TUJISAHIHISHE

jembepori

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
618
193
Mimi ni moja ya wapenzi na shabiki mkubwa sana wa Rais wetu Dr Jp Magufuli..... yan namkubali sana na ndiyo maana kwenye uchaguzi nikaanzisha uzi hapa wa Team Magufuli na nikawa napambana sana na ndugu jamaa na marafiki nikiwashawishi wamchague ingawa wengi walikuwa hawamwamini na hatimae hawakumpigia kura ila mimi nilidiriki kuamka asubuh sana kwenda shule ya msingi kinondoni na kumpa kura rais wangu ninayemwamini sana tangu moyoni kuwa anauwezo mkubwa na utashi mkubwa wa kuivusha Tanzania kwaa dhat kabisa kuwaisaidia hasa walio wanyonge.

Changamoto.
Kwa hili la kulipia daraja mimi binafsi naliunga mkono tena sana maana nchi nyingi tu zinafanya hivyo na inawezekana....lakini nilikuwa namuomba rais wangu kuwa awaruhusu hawa ndugu zetu wenye BAISKELI nao wapite bure bila kulipa maana wengiwao ni wanyonge tu wa nchi hii.......wanahatarisha maishayao kwa kuendesha baiskeli mjini humu ili kupunguza kutumia NAULI za madaladala hivyo kwa kuwasaidia wapite bure pale darajani itakuwa ni kuwaongezea tija ya maisha yao ya kilasiku.....

Ni maoni binafsi na ningependa ieleweke hivyo..

Mungu ibariki Tanzania.....Mungu mbariki JPM
 
Back
Top Bottom