Tujitahidi sana kusoma vitu vinavyotupasa kusoma. Dili nzito zinakuwa kwenye maandishi na si maneno matupu

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,205
22,255
Natumaini mko poa.

Nawasalimu katika jina la Chama Cha Mapinduzi. Chama kiendelee. Leo tena nimeona niandike kuhusu jambo la kusikitisha sana ingawa linachukuliwa kikawaida. Tukiachana na hili tatizo la kuchanganya "R" na "L" kuna tabia nyingine hatari zaidi.

Kama mjuavyo kwa miaka mingi nchi yetu imeingia kwenye majanga ya watu kusaini mikataba bila kusoma vizuri na kuielewa. Sababu kuu ikiwa ni uzembe na pengine mara chache kutoelewa kilichoandikwa.

Sasa hii tabia kwa siku za karibuni imezidi kuimarika kwa vijana wengi. Wamekuwa wazembe kusoma hata ujumbe tu wa kwenye simu.

Mtu unamtumia msg lakini baada ya muda anakupigia kukuuliza kitu ambacho kilikuwa na ufafanuzi wa kutosha kwenye msg hadi inabidi umuulize kama msg alisoma. Hata hapa JF mtu anaona kichwa cha habari na kukimbilia kuandika maoni bila kusoma na kuelewa kilichoandikwa.

Huko Instagram na Facebook ndo majanga zaidi. Watu hawasomi kabisa caption. Juzi hapa kuna mtu nimeona anatangaza biashara yake nikaamua nimtumie list ya vitu ninavyotaka kwake.

Vitu vya mwanzo wa list alikuwa hana lakini vya katikati hadi mwishoni anauza. Akanijibu haraka hivi vitu hatuna. Ikabidi nimuulize hiyo document umeisoma yote ndo akakurupuka. Kiukweli hiyo kazi nikapeleka kwingine sababu nilishindwa kuvumilia uzembe ule.

Ndugu zangu nawasihi sana tujitahidi sana kusoma vitu vinavyotupasa kusoma. Dili nzito zinakuwaga kwenye maandishi na sio maneno matupu.
 
na ndomana tulio soma darasa la kwanza C tulianza na somo la kusoma na kuandika... ukijua kusoma tu tayari una asilimia 60 za kufaulu na maisha
 
Naombeni soft copy ya THE SECRET TEACHINGS OF THE MASONIC LODGE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom