Tujipange kimatumizi na kutafuta vyanzo vya mapato kwa mwezi huu wa Desemba ili tuepuke kukwazana kuanzia January 2020

Asbm

Member
Jun 26, 2019
38
33
Ndugu WanaJf, Heshima kwenu

Tunapoelekea kufunga mwaka, kuna matukio mengi mbele yake yote yakihitaji fedha nyingi kuyafanikisha.

Kwa mfano tu, kuna sikukuu kubwa ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mtoto Yesu Kristo (25 Dec-Christmass), Boxing day, na kuukaribisha mwaka mpya. Lakini isitoshe kwa wazazi wana watoto wanaotakiwa kuwapeleka shule hivo ada zahtajika. Kuna wapangaji ambao tunatakiwa kulipia kodi za nyumba kwa wenyenyumba.

Yawezekana muda ukawa hautoshi kama hukujipanga mapema kwa mwaka mzima kufanikisha hilo na kuishia kusumbua ndugu, jamaa na marafiki ili wakuazime fedha kufanikisha mahitaji yako.

Ni kipindi ambacho kila mmoja anakuwa na matumizi makubwa hivo unapoomba mahitaji yako kwa mtu na akashindwa kukusaidia usichukie.

Nakumbushia tu ili tusije kuishia kukwazana na kuchukiana eti kwa sababu tu tumeshindwa kusaidiana. Ni muda mzuri wa kujipanga tunapoelekea mwishoni mwa mwaka ili mwakani tuwe na vyanzo vya mapato vitakavyosaidia kukidhi mahtaji yetu kwa miaka ya mbeleni inayokuja.

Ahsanteni
 
Back
Top Bottom