Tujiulize kama Watanzania na Waafrika kwanini hatupati wabunifu wa kimataifa?

Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
3,416
2,000
Watanzania na Waafrica tuna akili na uwezo kama wenzetu wa mabara mengine. Lakini tujiulize hata ukiangalia mika 20 tu iliyopita ugunduzi sehemu mbalimbali umefanywa na watu wanaoishi nchi za Mangaribi ukiangalia kwenye teknologia pekee. Hata wahindi hatuchekani kuna wahindi wengi wamegundua vitu lakini wanaishi karibu wote nchi nyingine.

Sasa tujiulize je ni mazingira gani ambayo yameturudisha nyuma. Mimi naoumia sana Bill gates ambaye ni mgunduzi akija Tanzania ni kusaidia tu lakini sijawahi kusikia tunaomba tusadie mbinu au teknologia tunaomba pesa tu za Afya na chanjo.

Je tunatoa elimu ya kisasa kwa watoto kuwa wabunifu
Je Tunasikilizana au ni kupigana madongo tu bila tija.
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
47,622
2,000
Mfumo wa elimu, maisha, siasa na umasikini hauleti tija kwenye kuvumbua.

Unaweza ukawa na wazo zuri sana ila usipate nafasi ya kutekeleza kutokana na changamoto tajwa hapo juu.

Mfano; Maxmalipo, NALA n.k
 
Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
2,830
2,000
Uzi huu ukichangiwa na watu wengi nahama Jf. Humu post Ngono, kuchakata papuchi, udaku utaona.
Ndipo nimekuja kujua kuwa % kubwa ya waliomo na kupost humu ni wanafunzi au wapenda ngono halafu tunategemea maendeleo.

Hoja Fikirishi. Afrika tunaendelea kulaumu kuwa ukoloni uliturudisha nyuma lkn sitaki kuamini. Huenda ukoloni umetuhujumu kiakili na hadi leo tunatawaliwa KIFIKIRA. Mimi mpenzi wa Siasa lkn , kama kuna kitu kinatupotezea muda ni Siasa, na maneno kama Demokrasia, Haki za binadamu, Haki za ....... naziona kama upumbavu.
Nahisi huu mtego umewekwa na wazungu ili tutawalike kifikira, haiwezekani uniambie mtoto wangu awe na haki fulani , je unataka kumuaminisha mwanangu simpendi ila wewe uliye pembeni unampenda zaidi?

Maendeleo na Ubunifu yanahitaji mchalato iliwezekana kwa kulazimishana, kama wewe umesoma kitu fulani kwa kweli tunatakiwa kukulazimisha ku deliver kitu kulingana na hiyo elimu otherwise umetupa hasara ya kukusomesha.
Yanahitajika mapinduzi seriously ya Kifikira na Utendaji.

Afrika tunawaza K zaidi,
 
isajorsergio

Platinum Member
Apr 22, 2018
2,587
2,000
Mfumo wa elimu, maisha, siasa na umasikini hauleti tija kwenye kuvumbua.

Unaweza ukawa na wazo zuri sana ila usipate nafasi ya kutekeleza kutokana na changamoto tajwa hapo juu.

Mfano; Maxmalipo, NALA n.k
Haya ndio tunayoyahitaji si unaona kwa MaxMalipo na Nala imagine vumbuzi nyingi zaidi kama hizi kwa taifa?! Tutaweza kujiendesha bila kutegemea wauaji na wanyonyaji. Hata vikwazo vikija vitakuta tuna kila jambo la kutufanya tuishi bila stress.
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
47,622
2,000
Haya ndio tunayoyahitaji si unaona kwa MaxMalipo na Nala imagine vumbuzi nyingi zaidi kama hizi kwa taifa?! Tutaweza kujiendesha bila kutegemea wauaji na wanyonyaji. Hata vikwazo vikija vitakuta tuna kila jambo la kutufanya tuishi bila stress.
Huwezi kuvumbua 100% ya vitu unavyotumia nchini kwako.

Dunia ya sasa kuna kutegemeana. Huyu anazalisha kitu ambacho yupo bora zaidi.

Hata nchi za dunia ya kwanza wanategemeana kwenye kila kitu.
 
gataca

JF-Expert Member
Aug 15, 2015
344
500
Tupia habari za umbeya au kukwama kimaisha ushuhudie SMS zitavyochangiwa hapa kwa kasi ya 5 G
jibu ni kuwa elimu yetu haiko sawa ni ngumu kupata mtu achangie kitu kilicho juu ya uwezo wake na hata ambao wanacho cha kuchangia wanajua fika kuwa tech na mambo kama hayo hakuna mtu kutoka taifa jingine anaweza kutuletea teknolojia , kuna limit ya kiwango cha technolojia nchi kama zetu zimewekewa haziwezi kuvuka hiyo ni kwa maslahi yao (weupe) ukijaribu kukaidi yanaweza kukuta makubwa mfano ni kwa aliyewahi waziri mkuu wa italia wa wakati huo Aldo Moro(1963 -1968)na( 1974-76)Alienda kinyume na matakwa ya waamerika na warusi na walipomwambia akakaidi wakatumika Red brigade kumteka akielekea bungeni ambako kuna kura kupitisha mswada uliopelekea yeye kutekwa kwa zaidi ya miezi miwili hatimaye Aldo Moro akauwawa na hilo lilitokea siku chache baada ya kuambiwa na waziri wa mambo ya nje wa wakati huo wa marekan Henry Kissinger kuwa atatoa mfano kupitia yeye.
kwa mkabala huo usitegemee Bill Gate zaidi ya vyandalua na dawa za malaria au mpango wa uzazi atakusaidia teknolojia ukiwa na akili sana basi utapata The O-1 non-immigrant visa na EB-1 unaenda kutumia akili zako kuwatumikia
kingine hata kama nchi tukiamua kuwekeza kwenye mapinduzi ya kweli ya ya elimu viwanda (industries sio factories) na technolojia, zikianza figisu toka mataifa makubwa vijana wa leo wako overly braiwashed watamgeuka kiongozi atayetaka kufanya hivyo na kuungana na mataifa hayo kwani wengi wanaamini bila wao hatuwezi,ila siku mali asili tunazojivunia sana zikiisha au ikaja technolojia(mfano zao la katani) isiyovihitaji kizazi kitachokuwapo nyakati hizo kitatulilia sisi
TUMEKALIA POLITIKI
 
interlacustrineregion

JF-Expert Member
Oct 28, 2018
7,162
2,000
Asante sana kwa maarifa uliyonielezea hapa Chifu

Handsome Rob

Senior Member
Jan 12, 2017
124
500
Uzi huu ukichangiwa na watu wengi nahama Jf. Humu post Ngono, kuchakata papuchi, udaku utaona.
Ndipo nimekuja kujua kuwa % kubwa ya waliomo na kupost humu ni wanafunzi au wapenda ngono halafu tunategemea maendeleo.

Hoja Fikirishi. Afrika tunaendelea kulaumu kuwa ukoloni uliturudisha nyuma lkn sitaki kuamini. Huenda ukoloni umetuhujumu kiakili na hadi leo tunatawaliwa KIFIKIRA. Mimi mpenzi wa Siasa lkn , kama kuna kitu kinatupotezea muda ni Siasa, na maneno kama Demokrasia, Haki za binadamu, Haki za ....... naziona kama upumbavu.
Nahisi huu mtego umewekwa na wazungu ili tutawalike kifikira, haiwezekani uniambie mtoto wangu awe na haki fulani , je unataka kumuaminisha mwanangu simpendi ila wewe uliye pembeni unampenda zaidi?

Maendeleo na Ubunifu yanahitaji mchalato iliwezekana kwa kulazimishana, kama wewe umesoma kitu fulani kwa kweli tunatakiwa kukulazimisha ku deliver kitu kulingana na hiyo elimu otherwise umetupa hasara ya kukusomesha.
Yanahitajika mapinduzi seriously ya Kifikira na Utendaji.

Afrika tunawaza K zaidi,
Mkuu umeongea mengi lakin nadhani hujui tatizo ni nini, tatizo kubwa la nchi hii ni mfumo mzima wa elimu na utawala. Umesema kulazimishana.!! Kulazimishana ndo kuliko tufikisha apa tulipo hasa kwenye mfumo wa elimu na utawala kwa ujumla, laiti kama tungejengewa mfumo wa fikra huru tungekua mbali sana kimaendeleo kama taifa.

Tatizo lingne kuna watu wanaona wao ndo wanastahili kutawala nchi hii milele, ukiangalia hakuna fikra mpya mambo ni yaleyale miaka nenda rudi, mfano hata serikalini watu ambao ni wakweli na professional wanapigwa vita sana na wanasiasa vilaza, kwa mtindo huu hatuwez kua na taifa lanye watu wabunifu na hata ukibuni kitu kizur urasimu unakua mwingi na kukatishana tamaa kipuuzi tu. Kwahyo ili kuwa wabunifu na kua na fikra huru ni lazima tubadilishe mfumo wa elimu na utawala, hatuwez kupiga hatua kama tunakua na kiongoz mkubwa ambae hajui hata yuko ofisini kwa ajili gani, kiongoz hana vision wala mission yupo yupo tu.
 
N kweli mkuu lkn ELIMU yetu mitaala tumepcopy ya wazungu au tulisha kuwa na mitaala yetu kwa ELIMU ngazi gani?
Je ina maana nchi zoote za Afrika hakuna hata moja yenye utawala bora? kam ndio basi waafrika wote ni wa kutawaliwa hawawezi kujitawal
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
1,342
2,000
Watanzania na Waafrica tuna akili na uwezo kama wenzetu wa mabara mengine. Lakini tujiulize hata ukiangalia mika 20 tu iliyopita ugunduzi sehemu mbalimbali umefanywa na watu wanaoishi nchi za Mangaribi ukiangalia kwenye teknologia pekee. Hata wahindi hatuchekani kuna wahindi wengi wamegundua vitu lakini wanaishi karibu wote nchi nyingine.

Sasa tujiulize je ni mazingira gani ambayo yameturudisha nyuma. Mimi naoumia sana Bill gates ambaye ni mgunduzi akija Tanzania ni kusaidia tu lakini sijawahi kusikia tunaomba tusadie mbinu au teknologia tunaomba pesa tu za Afya na chanjo.

Je tunatoa elimu ya kisasa kwa watoto kuwa wabunifu
Je Tunasikilizana au ni kupigana madongo tu bila tija.
Nikukosoe kidogo.Elimu haifundishi ubinifu bali inaamsha 'instinct' vinginevyo marekani ulaya wangejaa wabunifu.Wabunifu duniani ni kama 2% ya watu wote.Zipo theory kadhaa zinaeleza chanzo cha ubunifu lakini hakuna mtazamo unaofafana.
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
1,342
2,000
Mkuu umeongea mengi lakin nadhani hujui tatizo ni nini, tatizo kubwa la nchi hii ni mfumo mzima wa elimu na utawala. Umesema kulazimishana.!! Kulazimishana ndo kuliko tufikisha apa tulipo hasa kwenye mfumo wa elimu na utawala kwa ujumla, laiti kama tungejengewa mfumo wa fikra huru tungekua mbali sana kimaendeleo kama taifa.

Tatizo lingne kuna watu wanaona wao ndo wanastahili kutawala nchi hii milele, ukiangalia hakuna fikra mpya mambo ni yaleyale miaka nenda rudi, mfano hata serikalini watu ambao ni wakweli na professional wanapigwa vita sana na wanasiasa vilaza, kwa mtindo huu hatuwez kua na taifa lanye watu wabunifu na hata ukibuni kitu kizur urasimu unakua mwingi na kukatishana tamaa kipuuzi tu. Kwahyo ili kuwa wabunifu na kua na fikra huru ni lazima tubadilishe mfumo wa elimu na utawala, hatuwez kupiga hatua kama tunakua na kiongoz mkubwa ambae hajui hata yuko ofisini kwa ajili gani, kiongoz hana vision wala mission yupo yupo tu.
Nikuulize kitu, kwani ulaya walipokuwa wanabuni teknolojia karne ya 18 walikuwa wanaelimu kubwa kama tulionayo sisi watanzania na waafrika kwa sasa? Je watanzania waliosoma nje wamebuni nini? Je tukipeleka watoto nusu ya population tutakuwa wabunifu sana? Je kwa nini nchi nyingi tu za ulaya hazifanyi ubunifu kuna shida gani? Suala la ubunifh ni kama suala la maendeleo ni complex issue ambayo haitakiwi kutamkwa kjuju tu.Nimefuatilia kwa kina sana China na Iran jinsi walvyofikia kiwango cha juu cha ubinifu,haitaji maneno maneno na wala sio jambo la mtu mmoja.Kuna mlolongo wa matukio.
 
moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,278
2,000
Watanzania na Waafrica tuna akili na uwezo kama wenzetu wa mabara mengine. Lakini tujiulize hata ukiangalia mika 20 tu iliyopita ugunduzi sehemu mbalimbali umefanywa na watu wanaoishi nchi za Mangaribi ukiangalia kwenye teknologia pekee. Hata wahindi hatuchekani kuna wahindi wengi wamegundua vitu lakini wanaishi karibu wote nchi nyingine.

Sasa tujiulize je ni mazingira gani ambayo yameturudisha nyuma. Mimi naoumia sana Bill gates ambaye ni mgunduzi akija Tanzania ni kusaidia tu lakini sijawahi kusikia tunaomba tusadie mbinu au teknologia tunaomba pesa tu za Afya na chanjo.

Je tunatoa elimu ya kisasa kwa watoto kuwa wabunifu
Je Tunasikilizana au ni kupigana madongo tu bila tija.
Nikusahishe, siyo miaka ishirini tu ni tokea dunia imeumbwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom