Tujulishane ulitumia mbinu/dawa gani kupona ugonjwa uliokusumbua

ngunde11

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
682
889
Wakuu kama Mada hapo juu nia ni kushirikishana mbinu au dawa mbalimbali ambazo uliwahi kutumia na ukapata mafanikio ili na wengine wenye matatizo kama yako wawezi kupona au kujikinga

Mfano mimi nilipata tatizo la kukoroma nikilala tena kwa sauti kubwa sana yaani ilikuwa kero sana kwangu

Nilichojifunza mimi (uzoefu sio kisayansi) kukoroma hutokana na hewa kupita kwa shida kwenye njia yake pengine ni kutokana na uchafu kama kamasi au shingo kujikunja au pengine unene au mapafu kutofanya kazi vizuri kwangu hii ndio sababu kubwa.

Nilizofanya jitihada kadhaa kipindi hicho za kukabiliana na tatizo ikiwepo pamoja nakuweka mkono wangu mmoja juu ya kidevu ili kuisukuma shingo juu ili isijikunje mbinu inasaidia kwa muda ila ukigeuka tu usingizini unaanza tena kukoroma.

Nilikuja kujifunza kuwa kukoroma husababishwa na uwezo mdogo WA mapafu kufanya kazi yaani unapo lala ile hali ya kuvuta hewa ndani inapungua sana kulinganisha ukiwa macho, na hii inasabaibiswa na mapafu kukosa nguvu yake ya asili pengine sababu ya umri na sababu nyingine hapo juu

Suluhisho kufanya mazoezi ya kukimbia kuzunguka uwanja unaweza kuanza kidogokidogo kwa kuzunguka round moja utaongeza polepole angalau Mara mbili kwa wiki na hakikisha unatumia pua kupumua na SIO mdomo kwani mapafu yanafanya kazi vizuri ukitumia pua,na hakikisha wakati wa kuvuta hewa ndani mapafu yanajaa hewa na kifua kinapanda juu na wakati wa kupumua mapafu yanashuka,

Ila pia unaweza kutumia dawa za mafua kutoa ule uchafu wote kwenye kolomeo na sehemu tunazolala ziwe na mzunguko mzuri wa hewa

Natanguliza shukrani kama utapona kwa kutumia mbinu hii basi nijulishe na tuwajukishe na wengine na kama wewe ulishawahi kupona tatizo lolote basi tujulishe ulitumia njia gani.
 
Issue ya kuongea usingizini wakuu mnaichukuliaje, ni ugonjwa ama ni jambo la.kawaida? Linamhangaisha sana wife, ninaongea muda mrefu kana kwamba ninajizibizana na mtu, ijapo mie binafsi nakuwa sifahamu na hata ukiniuliza niliongea nn sijui yaani!
Sasa Kwa aliye wahi kukutana na changamoto hii na akaipatia suluhu, anaweza kututonya huo ufahamu au dawa..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom