Lekachonka
Member
- Dec 17, 2016
- 35
- 17
Heri iwe nanyi nyote.
Moja wapo ya habari iliyotawala vichwa vya habari kutoka kwenye magazeti na mitandao mbalimbali katika Taifa letu ni suala la NJAA. Tumeshuhudia kauli tofauti kutoka kwa viongozi wetu wenye dhamana na wale wasiyo na dhamana. Suala hili likaweza kumwibua Kiranja mkuu wa serikali,kwa kauli moja akaweza kuonyesha sura kamili ya tatizo hili. Kweli Taifa linakabaliwa na NJAA. Yawezekana isiwe sasa lkn huo ndiyo ukweli.
Kwanini Tujisahihishe? Kina suala ambalo limeanza kujengeka miongoni mwa viongozi wetu hasa hawa wateule. Wamekuwa watu wa kupinga kila wanalokosolewa hata kama ni jema. Sikuona mantiki pale waziri mwenye dhamana alipojitokeza na kupinga tena kwa kujiamini kuwa hali ya Nchi ni nzuri hasa katika suala la Chakula. Haikuchukua muda tukasikia Mara wameomba Chakula, bado tukitafakari tukasikia Kwimba nao wana Njaa, kagera huko ndo usiseme...mambo kama haya hayahitaji siasa.
Zipo sababu nyingi tu na zenye mashiko kama angejitokeza na kusema kwanini tunaweza kukabiliwa na balaa hili la Njaa. Sote tunajua hali ya hewa ya Nchi yetu, mabadiliko ya Tabia ya Nchi, hali ya Uchumi wa Nchi yetu kwa sasa, na sababu nyingi kadha wa kadha.
Kipi kifanyike? Lazima tukubaliane kuwa kuna mambo ya Kitaifa na mambo binafsi. Ni aibu kwa Tanzania kusikika kwenye vyombo vya habari viwe vya ndani ama vya nje kuwa tunakabiliwa ama kuna maeneo yanakabiliwa na Njaa. Nimedokeza kwenye kichwa cha habari kuwa suala hili halikuanza awamu hii. Ni suala ambalo lina historia ndefu katika Taifa letu. Ni vyema tubadilike! Kwanza kabisa namna tunavyoendesha kilimo chetu.
Wananchi wengi kwa sasa wamekimbilia kwenye kilimo cha mazao ya biashara zaidi badala ya kilimo cha mazao ya chakula. Hili si baya..lkn wanahitaji waelimishwe zaidi.
Tunatakiwa tusiendelee kutegemea mvua tu katika kulima, watu waelekezwe kilimo cha Umwagiliaji. Wananchi waelekezwe namna ya kulima kilimo bora na si bora kilimo.
Serikali ifanye juhudi ya kusambaza mbolea kwa wakulima wetu. Asilimia kubwa ya wakulima wetu bado wanaamini kuandaa mashamba kwa kuchoma nyasi tu kabla ya kulima badala ya kutumia mbolea.
Lkn vilevile,ni vyema kwa wilaya na mkoa kuwa na eneo ama ekeri kadhaa kwa ajili ya kilimo. Wanaweza tumia wafungwa wetu walioko magerezani kufanikisha hili.
Serikali iiangalie mikoa ile ya kijani kama vile Mbeya,Morogoro,nk kwa jicho la Tofauti. Maana kama tunaamini kuwa ndiyo mikoa inayotulisha kwa asilimia kubwa basi kipaumbele kiwekwe hasa kwa kutenga bajeti toshelezi katika mikoa hiyo kwenye sekta ya kilimo.
Ushauri. Ni vyema viongozi wetu wakawa wasikivu na washaurike katika mambo nyeti kama haya. Haimaanishi kuwa kukubaliana na maoni ya mpinzani ama mtu usiyempenda basi ni kujivua nguo..la hasha!
Nchi hii ni yetu sote...tuache siasa hata katika suala la UHAI WA WATU WETU