Tujitafakari upya ama tujihukumu kama Taifa

Mheikungu

JF-Expert Member
Oct 15, 2018
214
448
Wakuu habari za jioni hii. Poleni na majukumu ya weekend hii iliyojaa simanzi kufuatia vifo vya watanzania wenzetu zaidi ya 70 huku vikitengeneza majeruhi zaidi ya 60 kwa ajali ya moto huko Msamvu Morogoro.

Ninawiwa kuandika haya huku moyo ukiwa mzito kutokana na mandhari ya ajali ile.

Msingi wa andiko langu unasimama katika mambo matatu.

1. Chanzo cha ajali ya gari lile tunaambiwa ni dereva wa lori kujaribu kumkwepa bodaboda. Hawa ndugu zetu na wadogo zetu wamekuwa ni tatizo. Hawajali sheria na hawajielewi, japo sio wote. Tufanyeje ili waelewe kuwa hii ni ajira kama ajira zingine?

2. Baada ya lori kuanguka, makumi kwa mamia ya watanzania wanyonge walibeba madumu na vikombe kwenda kuchota mafuta wakijua kuwa neema imeshuka kutoka mbinguni kama kile chakula kiitwacho Mana kwa wana waisraeli.

Hiki sio kiashiria chema kwa nchi. Inaonyesha kuwa wananchi wana njaa na hawajui riziki yao wanaipataje ndio maana wakaamua kujitoa muhanga kutafuta ridhiki by hooks and croock. It was a "do or die" kama bahati ingekuwa upande wa "do" wangekula sikukuu ya Eid el Hajj na familia zao vizuri kwa heshima kubwa kwa mapambio kuwa wanajua kutafuta chenchi, mitaa ya mafisa, sabasaba, Mazimbu, Modeko, Nanenane, Kilakala, Tubuyu,Kihonda bila kusahau vijiji vya jirani kama Mindu, Sangasanga, Kipera, Mzumbe,MELELA hadi Wami Sokoine mpaka Dakawa vingejaa vicheko na nderemo kwa machangudoa na ma barmaids JUST KIDDING. Lakini bahati mbaya imekuwa upande wa die kwenye ile "do or die" WAMEKUFA na zile mishemishe zimeishia pale Kola hills alipowaaga PM Kassim Majaliwa. Very sad

3. Jeshi letu la polisi haliwezi kuachwa kutupiwa lawama katika hili.

Nimeona video clip ya kabla moto haujawaka, inaonekana wazi gari lilianguka muda mrefu na wahanga wakawa wamejisahau wakawa wanachota mafuta kama maji.

Polisi ni usalama wa raia. Walikuwa wapi? Kama wangetimiza wajibu wao wa kulinda raia na mali zao, je janga hili lingetokea? Hawapaswi kuwajibika? Wale polisi jamii na polisi kata wanakaa wakisubiri intelijensia ya uvunjifu wa amani kwa vyama vya upinzani peke yake? Kwa style hii kama majeshi yetu yanashindwa kujua mahali penye tatizo katikati ya mji, ingekuwa ni kijijini si kingeteketea chote? Najiuliza maswali ambayo sina majibu.

Tujitafakari kwamba je tuna haja ya kuwa na jeshi la polisi blind namna hii?
Fire and rescue team mlifanya kazi yenu sawasawa?
Yale maderaya ya kulinda usala pale eneo la ajali leo jumapili ni ya nini wakati ajali ilipotokea jana hamkuweza hata kufika na deffender.

Tujitafakari ama tujihukumu.

Pumzikeni WANYONGE najua mlienda pale kutafuta pesa,

Nendeni kwa amani
 
Polisi mmoja wa Tanzania anawajibika kuwatumikia raia 10000 kwaiyo kabla ya kuwalaumu polisi tuanzie kuangalia polisi wetu walivyo na kazi kubwa
 
Back
Top Bottom