charles kingunge
Member
- Aug 30, 2016
- 10
- 15
A
Yaani ningekuwa mie? Hee! Huoni hii ni fursa kwako? Tena tafuta house girk mremboooo! Wa kijijini kwao.Naona kichwa cha uzi huu kimejieleza vizuri.
Kwa kuanza, mke wangu mimi ni mwalimu wa Sekondari, anafundisha shule fulani Manispaa ya Temeke. Changamoto zinazonikabili mara nyingi ni Wife kuamka mapema sana na kuwahi kazini hasa siku ambazo anakuwa Mwalimu wa zamu.
Pia, kwa kipindi hiki kunakuwa na semina nyingi sana zinazizotolewa na viongozi wa elimu hasa Maafisa Elimu Manispaa, Afisa elimu Kata nk kuhusiana na jinsi gani wanaweza kuongeza ufaulu wa Watoto.
Hapa husababisa Wife kuchelewa sana kurudi nyumbani. Na mwisho kipindi cha mwisho wa Mwaka huwa anachaguliwa kufanya kazi ya kusahihisha mitihani ya Kidato cha Nne, kinachotokea hapa ni kwamba wakati yupo kule marufuku kuwa na simu mkononi. Kwa hiyo hakuna mawasiliano yoyote naye kwa kipindi chote anapokuwa kwenye hiyo kazi kwa mwezi mzima. Baba ndo unakuwa mama huku nyumbani.
Jinsi gani nakabiliana na changamoto hizi ni kumwamini, hii ndo nguzo kubwa katika Ndoa yetu. Naamini kwamba yupo kazini na kwamba namwacha afanye kazi. Upendo na amani vimetawala kati yetu na maisha yanaendelea.
Vipi mwenzangu unakabiliana vipi na changamoto hizi?