Tujulishane wabunge wanamuziki

Jof3

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
656
313
Habari wanaJF
Kuna jambo Fulani huwa linanijia kichwani pale ninapoona wabunge machachari ambao pia walikuwa wanamuziki na wengine bado wanaimba muziki.
Najua kupitia uzi huu tutawajua wengi na kujifunza mengi. Mimi nawafahamu wachache ntawataja, kama nawewe mwana JF unawajua kutoka chama chochote au nchi yoyote basi tunaweza tukashare humu ikiwezekana tupia na jina la wimbo wake ikibidi na mistari kidogo.
Mimi naanza kama ifuatavyo
1. Mr.II (CHADEMA)- huyu jamaa napenda nyimbo zake nyingi ila nyimbo zake zinazonifurahisha zaidi ni
- kura yangu
- miaka chini ya 18
2. Professor J (CHADEMA)-huyu ni kichwa wa mashairi. Nakumbuka nyimbo zake nyingi sana ila kuna nyimbo ya singeli ya hivi karibu pia ameimba. Nyimbo iliyonikamata zaidi ni Zali la mentali, na NDIO MZEE. Ila hiyo nyimbo ya NDIO MZEE alikuwa anawaamsha viongozi wazembe na wenye kutoa ahadi za uongo. Sasa mwenyewe yuko mjengoni ,nimatumaini yangu atakuwa mfano bora.
- Kama kuna wengine tujulishane huenda tukamuamsha na muuza chipsi aingie mjengoni.

Nawasilisha.
 
kuna yule demu wa arusha aliimba mr politician cdm walitaka kumpa ubunge boyfriend akamuinglza chaka akaenda ccm mpaka leo analia
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom