Tujiulize; sinema ya Kova na Joshua Gitui,mtesaji a Ulimboka imeishia wapi?

Seif al Islam

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
2,156
638
sitaki kuamini kuwa ile sinema iliyoanzishwa na kamanda kova na bwana joshua gitui,mkenya aliyedaiwa kumteka na kumtesa ulimboka imeisha hivihivi.alifikishwa mahakamani kimyakimya bila watu kuona wala kujua.haikujulikana kawekwa gereza gani na kesi yake itatajwa tena lini.tuwe makini sana jamani hata na huyu aliyemuua mwangosi asije akatoweka kama huyu wa kova/ulimboka.
 
Watanzania tuna tabia ya,
1. Kusahau... Mkuu anaposema ni "upepo tu utapita"
alishaona mbali...

2. Watanzania tuna tabia hii, tuko radhi kuutafuta ukweli
hasa kuhusu tuhuma na mambo kama hayo na
tukishaupata huo "ukweli" tunaishia hapo na kusahau
NGUVU, MUDA,RASILIMALI iliyotumika kuutafuta
"UKWELI".. Hii inajidhihirisha kwenye Tume
mbalimabali, mikasa ya kila leo tunayoisikia na kuiona
n.k.

3. Ushabiki, ili mradi tu kila mtu aongee/atoe mawazo ya
jambo fulani, lakini hakuna njia sahihi ya kuiendea( a
way forward)!

With all that, na mengine mengi Watanzania tunaletewa story moja baada ya nyingine kama mtoto mdogo wa chini ya mwaka mmoja, ambaye akiwa anachezea kitu(mfano playing toy), na ukachukua toka mikononi mwake na kuficha nyuma ya mgongo HAKUMBUKI, na iwapo utaleta kitu kingine tofauti na alichokuwa anachezea muda huo huo, HATAMBUI kama kuna kitu kilikuwepo kabla ya hicho( EXISTENCE OF PREVIOUS EVENT)...na tumeridhika.
 
Tatizo la nchi hii ni kutawaliwa kwa matukio. Yaani kwasasa likitokea jambo tayari tunasahau habari za Mwangosi kama tulivyomsahau Dr Ulimboka!!!!
 
jamani hatujasahau bado ila tunaletewa filamu nyingi kwa wakati mmoja yani ni bandika bandua mpaka tunachanganyikiwa!!!
 
Tutoe maoni yetu katiba mpya iwe na kipengele cha kuwawajibisha viongozi wa wenye dhamana kama Kova kuwajibishwa kisheria wanapodanganya umma kama hii sinema ya huyu Mungiki fake!
 
Tatizo la nchi hii ni kutawaliwa kwa matukio. Yaani kwasasa likitokea jambo tayari tunasahau habari za Mwangosi kama tulivyomsahau Dr Ulimboka!!!!

Kuna tetesi tu kua dr uli yuko nje ya nchi na kapewa kitita chake fresh ili asiongee...ni tetesi tu
 
Kuna tetesi tu kua dr uli yuko nje ya nchi na kapewa kitita chake fresh ili asiongee...ni tetesi tu
Bahati nzuri ni tetesi, uhakika tulio nao ni kuwa yuko hapa hapa bongo ila familia yake imemzuia kuongea na vyombo vya habari. Wiki ilopita kuna mwandishi wa gazeti la Mwananchi kidogo achapwe na dadake Dr Ulimboka alipokwenda kwao kufuatilia hizi issues!
 
Picha la yule mtesaji wa Ulimboka Joshua Githindi kutoka kenya aliyetambulishwa na kamanda Kova, limefikia tamati baada ya mahakama ya kisutu kusema hausiki na kumuachia huru, japo alikamatwa tena jwa kosa la kusema uongo. Haya sasa tunasubiri 'BEHIND THE SCENE'
 
Movies nyingine huwa haina haja ya kuzifuatilia maana mwisho wake hujulikana mwanzoni.
 
Back
Top Bottom