Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,603
- 29,743
Amani iwe kwenu wachambuzi jadidifu.
Ninaleta hoja kwenu ili tuelimishane ikibidi tukosoane ama kuwajibishana
Wanasiasa wengi kama siyo wote, wamekuwa wakionesha matendo yao fulani fulani kwa kificho au kwa uwazi kabisa.
Wamejenga mazoea ya kutumia watu wanaoitwa waganga wa kienyejj ili kupata vyeo vya kuchaguliwa au uteuzi. Wanasiasa hawa wengi wamehusika kutoa kafara mbalimbali hususani wanyama na hata wengine wametuhumiwa kuwatoa kafara watu wao wa karibu ili wapate wanachokikusudia.
Tumeona hata chaguzi nyingi za ndani ya chama kikubwa, watu wakitumia usaidizi wa ulozi kufanikisha malengo yao wachaguliwe. Wengi wa wanasiasa hao ni wasomi na wengine viwango vya juu. Lakini inapofika wakati wa kusaka vyeo wanaweka taaluma pembeni na kuwatumia waganga ambao wengi hawana hata elimu ya sekondari
Kitu cha ajabu ni kwamba wanasiasa hao hao wakishinda chaguzi au wakiteuliwa huwa wanatumia misahafu wakati wa kuapishwa. Misahafu hiyo inakemea uchawi na namna yoyote inayofanania uchawi.
tujjulize maswali.

- Je uchawi na ramli vina nafasi gani kwenye maendeleo ya Taifa letu?
- Je utendaji usioridhisha wa viongozi wetu ambapo hata walioteuliwa hawagusiki, hayo yanatokana na nguvu za uchawi huo?
- Wananchi kugojishughulisha kuhoji ama kutaka utatuzi wa athari za utendaji mbovu, nao wefubazwa na nguvu za uchawi ambazo ziliwslazimisha kuwapa kura viongozi wababaifu kwenye utendaji?
- Kwa nini wasomi ndiyo wanaongoza kwa idadi kubwa kwenda kwa wachawi kuroga ili wachaguliwe, wateuliwe ai waajirike?
- Una mtazamo gani kwenye eneo hili?
- Nini kifanyike?