Tujiunge na kuanzisha JAMII FARM

Mgombezi

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
610
178
Wana JF!

Katika kuonyesha KILIMO KWANZA kwa vitendo, nimekuwa na wazo kwamba wana JF tunaweza kuunganisha nguvu zetu na kuwa na shamba la kisasa litakaloitwa JAMII FARM. Shamba hili liwe kumbwa sana na linapaswa kuwa la mfano. Shamba hili liwe na mifugo mbalimbali (kuku wa aina zote, ng'ombe (maziwa na nyama), mbuzi, bata mzinga na wengineo; pamoja na bustani za mboga mbalimbali. Hili ni wazo, nakaribisha mawazo ya wengine. Tuwaweza kutumia mfumo wa kuwa na hisa na watu kununua hisa.
 
Kilimo Kwanza ni nini? Nini misingi na malengo yake? Wakulima wadogo na wa kati wamefikiriwaje? Ukijibu maswali haya,ndio uje tupange huo mpango wako.
 
Mkuu mbona umemsahau Mbuzi Katoliki !.
 
Kilimo Kwanza ni nini? Nini misingi na malengo yake? Wakulima wadogo na wa kati wamefikiriwaje? Ukijibu maswali haya,ndio uje tupange huo mpango wako.
Inawezekana nisieleweke sana kwa kutumia kauli mbiu ya Kilimo Kwanza; lakini wazo langu linatokana na jinsi ninavyoona wana JF wengi wakitaka msaada wa kuanza kilimo na ufugaji. Hivyo badala ya kila mmoja kutafuta uwekezaji wa peke yake, nafikiri inaweza kuwa nafuu zaidi kwa kuunganisha nguvu. Haswa unapoangalia suala la kuajiri waatala, pembejeo za kilimo (kama tractors) n.k
 
Ni wazo, mdau na linaitaji uongozi wa JF ili kutuonganisha vizuri
 
QUOTE=Mgombezi:Inawezekana nisieleweke sana kwa kutumia kauli mbiu ya Kilimo Kwanza; lakini wazo langu linatokana na jinsi ninavyoona wana JF wengi wakitaka msaada wa kuanza kilimo na ufugaji. Hivyo badala ya kila mmoja kutafuta uwekezaji wa peke yake, nafikiri inaweza kuwa nafuu zaidi kwa kuunganisha nguvu. Haswa unapoangalia suala la kuajiri waatalam, pembejeo za kilimo (kama tractors) n.k

Kama ni ivyo,umeeleweka. Nadhani wadau watakupa mawazo mazuri zaidi ya namna gani ya kuimplement mpango huo. Ingawa kama mtoa wazo,ungekuja na mpango mkakati ulio kamili,then sisi wadau wengine tuujadili kwa kina.
 
Asante Sana Nyandaigobeko kwa kunielewa maana nilihisi wazo linaweza kuleta mgongano wa kisiasa. Nafikiri hapa JF tuna wataalamu mbalimbali; hivyo basi kwa kutumia taaluma tulizonazo ninaamini tunaweza kufanya jambo la kihistoria kwa vizazi vyetu vijavyo.

Kwa mawazo yangu nafikiri tungeanza na upatikanaji wa ardhi isiyopungua hekari 1000; hivyo wadau tungeanza kuchangia hapa na kutoa mapendkezo ya eneo husika ambalo linaweza kufaa kwa mradi huu mkubwa.
 
Tukimwingiza hapa tunaweza tukaleta mtafaruku wa kidini; wantasema JF ni wakristu. Tusielekee huko!

Sasa huo ndo mfugo unaolipa zaidi So kama hautakuwepo hapo shambani mi naenda kwenye biashara zingine........ kwaheri shamba halina dili hilo halina pokoloko............
 
Hivi shamba la ekari zaidi ya 1000 linaweza kupatikana wapi na utaratibu unaweza kuwa vipi katika kupata hati na gharama za umiliki.
 
Wana JF!

Katika kuonyesha KILIMO KWANZA kwa vitendo, nimekuwa na wazo kwamba wana JF tunaweza kuunganisha nguvu zetu na kuwa na shamba la kisasa litakaloitwa JAMII FARM. Shamba hili liwe kumbwa sana na linapaswa kuwa la mfano. Shamba hili liwe na mifugo mbalimbali (kuku wa aina zote, ng'ombe (maziwa na nyama), mbuzi, bata mzinga na wengineo; pamoja na bustani za mboga mbalimbali. Hili ni wazo, nakaribisha mawazo ya wengine. Tuwaweza kutumia mfumo wa kuwa na hisa na watu kununua hisa.

Huko nyuma kuna mtu alitoa wazo hilo na tukaunga mkono sana, na baadhi tumeanza tayari kkwa vitendo wazo hili,kwa hiyo mzee inawezekana kwa gharama kidogo zaidi. Sisi tunakwenda kwa mfumo wa estate kubwa.

Eka 1000 ni ndogo mno na hata saa hizi naweza kukwambia ziko wapi kanunue/tukanunue.
 
Malila nakushukuru kwa mchango wako; inaonekana tayari nyinyi mmeshajiunga na kuanzisha hiyo estate. Naweza kupata details za hicho kikundi ili nami niweze kujiunga.
 
Wazo zuri ,utekelezaji huwa mgumu.sisi waswahili huwa tunaunga mkono wa maneno matamu tu,then vitendo hatutekelezi hata chembe.mtafute malila and Co,watashauri ardhi kubwa ipo wapi Tz.
all the best,kwa sasa nimeamua kuanza na subsistence farming (eka 30tu) kilimo cha heka 1000Plus kitahitaji pesa nyingi,Tractors,Excavators na Combine Harvesters.
hapo ubia ndo utatakiwa
 
Ni kweli, lakini sasa ndio tunataka tuondoke kwenye maneno mengi vitendo vichache. Nimeleta wazo hili nikitegemea hapa JF kuna hazina za wataalamu hivyo tunaweza kushirikiana katika kujitengenezea huo mchakato na hatimaye kuweka katika utekelezaji.

Badala ya kutafuta wabia toka nje, hili tungeweza kuunganisha nguvu zetu sisi wenyewe.

Hivi maeneo ya Morogoro tunaweza kupata ardhi ya kutosha, vipi wadau wenye uzoefu na maeneo hayo. Kumbuka tunaangali hekari zaidi ya 1000.
 
Wana JF!

Katika kuonyesha KILIMO KWANZA kwa vitendo, nimekuwa na wazo kwamba wana JF tunaweza kuunganisha nguvu zetu na kuwa na shamba la kisasa litakaloitwa JAMII FARM. Shamba hili liwe kumbwa sana na linapaswa kuwa la mfano. Shamba hili liwe na mifugo mbalimbali (kuku wa aina zote, ng'ombe (maziwa na nyama), mbuzi, bata mzinga na wengineo; pamoja na bustani za mboga mbalimbali. Hili ni wazo, nakaribisha mawazo ya wengine. Tuwaweza kutumia mfumo wa kuwa na hisa na watu kununua hisa.

Halafu iwe kama ile hadithi ya Animal Farm; ubabe wa moderators uendelee, ushabiki wa members pale pale, halafu na hizi ID za a.k.a. zibakie lakini members waruhusiwe kuvaa kininja ili wasijulikane.

burka_0.jpg
attachment.php
 
Back
Top Bottom