Tujiulize: Ni nani hasa ananufaika na mfumo wa vyama vingi hapa Tanzania?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,699
2,000
Tukiachana na zile sinema za kina Msukuma, Sugu, Kibajaji nk kule mjengoni ni vema tukajiuliza ni nani hasa mnufaika wa huu mfumo wa vyama vingi?...... Je ni wananchi, wanasiasa, serikali au ni " wamiliki" wa hivi vyama?!! Maana hapa tulipofika wabunge na madiwani wanaachia nafasi za uongozi wa kuchaguliwa bila kujali hasara wanayoisababisha kwa wananchi, nachelea kusema yawezekana mfumo wa vyama vingi hapa Tanzania ni wa " kipekee" kabisa na huenda hauna maslahi ya moja kwa moja kwa wananchi. Nawasilisha!
 
issac77

JF-Expert Member
Apr 26, 2013
2,549
2,000
kwa upande wa upinzani mbowe/lowassa wanufaikaji wa ruzuku, kwa upande wa kijani hawa ndio wanufaikaji zaidi sababu wanadiliki hata kutumia Mali,pesa ya umma kuendesha masuala yao ya chama
 
Jspmsl

JF-Expert Member
Aug 7, 2017
437
500
Tukiachana na zile sinema za kina Msukuma, Sugu, Kibajaji nk kule mjengoni ni vema tukajiuliza ni nani hasa mnufaika wa huu mfumo wa vyama vingi?...... Je ni wananchi, wanasiasa, serikali au ni " wamiliki" wa hivi vyama?!! Maana hapa tulipofika wabunge na madiwani wanaachia nafasi za uongozi wa kuchaguliwa bila kujali hasara wanayoisababisha kwa wananchi, nachelea kusema yawezekana mfumo wa vyama vingi hapa Tanzania ni wa " kipekee" kabisa na huenda hauna maslahi ya moja kwa moja kwa wananchi. Nawasilisha!
Ni wananchi tungejua wapi richmund, escrow na madudu mengi tu kama tungekuwa na bunge lile la ndiyo bwana. Huyu mkuu anajitahidi hivi kwa sababu kuna upinzani faida za upinzani ni mjinga pekee anayeweza kudharau lkn kwa sababu waTZ majinga yanasapoti kuzimwa upinzani. Je kwenye hizi siasa mnufaika nani? Kna mtu asiye na mapungufu asiulizwe, hakuna wenye tamaa ina maana kuna watakatifu wameingia mbn huko nyuma wana madudu.
Upinzani ni mhimu sana kuwepo hata nchi za kifalme serikali zinaendeshwa na wanasiasa ili kuleta ushindani katka kazi. Awazae upinzani hauna maana ni mjinga.
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,699
2,000
Enzi ya chama

Enzi ya chama kimoja alikuwepo mbunge pale Temeke akijulikana kama Masoud kama sikosei huyu aliibua ufisadi wa kivuko cha kigamboni so ufisadi hufichuliwa katika mfumo wowote!
 
nygax

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,082
2,000
Wanaonufaika na upinzani ni wapinzani wenyewe, maana kama wangekuwa hawanufaiki tangu 1992 wangekuwa tayari wameshajifuta kabisa kwenye ulimwengu wa siasa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom