Tujulishane lugha zinazotumiwa kwenye jamii, biashara, kazi na n.k

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,712
Baada kuishi sehemu tofauti kuna lugha kama code ambazo kama ufahamu basi kazi bure.

Lugha hizi mfano Kariakoo :-

*kimeo
- neno hili linatumika pale kama kitu kibovu au jambo baya au hatari,tatizo.
*kipusa - neno hili linatumika kwa mtu ambaye anatafutwa sana kwa maovu yake yoyote.
*jokeri - neno hili linatumika kwa wacheza kamali ambaye ni mtu wa kuliwa sana mchezo wa kamali.
*kimenuka - neno hili utumiwa kueleza hatari .
*sepa/tujisepe - neno hili utumiwa kuondoka haraka.
*ngoma ya road - neno hili utumiwa kueleza kuwa mali imeibiwa barabarani.
*vishandu/waroad - hawa ni wahalifu wanaotumia pikipiki.
*sankala - neno hili madawa ya kulevya
*slimisha - kubadilisha IMEI
*dodose - hawa ni wale matapeli wanawaibia wanawake kwa njia ya kutongoza na ngono.
*mchomoko - hawa ni wezi wa kuvizia majumba ya watu kama wametoka.
*king - kukamatika, kujichanganya mfano kwa matapeli,madalali na n.k
*saa ngapi - neno hili utumika kama kiasi gani na kuanzia laki
*sungura - shilingi elfu hamsini
*tunafanyeje/tuyajenge - neno hili ukisikia basi kama ni kosa au kuna jambo limalizike.ukisikia neno hili sana Polisi
*kiswaswadu - visimu vidogo ambavyo bei yake hipo chini.
*koro - mshamba au mjinga
*zwazwa - zaidi ya mjinga au mshamba
*malaika weupe - hawa ni matrafiki wa barabarani
*jeti rumo - kazi imeshindika ilisha kwenda na kurudi.
*ten - shilingi elfu kumi
*giza - hakuna la maana
*mende - hawa ni watu wanaopenda kwa mparange sana
*sababisha - fanya lolote kutatua au kuanzisha
* guarantee kisogo - neno hili kama dhamana ambayo mkimalizana ndo basi.
*kumeza - kutapeli au kuchukua bila ruhusa ya mtu.
*chekecha - chambua vizuri kiasi ulicho nacho ,”neno hili polisi lazime ulikute”

maneno mengine
 
*chuma chakavu-wanaweke ambao sio wazuri au wametumika sana.
*Oyaa hee -teyari kimenuka
*kimavi -mkosi
*kazi imenyooka -imekamilika,aina tatizo lolote,hipo safi.
*kakijambisha - kachokosha au kasabisha tatizo.
*kimenuka -tatizo limetokea au vurugu.
*ubaoni - utumika pale mtu yupo kituoni kabla kuingizwa chumba cha mahabusu.
*tepeta -kulainika kwa kipigo
*umesha mlisha sumu-umeongea nano ya kuchochea,kushambulia mtu.
*umemtia mtu ndimu -kumdanganya mtu ili kununua
*kazi inaliwa - biashara ya kitu inauzika au inafanyika
*mzungu - mtu ambaye jambo lolote kwenye biashara yupo poa
*kiroho safi- kutokuwa na kinyogo wala lawama.
*kifutio- k-vant
*mpenja - pombe kali
*kuteleza - kupata vitu vya bure kama kununuliwa bi,chakula,starehee na n.k
*kitonga - vitu vya bei rahisi au rahisi sana
*kulenga - kuvizia vitu vinavyouzwa nzuri ambayo ukauze.
*winga -dalali
*ganji-mgao wa udalali
 
*pakua -chukua au kuchukuliwa pesa au kitu.
*manyani - wezi wa mgodini wanaoingia usiku kwenye mashimo.
*ngumu kumeza-kazi inaweza kuwa na tatizo au biashara yenye tatizo.
*bwaga bwaga - kuuza mali kwa bei ya yoyote
*mkali - mtu mwenye uwezo wa fani,kazi,ufundi na mambo mengine.
*gari moshi-mvutaji wa sigara
*tembeza- supply
 
*kaoza -yupo mahabusu ua jela mda mrefu,kalewa chakari.
*kalambwa -kakamatwa
*mbwa -polisi
*pira-kesi kuletewa
 
*mwepesi- unaweza kumkabili kama biashara,nguvu au uwezo.
*mchelemchele -shoga
*king’amuzi -kifaa cha kufatilia track GPS
*kisu mkasi-kitu kisicho kuwa na tatizo lolote.
*soma upepo-kuangalia kinachoendelea
 
Back
Top Bottom