Tujipongeze kuona CCM inarudi kwa wenye chama, Tunashukuru Mungu kuiongoza CHADEMA irudi kwa wananchi

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Ni jambo jembo na jambo la wakati pale unaposikia viongozi wa CCM wakijipongeza na kusherekea CcM kurudi Kwa wenyewe( Kwa maneno mengine CCM Ina wenyewe). Ni jambo la msingi sana na utokea pale ambapo chama ukua na kumiliki dola Kisha kuishi na kuendelea kujiimarisha Kwenye dola. Ni vigumu Kwa chama kilichofikia kuwa mikononi Kwa KUNDI la WATU kuwekeza muda na rasilimali Kwa wananchi.

Rasilimali nyingi uwekezwa Kwenye dola kwa sababu wenye chama mara nyingi uamini kwamba wananchi ni liability wakati dola ni asset. Chama kilichopo mikononi Kwa wenye chama hakitaki UCHAGUZI, hakina demokrasia inayoonekana na mfumo wake wakutawala hautegemea Sheria na kanuni Bali utegemea utashi wa mtawala.

Wakati CCM ikirudi Kwa wenye chama, CHADEMA kinaondoka Kwa wenye chama na kuelekea kumilikiwa Kwa Kasi na wananchi. Usajili wa wananchi unaoendelea Tena kw WATU kulipia ni ishara kwamba wenye chama wamekosa tegemeo na kubaki na ñguvu ya umma. Kwa chadema ya Sasa dola ni liability wakati wananchi ni Asset.

Kwao wao demokrasia ni mtaji na siyo igizo. Maskini wanajiunga na kushika nafasi na vipaji vinaibuliwa. Ni kwa msingi huo basi, utabaini usajili unaofanywa na chadema unalipa na hivyo kupelekea CCM Kwa kutumia wanaoitwa wenyewe kushawishi Wana chadema mahiri wajiunge nao na kuwapa ajira.

Njia hii ya kutoa ajira imezidi kuwapa hari vijana na wazee kuwa na bidii waonekane na kwenda kukalia viti vya akina ESTER huko CCM. In long run wananchi watashinda dola, wananchi watatumia nguvu Yao kutawala jukwaa. Tuzidi kuomba Mwenyenzi Mungu atuvushe salama Kwenye mbadilishano wa madaraka Kati ya wananchi na WENYEWE.
 
Back
Top Bottom