Tujipe likizo ya siku 3 mfululizo, tu ‘Concentrate’ kwenye hili ya ajira kwa vijana

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
1572269523893.png
Wakuu, naomba niwashawishi kwamba hebu tujipeni likizo ya kama siku 3 hivi, tuahirishe mijadala ya kupinga au kusifu; tutulize akili kwenye kufikiri ni kwa namna gani tunaweza kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Hata kama kwenye hii mada utakuwa unapata hamu ya kulaumu mtu mwingine, hebu jizuie kwanza halafu baada ya kupata picha halisi tuendelee na zile timu zetu.

Suala la ukosefu wa ajira kwa vijana ni swala tete sana na linaendelea kukuwa siku hadi siku na mwisho wake itakuwa ni balaa.

Mwanzoni hoja ilikuwa kuwa vijana hawapati ajira maana hawajasoma. Sasa hivi wengi wamesoma, kuna hoja kuwa hawaajiriki maana hawana maarifa ‘Skills’ jambo ambalo ni kweli. Lakini hayo yote madogo, kubwa ni kwamba nafasi za kazi ni chache kuliko idadi ya wahitimu, kwa hiyo hata hao wahitimu wawe competent kiasi gani, hawawezi kupata nafasi za kuajiriwa kwenye ajira rasmi.

Sasa kuna hoja kwamba vijana wanaosoma kwenye vyuo mbalimbali wafikirie kujiajiri wakimaliza badala ya kuajiriwa lakini kuna masuala matatu yanajitokeza. Kwanza, elimu wanazosoma vyuoni ni ‘Academics’ ambazo hazifanyi kazi mtaani. Mfano mtu ana shahada ya Historia ambapo amejikita kwenye masomo ya jinsi ‘Wazungu walivyotunyonya’.

Cngangamoto ya pili, ni wahitimu kutokuwa na maarifa ya biashara na maisha ‘ Business and life skills’ Kwa hiyo wanapoambiwa wajiajiri wanakuwa hawaoni pakuanzia. Na

Tatu, wahitimu hao wanakuwa hawana mitaji. Fikiria kama watu walioajiriwa miaka na miaka hawana mitaji na hivyo hawana mradi wowote, vipi mhitimu toka chuo aliyesomeshwa kwa mkopo?

Sasa nini cha kufanya?

Ushauri huu wa cha kufanya ni kama kuchokoza mjadala tu, lakini naamini wadau wataongezea ushauri wa msingi ili wazo likae vizuri na liwasaidie wenye uhitaji.

Tunaweza kushauri kuwa badala ya wanafunzi wengi kupewa mikopo kisha wasome ‘Degree’ baada ya hapo hawazifanyii kazi, ajira hawapati, kujiajiri hawawezi, mikopo hawawezi kurudisha na kujitegemea hawawezi; mikopo hiyo igawanywe mafungu mawili.

Fungu moja wakopeshwe vijana kadhaa ambao wana ‘strong commitment’ na ‘academics’ na fungu jingine wakopeshwe vijana ambao wako ‘committed’ na biashara, uzalishaji na ujasiriamali.

kwa kufanya hivi tutakuwa hatujaweka mayai yote kwa kapu moja. Tutakuwa tumefanya ‘diversification’ na kutengeneza mazingira ya mambo kwenda vizuri zaidi.

Kwa kufanya hivyo, kama nchi tutakuwa tunajenga mazingira ya watu kutawanyika kwenye shughuli za kiuchumi na hivyo kuchochea uchumi kukua, tutakuwa tumepunguza changamoto ya ukosefu wa ajira, tutakuwa tumeongeza uzalishaji na hivyo kuchochea kuongezeka kwa pato la taifa na kuweka mazingira ambayo angalau wahusika wataweza kulipa mikopo na kuweza kujitegemea kiuchumi.

Ndugu yangu nakuomba sana usaidie kufikisha wazo hili kwa wahusika na waone kama inafaa kuliboresha na kulifanyia kazi kwani litakuwa ni jambo jema kwa Watanzania wote.Nakushukuru sana .

kutokana na kusoma trend mbali mbali, sasa naweza kutoa hoja kwamba; ukosefu Wa ajira kwa vijana huenda likawa janga kubwa zaidi nchini, kuliko majanga mengine katika miaka michache tu ijayo.

Ikumbukwe kila mmoja wetu anahitaji kuishi maisha ya heshima na kuweza kujitegemea. Ni jambo gani la kizalendo zaidi ya hili ambalo tutakuwa tumelifanya kama tukifanikisha baadhi ya wenzetu wenye uhitaji wakaweza kuishi maisha yenye heshima na mafanikio?

Inawezekana wewe jambo hili lisiwe linakugusa moja kwa moja, ila ungetaka kulielewa vizuri, jiweke kwenye nafasi ya muhanga halafu fikiria sulubu ambayo ingekuwa inakukabili.

Uzuri wa jambo wazo hili, ni ‘Win Win’ hakuna atakayepoteza na wala hailazimiki kuwekeza fedha nyingi zaidi ambazo pengone hazipo.

Ni muhimu wadau wakaliboresha zaidi wazo hili ili kama likionekana linafaa, linaweza kuwasaidia wengi.
 
Kwanini kusiwe na shift ya wafanya kazi katika idara mbalimbali,
mfano kwawalimu:
Mwl. afundishe siku kumi tano then anaangia mwingine kumalizia mwezi...
Pia hata mshara ugawanywe vivyo hivyo kwa nusu mwezi
Hii itafanya mtu kuwekeza nje ya ajira kwasiku anazokua nje ya shift ya kazi...
 
wazo langu

mbunge yeyote aliyee dumu vipindi vi 2 tayar amepata mtaji wake awapishe wengine

mfanyakazi ws umma aliyedumu miaka 20+ aachie ngazi tayari kashapata mtaji wake

ubunge, udiwani angalau mwenye cheti cha diploma, na kuendelea

wenye cert,dipl. huwa wakiongoza vitengo wapewe muda 4yrs wakasome kupata sifa stahili tofauti na hapo waachie ngazi

fm 4 waliopata matokeo yasiyo ridhisha waandaliwe utaratibu wa kwenda veta

yarudishwe mashamba ya jumuiya/kijiji vijana tukalime kwa nguvu kitakacho patikana kiwe mtaji wa kuanzia kwa baadhi yao/yetu

vijengwe viwanda vidogo (achana na porojo za mwaijage vyerehani vi 4 ni kiwanda) ili kuweza kubangua mazao kiasi kabla ya kusafirisha.

wizara ya kilimo iendeshe warsha na makongamano kuhimiza ulimaji wa mazao kama maua, karoti, mbogamboga na ihakishe ina simama kati kama dalali wa masoko wa mazao hayo.
 
Nawaangaliaga wana mtaani kwangu nasikitika tu,

wana miaka mitatu mpaka minne hawana ajira na wapo tu home wanasubiria ugali,

Sina cha kulaumu wao au mfumo wa wa elimu

Tatizo ni kama nchi hatuna muelekeo

Nchi hatuna plan na watu wake

Nchi ya shamba la bibi

kinachotakiwa ni reform ya elimu tu

watu wafundishwe uzalishaji zaidi kuliko uongozi

hizo unazozita degree wengi waqnaandaliwa kuwa katika managerial posts,

tungekuwa na vyuo vya veta kila wilaya watu wafundishwe ufundi
 
Ki ukweli suala la ukosefu wa ajira kwa vijana ni wimbo wa taifa kwa sasa. Vijana wengi waliojiajiri wanapitia changamoto mbalimbali na waliofikia kilele cha mafanikio ni wachache kati ya wengi waliothubutu.

Nirudi kwenye mada. Nini kifanyike?

Kwa mtazamo wangu serikali imeshafanya juhudi mbalimbali katika kuhakikisha vijana wanawezeshwa. Mfano Kuna utaratibu wa ugawaji mikopo na uwezeshwaji wa vijana kupitia mifuko mbalimbali. Kwa leo nizungumzie mfuko wa halmashauri za miji na vijiji katika wilaya.

Mikopo ya halmashauri inatolewa kwa makundi ya wakina mama na vijana kupitia tena bila riba. Kuna mikopo ya kiasi taslimu cha fedha na mikopo ya vifaa na nyenzo za uzalishaji mali. Utaratibu wa mikopo hii unatolewa kwenye ofisi za kata na mitaa.

Binafsi naifahamu vizuri sana mikopo hii na haina ugumu kwenye upatikanaji wake. Viwango mbalimbali vinatolewa kulingana na mchanganuo wa matumizi ya mikopo.

TATIZO

Tatizo kubwa katika mikopo hii ni kila mara kuja na mahitaji tofauti. Mwaka jana kikundi cha vijana watano (18-35) waliruhusiwa kupata mkopo ila sasa ni kuanzia vijana kumi. Navyojua mimi sio rahisi kwa kikundi cha vijana 10 kufanya mradi wa pamoja.

SULUHISHO

Nafikiri mikopo hii ya halmashauri ingetanua wigo(wasijikite mitaani tu) na badala yake maafisa mikopo wazunguke mavyuoni na kutoa elimu ya mikopo hii kwa wanachuo ili kama wanafikiria kufanya mradi ama kutokana na taaluma yao au ujasiriamali waweze kuwapatia (hasa wanaomaliza chuo) na wenye uthubutu wa kujiajiri.

NB: Kama mwanafunzi anakopeshwa milioni 10 kusomeshwa kwa nini asikopeshwe ili ajiajiri?
 
Back
Top Bottom