johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,826
- 141,737
Tukiachana na zile sinema za kina Msukuma, Sugu, Kibajaji nk kule mjengoni ni vema tukajiuliza ni nani hasa mnufaika wa huu mfumo wa vyama vingi?...... Je ni wananchi, wanasiasa, serikali au ni " wamiliki" wa hivi vyama?!! Maana hapa tulipofika wabunge na madiwani wanaachia nafasi za uongozi wa kuchaguliwa bila kujali hasara wanayoisababisha kwa wananchi, nachelea kusema yawezekana mfumo wa vyama vingi hapa Tanzania ni wa " kipekee" kabisa na huenda hauna maslahi ya moja kwa moja kwa wananchi. Nawasilisha!