAFUTA
Na ndio maana nikasema ingekuwa na nguvu tungekuwa tunafanikiwa. Timu zetu za mpira zinasifika kwa ushirikina lakini wanafika wapi?

Hakuna utafiti wenye kuonyesha direct correlation ya uchawi na mafanikio. Na hakuna utafiti wenye kuonyesha kuwa bila uchawi hutofanikiwa.

Na tunawaona wengi wanafanya ushirikina lakini hawafanikiwi.

CONCLUSION: Ni upotezaji muda ku spent time na energy yako katika mambo haya wakati unaweza kutumia muda wako katika kujifunza jinsi gani ya kutatua changamoto unazokumbana nazo.
 
matron,

Asante nami siuamini kabisa uchawi kilichonifanya nijiulize sana ni baada ya kwenda sehemu yangu kuna jamaa yeye hana biashara hii ninayotaka kuingia ila kuna jirani yangu ana biashara hiyo sasa inaonyesha eti ni mwingi wa waganga NAONGEA NAE VIZURI NA ANA MOYO MZURI KWA MACHO LABDA KAMA ANATUNZA CHUKI lakini wapembeni ndo wanamsema ivo
na ukiangalia hili jambo limeshamiri sana BIASHARA NYINGI ZINA UCHAWI NDANI YAKE but nafarijika wengi hamuyaamini haya TUSONGE KUIKUZA NCHI YETU THANKS
 
the RICHARDS,

mkuu mimi ni mfanya biashara angalia hapa www.jajojo.com sijawahi kwenda kwa mchawi na naendelea vizuri sana. Ushauri- Ukikaa na mwizi utaiba pia, ukikaa kwa kinyozi utakatwa nywele siku moja. Hivyo achana na hao watu wanao husisha biashara na uchawi. Tafuta marafiki wapya wasio na imani hizo. Utafanikiwa tu, Kama mimi nimeweza kwa nini wewe ushindwe!.Mkuu unayaweza yote katika Mungu anayekutia nguvu za kufanya kazi/biashara kwa bidii.
 
Back
Top Bottom