Tujitafakari: Kwanini wananchi wanyonge wamlilie Hugo Chavez na hayati Magufuli?

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
4,213
2,000
Chozi la mnyonge halina thamani? Hapana Mungu huwa analiona.

Kwa nini Hugo Chavez na Hayati Magufuli waliliwe na wanyonge kiasi cha kushangaza dunia?

Mbona George Bush snr hakuliliwa na wanyonge?

Siasa zina mambo mengi sana. Ila mengi ni mabaya.
image_search_1620497847343.jpg
image_search_1620497802583.jpg
 

kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,198
2,000
Sababu ni rahisi kuwaproganda kuliko makundi mengine.
Mnyonge ni futureless person yaani mtu hoe hae asiye na mbele wala nyuma na hana mawazo mengine zaidi ya kula.Wanyonge ni mtaji wa wanasiasa uchwara wanaosababisha watu wawe wanyonge Ili wawatumie kisiasa.
 

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,388
2,000
Mnyonge ni mtu gani? Mnyonge ni mtu anaye nyimwa haki yake. Mnyonge ni mtu ambaye anakandamizwa na utawala akihangaika kulima, mazao yake yanaporwa, au anapangiwa bei ya kuuza, au anapangiwa sehemu ya kuuza. Hayuko huru kufanya kazi zake.

Mfanyakazi mnyonge hapandishwi mshahara. Anatumikishwa. Hana sauti, hawezi kudai haki. Hawezi kuchagua kiongozi anaye mpenda maana kura yake inaporwa. Eneo lake na nyumba yake inachukuliwa na serikali bila kulipwa fidia. Akifikwa na majanga ya asili kama matetemeko au mafuriko serikali haimpi msaada inasema siyo iliyoleta majanga.

Akilalamikia malipo ya choo anaambiwa akae na mavi yake.

Mnyonge hama sauti, hasikilizwi.

JPM alitengeneza wanyonge ili awe kiongozi wa wanyonge. Fundi mkuu akafanya yake.

Serious kiongozi yeyote anayeweza kujisifu kuwa ni kiongozi wa wanyonge anatakiwa akataliwe. Maana kiongozi mzuri anawatoa watu kwenye unyonge.
 

masaka kwetu

Member
Jun 6, 2020
66
150
Huyu yawezekana ni wale waliochinjiwa baharini na utawala wa mwamba! Yawezekana aliamini kuwa ktk maisha yake hata kuja kuguswa na kiongozi yeyote wa serikali..take my word brooo. Fuata njia iliyo sahihi ktk maisha yako! Yupo uncle mwingine anakuja! Angalia watoto wako wasije wakalipiga kabuli lako mawe kwa kuwaaribia future yao.
 

gataca

JF-Expert Member
Aug 15, 2015
619
1,000
Sababu ni rahisi kuwaproganda kuliko makundi mengine.
Mnyonge ni futureless person yaani mtu hoe hae asiye na mbele wala nyuma na hana mawazo mengine zaidi ya kula.Wanyonge ni mtaji wa wanasiasa uchwara wanaosababisha watu wawe wanyonge Ili wawatumie kisiasa.
sasa kwanini wanasiasa makini na wanofanya vyema kuliko wanasiasa uchwara hawafanikiwi kuwavutia hilo kundi lisilo mbele wala nyuma huwa wanakosea wapi?
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,607
2,000
Chozi la mnyonge halina thamani? Hapana Mungu huwa analiona.

Kwa nini Hugo Chavez na Hayati Magufuli waliliwe na wanyonge kiasi cha kushangaza dunia?

Mbona George Bush snr hakuliliwa na wanyonge?

Siasa zina mambo mengi sana. Ila mengi ni mabaya. View attachment 1777899 View attachment 1777901
Ni kawaida wapambe wa madhalimu kuaandaa waliaji ili kuhadaa umma kuwa walikuwa wanakubalika sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom