chizcom
JF-Expert Member
- Jul 31, 2016
- 7,581
- 15,718
Baada kuishi sehemu tofauti kuna lugha kama code ambazo kama ufahamu basi kazi bure.
Lugha hizi mfano Kariakoo :-
*kimeo - neno hili linatumika pale kama kitu kibovu au jambo baya au hatari,tatizo.
*kipusa - neno hili linatumika kwa mtu ambaye anatafutwa sana kwa maovu yake yoyote.
*jokeri - neno hili linatumika kwa wacheza kamali ambaye ni mtu wa kuliwa sana mchezo wa kamali.
*kimenuka - neno hili utumiwa kueleza hatari .
*sepa/tujisepe - neno hili utumiwa kuondoka haraka.
*ngoma ya road - neno hili utumiwa kueleza kuwa mali imeibiwa barabarani.
*vishandu/waroad - hawa ni wahalifu wanaotumia pikipiki.
*sankala - neno hili madawa ya kulevya
*slimisha - kubadilisha IMEI
*dodose - hawa ni wale matapeli wanawaibia wanawake kwa njia ya kutongoza na ngono.
*mchomoko - hawa ni wezi wa kuvizia majumba ya watu kama wametoka.
*king - kukamatika, kujichanganya mfano kwa matapeli,madalali na n.k
*saa ngapi - neno hili utumika kama kiasi gani na kuanzia laki
*sungura - shilingi elfu hamsini
*tunafanyeje/tuyajenge - neno hili ukisikia basi kama ni kosa au kuna jambo limalizike.ukisikia neno hili sana Polisi
*kiswaswadu - visimu vidogo ambavyo bei yake hipo chini.
*koro - mshamba au mjinga
*zwazwa - zaidi ya mjinga au mshamba
*malaika weupe - hawa ni matrafiki wa barabarani
*jeti rumo - kazi imeshindika ilisha kwenda na kurudi.
*ten - shilingi elfu kumi
*giza - hakuna la maana
*mende - hawa ni watu wanaopenda kwa mparange sana
*sababisha - fanya lolote kutatua au kuanzisha
* guarantee kisogo - neno hili kama dhamana ambayo mkimalizana ndo basi.
*kumeza - kutapeli au kuchukua bila ruhusa ya mtu.
*chekecha - chambua vizuri kiasi ulicho nacho ,”neno hili polisi lazime ulikute”
maneno mengine