marveljt
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 1,503
- 1,479
Wengi wetu tuliohapa tuko vyama tofauti.wengine kwa kulipwa na wengine kwa utashi wao.Watanzania tukubali mwaka 2015 tuliingia chaka kwa kuchagua viongozi,siyo tawala wala upinzani. Wabunge kazi yao ni kuishauri,kuisimamia serikali pamoja na kutetea haki za watanzania.
Leo hii serikali pamoja na wabunge wote wameungana na kutetea maslahi yao. Hakuna hata mmoja ambaye kweli amejithatiti kumsaidia mnyonge. Yanayoendelea ni sababu yetu sisi tuliopiga kura hakuna wa kumlaumu.Bado hapajatokea kiongozi ambaye yuko radhi kumsaidia mtu.
Lengo la uchaguzi ni ili kupata kiongozi atakayekutetea au kukusaidia katika jambo fulani. Vyama vya siasa viko kwa ajili ya wananchi wote kiujumla vilevile vyama vya wafanyakazi vipo katika malengo ya kuwasaidia wafanyakazi.
Mfano; Vyama vya sheria vipo kwa ajili ya kujilinda wenyewe pamoja na kutetea haki na amani. Leo hii zaidi ya matamko hakuna tija.
Wanaoumia zaidi ni wale wenye uelewa kuliko wasio na uelewa kwani wao wanajua fika ni kwa namna gani mambo yanavyopindishwa. Kikwete baadhi walimwita dhaifu ila leo hii hata wenye elimu za Poor Head Department ndiyo wamekuwa dhaifu zaidi.
Wamesoma ili kuisaidia nchi ila leo ndiyo wamekuwa mzigo kwa nchi. Yatupasa kuanza kujitafakari mwaka 2020. Mpaka muda huu hakuna chama au mwanasiasa ambaye anaumwa kwa matatizo ya wananchi na ndiyo maana wengine wako radhi kuua,kusema uongo,kuzusha ili tu kuhadaa wananchi.
Watanzania wanachotaka sasa hivi ni vitendo na siyo matamko,ngonjera. Hakuna kitu kibaya kama kuwa na njaa ya kwenye ubongo.