Tujuzane: Je, ni samaki gani mtamu kuliko wote?

Huwa nasikia mgebuka ni mtamu sanaa. Sijawahi kumla nitamuonja siku moja nione.
Ila mgebuka wanasema wenyewe watu wa Kigoma upate yule fresh aliyetoka kwenye maji siyo samaki aliyekaa kwenye mafriji wiki

Mgebuka wapo overrated...wanafanana na vibua kwa ladha.

Hakuna kitu hapo

Kwa Ziwa Tanganyika, bora ule Kuhe...
 
Membe na Korongo wa lake Victoria. Wana mafuta unique halafu watamu sana. Macho ya Sato ni matamu na kichwa chake kwa ujumla. Salmon ni samaki namla nikiwa nchi za watu maana ndiye anakubali mwili wangu wa kuchagua. (Samahani ni miaka mingi tangu nimewala hao samaki wawili wa mwanzo labda majina nimechanganya). Ningu naye ni mtamu sana ila mifupa!
 
Sato ni habari nyingine wana ..

Ila ukija baharini sasa ndio habari ya sayari ingine.. Kuna tasi.. Kibua.. Sansuli(mbuzi bahari)

Jau saaana.
 
Salam kwenu.
Si mjuzi sana katika nyanja hizi..hivyo naomba kujua
Je, ni samaki gani mtamu kuliko wote? Mtaje !
1. Changu
2. Sato
3. Kibua
4. Sangara
5. Kambare
6. Perege
7. Migebuka
8. Pweza
9. ________
Kamongo ashinda nyama(alisikika mluo mmoja akisema)
 
Back
Top Bottom