Tujipime

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,602
5,569
KATIKA SAFARI YA MAGEUZI:

Tumetoka wapi? tuko wapi? Na tunaelekea wapi?

Naomba kuwakumbusha wanaJF, na katika haya yafuatayo ndipo...


..... Ilibidi tume iundwe haraka na na ifanye kazi muhimu ya kutengeneza upinzani kutoka ndani ya Chama na Serikali kwa wakati huo, hivyo basi CCM, iliyakubali mapendekezo ya tume ya Jaji Nyalali. Ingawa baadhi walikubaliana na utafiti wa tume, Rais Mwinyi alinukuliwa katika vyombo vya habari vya ndani akipinga maamuzi ya “demokrasia ya vyama vingi kuwa kwa mfumo huo bado na ni haraka mno.” Hata hivyo, Mwl.Nyerere, ambaye
alijiuzulu wadhifa wa urais mnamo mwaka 1985, huku akibaki kuwa Mwenyekiti wa CCM. Kilifanyika kikao cha Halmashauri kuu chini ya Uenyekiti wake na bila kupingwa waliyakubali mapendekezo ya Tume ya Jaji Nyalali. Katiba ikafanyiwa marekebisho mwaka 1992 Februari, vyama vikaruhusiwa.


Haya kwa Tanzania yalifanyika kinyume na mabadiliko hayo katika nchi jirani ya Kenya, ambapo, hata hivyo, marekebisho ya katiba kuruhusu vyama vingi yalichukuliwa kutokana na shinikizo toka kwa wafadhili wa Nchi za Magharibi na mashirika ya fedha ya kimataifa hususan Benki ya Dunia.

Hivyo basi kwa sababu wakati wa uanzishwaji vyama hivyo, kulipatikana makundi mengi sana kuanzisha utitiri wa vyama kwa sababu ruzuki ilikuwa ikitoka serkali kuu moja kwa moja.


Inaendelea...
 
Kwa sababu hiyo vyama vingi vilishindwa kujiendesha kisayansi (kwani vilikuwa kama vile vya ushirika) watu hawakuwa na miundo mbinu ya kuvifanya vyama vijiendeshe kiuchumi. (Ndio maana mpaka leo hii vyama hivyo vikipewa fedha na wasio wanachama wao hawajiulizi wanaona ni uzalendo.) Hapakuwepo uzoefu wa kuendesha siasa za upinzani na mikakati endelevu kwa vyama vingi bali kila mtu alikuja na hoja zake kwa mfano palikuja misemo wakati huo MA-gaba-chori watu waliandamana yakaisha, pakaja mzee wa NJI HII wananji wakambeba mambo yakaisha! Pakaja Ngunguri Virungu vikatembea yakaisha! Juzi tumejionea wenyewe, YAMEPITA YAMEISHA. Watanzania tunasonga mbele. Ikumbukwe kuwa kwa sababu hatukuwa na historia ya siasa ya vyama vingi nchini, hakukuwa na uzoefu wa kuendesha siasa za aina katika Tanzania, lakini ikumbukwe ya kwamba viongozi na wafanyakazi waaminifu kwa serikali wengi wao ndio waliokwenda kuanzisha vyama hivyo. Kitu kingine ulikuwapo uadui ulioanza kuchomoza baina ya wasomi na watu wa kawaida ndani ya uongozi wa CCM hili nalo lilikuwa donda na ndio ikawa fungua mlango kwa wanaotaka kutoka na kutoa kiwingu ndani ya Serikali.... najiuliza mpaka leo Mh. 6 na wale wenzake mbona hawakutoka maana hawakuwa wenzao!! (KUWA MWENZAO ILIKUWA NI KUKUBALIANA NA MAWAZO YAO HATA KAMA NI YA OVYO!) samahani kwa hilo neno hapo nimelinukuu kwa....,

Na hali hivyo iliendelea wakati wa uteuzi wa majina ya Wabunge kwa mwaka 1995, na wale waliopigwa panga, wakahamia upinzani, na imeendelea kuwa namna hiyo mpaka leo. Wakishakosa ugali wao kule, wanaondoka kwa ghadhabu, na wakija huku wanaonekana mashujaa, kwanini basi hawakutoka mapema kabla ya kusigana? :A S angry: Kulikuwa na uzuri gani wakiwamo?:A S angry: Kwani nani asiyeujua ubinafsi na ubaya wa CCM toka awali?:tape:

Wote waliokuwamo kisha wakatoka binafsi yangu nina mashaka nao sana, kwani yaliyotokea kwa Amani Walid Kaburu sitoshangaa yakirejea tena na tena... maana MTU KWAO.

Nimewasilisha.
 
Jamani hii thread ni ya mwaka 2010 au nimeona vibaya?
Ni kweli ukionacho Mkuu. Tunajikumbusha tulikotoka ili tujipime... kwanini vyama vyetu vya upinzani havijimudu na kuwa imara zaidi ya miaka 10? Turejee historia...
NCCR 1995 TLP 2000 CUF 2005 CDM 2010-2015 Kwanini hutokea mvurugano na kudhoofisha vyama vyetu je tatizo ni nini? Je nini kifanyike ili makosa yanayojitokeza yasirudiwe?
Ukikumbuka ya Tanga, ukayaona ya Buguruni, unajiuliza hiki kinachoendelea Kinondoni ni nini?
Kwenye ukweli hatubembelezani kama tuna majipu tuyatumbue...
Umoja ndio silaha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom