Tujiulize kwa nini....?

GM7

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
492
24
Hili ni tukio lililotokea hivi karibuni huku Mbeya kama picha inavyoonekana
 
Attachments

  • kibaka1.JPG
    kibaka1.JPG
    92.6 KB · Views: 127
Ningekuwepo ningemuongezea. Wez sio watu. Wakikuwahi wanakuletea hasara.
 
Kwa sehemu kubwa inatokana na kuchoshwa na vibaka wengi au wezi wanapopelekwa kituoni au sehemu za usalama baada ya siku mbili tatu unawaona tena mitaani, ndio wananchi wanaona bora wajichukulie sheria mikononi japokuwa na lenyewe ni kosa.Je, wewe mwana JF unasemaje?
 
Nawapongeza hawa wakaz. Ukiwapeleka polisi hawakai sana wanatoka. Wakirudi uraian wanatusumbua. Mi naona bora wamefanya hivyo.
 
Hii ni hatari, na ndio adhabu inayowafaa maana vyombo vya kuwashughulikia vimelala.
 
Dah!kama ma great thinkers we have to think deep about ....thou all of us we know and we agree kua hawa vibaka nitatizo sugu lakini tukibariki mfumo huu wa kujichukulia sheria mkononi unaweza kutufikisha pabaya, naomba nieleweke " SITETEI UOVU "

Sio wote wanao fikwa na hali hii hua ni kweli wanastahili adhabu husika wengine huponzwa na misimamo yao ,chuki tu binafsi,kuzidiwa na nguvu ya kifedha , tukumbuke mtaani hivi sasa kuna vijana wengi sana wasio na ajira na ndio wanamapinduzi wakubwa nowdayz.

Binafsi naona kuhangaika na matawi sio njia sahii ya kuukausha mti ni vyema tukaliangalia tatizo kwa upana wake otherwise tukubali kujimaliza wenyewe kitaa .

Jeshi la police na serikali kwa ujumla ndio wakulaumiwa kwanza.
 
Kabisa kabisa,
 
Mimi ningemuongezea na vitunguu nimkahange.. maana wezi walichonifanya, wamenirudisha nyuma sana.
 
Inatisha unaweza akawa kaiba cm ya tochi tu wamempa adhabu kubwa sana,hv yule aliyeleta tair na mafuta na aliyemuwasha wana roho za kiubinadamu kweli?that is very bad na inatisha,ndio maana vitabu vinasema hukumu ya binadamu yaweza kuwa ndogo au kubwa tofauti na kosa that is why kuna siku ya hukumu
 
sasa sometymz huyo jamaa kasingiziwa coz kuna jamaa wa jamaa angu alinyang'anywa laptop na kupigiwa kelele za mwizi akapigwa mpaka kufa,kama hajakuibia wewe,saidia apelekwe kituoni then mengine yaendelee coz hauna uhakika wa 100% kwamba kaiba mpaka unpige na kumkaanga hivyo,anza sasa..........................kama huna uhakika usifanye
 
Nafikiri tulitakiwa kuwafanya hivi wale wanaotuibia maliasili zetu na kuzalisha tabaka la hawa vibaka badala ya kuwafanya hivi hawa vibaka.Maana kama kijana kama huyu angeandaliwa mazingira mazuri ya kuzalisha kwa jasho lake asingefikiria kuchukua profession ya wizi.Na inawezekana kabisa kuwa aliiba ili apate mlo wa siku hiyo.Sitetei vibaka maana binafsi wameshanitenda sana tu lakini wakati mwingine huwa nawahurumia kutokana na njaa waliyonayo na ugumu wa maisha.Ila kama anaiba ili apate hela ya mihadharati hiyo ni halali yake kabisaa..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom