Nimetafakari sana nakuona mtindo wa Siasa zetu unavyo pata mabadiliko hasa ndani ya chama chetu pendwa cha CCM .
Tangu mfumo wa siasa za vyama vingi ulipo anzishwa hapa Tanzania tumeona viongozi wa kisiasa katika chama wakitenda kwa mitindo mbalimbali , kabla ya uchaguzi wa 2015 tulishuhudia CCM ilipo ona ari na mapenzi ya watanzania kukichoka chama ,kutokana namfumo mbovu wa watendaji ndani ya serikali uliopelekea uchaguzi wa mwaka 2000 kuibuka na ushindi mwembamba ambao haujawahi kutokea,
Katibu Mkuu wa CCM wa wakati huo ndugu Abdrahaman Kinana akiwa na Katibu Mwenezi wa chama wakati huo Nape Nnawie, waliinuka wakaacha ofisi na kuelekea kwa wananchi moja kwa moja ili kujaribu kurejesha imani ya wananchi kwa chama. Kwakweli kwa jitihada walizo zifanya kwa kukosoa wazi wazi baadhi ya watendaji wa serikali,kwa kiasi Fulani wananchi ilirudisha imani kwa chama . Na ikumbukwe kuwa wakati hawa viongozi wakitenda haya upinzani ulikuwa nao unachukuwa kasi ya kujiimarisha sana.
Lakini baada ya mabadiliko yaliyo fanyika kwa kuwabadilisha katika nafasi zao na kuchukuliwa na Dr Bashiru na Polepole, tumeona mabadiliko yakijitokeza japo ni kweli kwamba kila uongozi huwa na mbinu zake za kiuongozi, hawa wamekuja na mbinu ambayo siyo ya kwenda kwa wananchi ila wao wamekuja na chamambinu ya kwenda kwa viongozi viongozi wa vyama vya upinzani na kuwashawishi wahame vyama vyao na kujiunga na chama chao,
Jambo la kujiuliza hapa ni kuwa unapo kwenda kwa viongozi na kuwashawishi wahame huku ukiwaacha maelfu ya wananchi wakiwa na mashaka makubwa hasa kwenye mfumo wa siasa zinazo endelea ndani ya nchi ambayo kwa kiasi kikubwa ni kwamba hata wana CCM wenyewe wanaziona kama zimekuwa kandamizi kwa vyama vya upinzani , kwani kama Taifa liliamua kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi basi ni wazi kuwa ilikuwa imekubaliana kupambana kwa hoja majukwaani na wala sio kuziba midomo ya vyama vya upinzani ili isiweze kunena.
Hivi kati ya hizi timu mbili kati ya ile ya Comrade na ya Dr ni ipi imeonyesha mafanikio ya kweli ya kidemokrasia halisi ?.