Tujuzane Ishara za 'Kiuchawi' na "Kiuchuro' kutoka kwa Wanyama, Wadudu na Ndege kwa Binadamu (Mwanadamu)

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,823
2,000
1. Nyumba unayokaa kama unafuga Njiwa na ukiwa Unauguza Mgonjwa ndani ukiona Njiwa Wote wanaondoka anza kuweka Oda ya Jeneza kwa Mgonjwa wako kwani utake usitake atakufa tu.

2. Nyumba unayoishi kama unafuga Mbwa kuanzia Saa 5 Usiku na Saa 11 Alfajiri ukisikia wanabweka sana jua Wachawi wanaingia Kazini na wanarejea kutoka Kututesa kwa Kutulimisha Majarubani Usiku kucha.

3. Ukiona Paka kuanzia Watatu kwenda mbele wanalia mno ama Dirishani Kwako au Getini Kwako Nyumbani jiandae kupokea Taarifa mbaya ya Msiba.

4. Kwa Mwanaume kama kuna Mwanamke au Mkeo umempa Mimba ( Ujauzito ) na ukiona tu mara kwa mara Mjusi Mdogo anakutambaa na Kukurikia na hatoki sehemu ulipo jua hiyo Mimba imeshaharibika.

5. Ukiwa umepanga Kusafiri (na hii ni hasa ukiwa Kijijini) kisha Usiku ukasikia au ukaona Bundi ametua Darini ya Nyumba uliyopo aihirisha upesi hiyo Safari yako kwani ukilazimisha lazima Ndugu zako waanze Kuulizia Maturubai ya Kukuwekea Msiba Kwenu yanapatikana (yanakodishwa) wapi.

6. Usiku kati ya Saa 7 mpaka Saa 9 kama Kwako unafuga Kuku ukiwasikia tu wanalia kwa Sauti isiyo ya Kawaida jua hapo Kwako kuna Watu wabaya ( hasa Majambazi ) wamekuja kusema nawe ili uwape vyao na ukikataa 'Wakucharange' vizuri.

7. Ukiona Mnyama Simba kaenda Mbuga ya Ugenini ( ya mbali kama ya Botswana ) kaua Adui mara Mbili jua baada ya Wiki Moja Simba huyo huyo ( akiwa Kwake Tanzania ) akibahatika tena kukutana na Adui wa Kufanana na Yule basi atamuua vibaya, Kikatili tena kati ya mara Tano au hata Saba kwani Simba huwa wakiwa Mbuga ya Lupaso Temeke Dar es Salaam huwa anakuwa Mkali na mwenye Hasira zaidi.

Na nyie ongezeni pia na zenu tafadhali.
 

Panctual Fwenga Boy

JF-Expert Member
Jun 11, 2019
237
500
Ukiwa unaenda safari ukakutana na siafu wamebeba vitu vyeupe, safari yako itakua ya mafanikio.

NB:.Kama nimechanganya nikosolewe.
Sio siafu ni MANYANSALE mkuu,wadudu weusi mithili ya sungununu ila wao ni wakubwa kidogo,wana sumu kali wang'atapo ila hawaui na pia hutoa mlio fulani hivi pindi wachokozwapo na hutumiwa sana katika mafungamo ya visasi vya kishirikina
 

Deejay nasmile

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
5,070
2,000
Ukiwa unafuga mbwa alafu mara kwa mara unaona wanafanyana fanyana tu...ujue hata usiku kazi ya Yao ni hiyohiyo tu,hawalindi wala nini..fukuzia mbali haraka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom