Biggs
JF-Expert Member
- May 3, 2014
- 1,914
- 2,037
The best way is to Sly like a Fox & Trust nobody.Nipende kuwaasa vijana walioko huko makazini kuwa waangalifu sana na hawa unaowaita wafanyakazi wenzako, mara rafiki zako.
Wengi wao wamejaa unafiki na hawa ndio watu wa kwanza kukuchongea ama kukushuhudia uongo pale linapotokea la kutokea kazini.
Tujitahidi sana kuwa na mipaka na hawa watumishi wenzetu, usiruhusu sana wakuzoee ama wakufahamu sana kiundani, maana wengine ni wachota taarifa hivyo basi jitahidi sana ufanye kazi yako kwa ufanisi muda wa kuondoka kazini ukifika ondoka acha kuweka vikao vya kijinga jinga na wafanyakazi wenzako utanishukuru sana.
Mwisho, tuwe makini huko makazini vijana wa sasa wamejaa majungu kushinda wazee.