Tujiulize baada ya Mzee Mwanakijiji kuhoji kwanini TISS hawakuwajibika kwa hili?

nchonga aliyebaki

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
573
823
Tunapozungumzia idara ya Usalama wa Taifa na jinsi imeiangusha serikali yetu na kuweka usalama wa taifa letu hatarini nafasi ya Bw. Apson Mwang'onda haiwezi kupuuzwa. Baadhi ya matukio yaliyotokea na kuruhusu ufisadi nchini yalitokea wakati wa "ulinzi" wake na hatujui ni kwa kiasi gani alisimamia idara hiyo katika Usalama wa Taifa.

Wakati umefika na huyu naye ajibu, alifanya nini kuiimarisha idara hiyo na kuhakikisha inajijenga sawasawa kukabiri matishio ya ulimwengu wa utanda wazi?

Kwa vile Rada ilinunuliwa wakati wa uongozi wake wananchi wana haki ya kujua ni kwa kiasi gani idara yake ilishiriki katika kuhalalisha mauzo ya kurushwa kwa Vithlani? Zaidi ya yote binafsi ningependa kujua mambo yafuatayo kuhusu idara ya TISS enzi za Apson:

a. Walijua nini kuhusu Saileth Vithlani yule Dalali aliyetoweka kwa kupanda ndege baada ya kuwaaga?

b. Idara ya Usalama wa Taifa ilijua nini kuhusu Jeetu Patel na uanzishaji wa banki ya Azania wakati Bw. Patel alishawahi kufilisi moja ya makampuni yake na sheria ya Fedha ilikuwa hairuhusu mtu aliyefilisiwa kuingia katika sekta ya Fedha? Kwanini Patel alipewa exception?

c. Apson alijua nini kuhusu kitendo cha Rais Mkapa na Waziri wake wa Nishati kutumia vyeo vyao kujinufaisha na kujigawia mgodi wa Kiwira?

Je yawezekana matatizo yetu mengi ya kiusalama yametokana na uongozi wa ndugu huyu na wakati wake wa kujibu umefika ili kina RO wajifunze kutokana na makosa?

Hayo aliyaandika mwanakijiji kushangaa kwanini hasa yatokee kama kuna TISS Safi?

Pili kuondoka kwa Apson Mwangonda kumerekebisha yaliyokuwa yameenda tenge?

Apson: The Beginning of TISS's Failure...
 
Kwa ufahamu wako TISS wanamkamata mtuhumiwa au muhusika wa tuhuma? Kwa ufahamu wangu mdogo idara hiyo ni waonaji tuu! kiufupi ni "idara ya wambeya" baada ya Hapo kuna vyombo vingine vyenye mamlaka kushughulika wenyewe hujiita "Jicho" !!

Sasa kama kuna ufisadi I think a proper authority to answer labda Takukuru au polisi lakini sio hao "wambeya" they can do nothing though they can see!
 
Bila shaka umeongea vizuri sana mkuu. TISS ni jicho la kuona mbali na baada ya kuona huwa wanashauri nini kifanyike kisha watekelezaji sio TISS tena bali ni polisi, TAKUKURU, JWTZ na Mamlaka ya nyinginezo kama vile mamlaka ya madawa ya kulevya.
 
Labda sasa wabadilishe I sheria uundwaji wa TISS kama tunataka wawe wanakamata na kushitaki wenyewe! La sivyo sheria ya sasa wao ni wambea tu kupika majungu na umbea kwa sana!! Info zote za watu na kila kitu wanazo.....issue jinsi kuzifanyia kazi......kwa serikali wanayompelekea hizo info!! Kosa lao lipi?? Wakisema walishauri na data zipo.......
 
Fungueni kesi kama mnao ushahidi mzuri.

Ila hiyo Idara imefeli mno mno na kwa sehemu tunapitia matatizo mengi kwa vile tu hawakutenda kazi zao kwa weledi na muda stahiki.

Hakuna namna uniambie wako kazini halafu huyo aliyeketi hapo king alipita kwenye chekeche lao, how???
 
Hao siku hizi kazi yao kubwa ni kuteka na kuua watu tu
kuna wanaotumia kofia yao na kujifanya wao ndio TISS, ndio maana weledi umepotea huku TISS ikipoteza uaminifu kwa jamii kutokana na WAHALIFU WANAOJIFANYA kuwa wao ndio TISS kutekeleza jinai na UHALIFU wao ULIOKUBUHU.
Vinginevyo iwe wanatumika kisiasa na wanasiasa uchwara.
Twafwaa
 
Kabla hujaandika utumbo wako embu itafute na kuisoma Sheria ya Usalama wa Taifa no. 5 ya mwaka 1975 kama sio 1995 alaf usome majukum yake
 
Tunapozungumzia idara ya Usalama wa Taifa na jinsi imeiangusha serikali yetu na kuweka usalama wa taifa letu hatarini nafasi ya Bw. Apson Mwang'onda haiwezi kupuuzwa. Baadhi ya matukio yaliyotokea na kuruhusu ufisadi nchini yalitokea wakati wa "ulinzi" wake na hatujui ni kwa kiasi gani alisimamia idara hiyo katika Usalama wa Taifa.

Wakati umefika na huyu naye ajibu, alifanya nini kuiimarisha idara hiyo na kuhakikisha inajijenga sawasawa kukabiri matishio ya ulimwengu wa utanda wazi?

Kwa vile Rada ilinunuliwa wakati wa uongozi wake wananchi wana haki ya kujua ni kwa kiasi gani idara yake ilishiriki katika kuhalalisha mauzo ya kurushwa kwa Vithlani? Zaidi ya yote binafsi ningependa kujua mambo yafuatayo kuhusu idara ya TISS enzi za Apson:

a. Walijua nini kuhusu Saileth Vithlani yule Dalali aliyetoweka kwa kupanda ndege baada ya kuwaaga?

b. Idara ya Usalama wa Taifa ilijua nini kuhusu Jeetu Patel na uanzishaji wa banki ya Azania wakati Bw. Patel alishawahi kufilisi moja ya makampuni yake na sheria ya Fedha ilikuwa hairuhusu mtu aliyefilisiwa kuingia katika sekta ya Fedha? Kwanini Patel alipewa exception?

c. Apson alijua nini kuhusu kitendo cha Rais Mkapa na Waziri wake wa Nishati kutumia vyeo vyao kujinufaisha na kujigawia mgodi wa Kiwira?

Je yawezekana matatizo yetu mengi ya kiusalama yametokana na uongozi wa ndugu huyu na wakati wake wa kujibu umefika ili kina RO wajifunze kutokana na makosa?

Hayo aliyaandika mwanakijiji kushangaa kwanini hasa yatokee kama kuna TISS Safi?

Pili kuondoka kwa Apson Mwangonda kumerekebisha yaliyokuwa yameenda tenge?

Apson: The Beginning of TISS's Failure...
Tunapozungumzia idara ya Usalama wa Taifa na jinsi imeiangusha serikali yetu na kuweka usalama wa taifa letu hatarini nafasi ya Bw. Apson Mwang'onda haiwezi kupuuzwa. Baadhi ya matukio yaliyotokea na kuruhusu ufisadi nchini yalitokea wakati wa "ulinzi" wake na hatujui ni kwa kiasi gani alisimamia idara hiyo katika Usalama wa Taifa.

Wakati umefika na huyu naye ajibu, alifanya nini kuiimarisha idara hiyo na kuhakikisha inajijenga sawasawa kukabiri matishio ya ulimwengu wa utanda wazi?

Kwa vile Rada ilinunuliwa wakati wa uongozi wake wananchi wana haki ya kujua ni kwa kiasi gani idara yake ilishiriki katika kuhalalisha mauzo ya kurushwa kwa Vithlani? Zaidi ya yote binafsi ningependa kujua mambo yafuatayo kuhusu idara ya TISS enzi za Apson:

a. Walijua nini kuhusu Saileth Vithlani yule Dalali aliyetoweka kwa kupanda ndege baada ya kuwaaga?

b. Idara ya Usalama wa Taifa ilijua nini kuhusu Jeetu Patel na uanzishaji wa banki ya Azania wakati Bw. Patel alishawahi kufilisi moja ya makampuni yake na sheria ya Fedha ilikuwa hairuhusu mtu aliyefilisiwa kuingia katika sekta ya Fedha? Kwanini Patel alipewa exception?

c. Apson alijua nini kuhusu kitendo cha Rais Mkapa na Waziri wake wa Nishati kutumia vyeo vyao kujinufaisha na kujigawia mgodi wa Kiwira?

Je yawezekana matatizo yetu mengi ya kiusalama yametokana na uongozi wa ndugu huyu na wakati wake wa kujibu umefika ili kina RO wajifunze kutokana na makosa?

Hayo aliyaandika mwanakijiji kushangaa kwanini hasa yatokee kama kuna TISS Safi?

Pili kuondoka kwa Apson Mwangonda kumerekebisha yaliyokuwa yameenda tenge?

Apson: The Beginning of TISS's Failure...
kwa Nini tujadiliwe ,tuulizwe Na kuhojiwa? Sasa Ngoja tukutafute Halafu utueleze vizuri!
 
Hivi tangu lini TISS wakitoa ripoti zao huwa zinawekwa hadharani?? Haijawahi kutokea kwa Tanzania chombo kama TISS kikaeleza ripoti zake za kikazi hadharani.

Hakuna ushahidi wowote ule kwamba TISS waliona madudu yakifanyika na hawakuchukua hatua husika. Inawezekana kabisa hatua zilichukuliwa na wao TISS wakatoa ripoti yao kwa vyombo husika lakini hivyo vyombo ambavyo ni Jeshi la Polisi na TAKUKURU ndiyo havikufanya kazi kama zinavyotakiwa aidha kwa shinikizo kutoka mamlaka za juu au kwa uzembe.
 
Enzi za JKN watu hawa walikuwa wanatafutwa kwa usiri kabisa na wanasomoeshwa na Serikali na walikuwa wanafanyiwa vetting yakutosha.Leo mtoto wa naomba,shangazi,bibi nk nk uajiri wao hauzongatii tena weledi wala hulka au tabia ya mtu bali unajua vipi muajiri au Mtawala gani unafahamiana naye.

Kama taratibu zitafuatwa yawezekana tunaweza kuirudisha tena
 
Back
Top Bottom