Tujikumbushe ya Joseph Ludovick usiku alio tekwa KIBANDA

Dec 11, 2010
3,321
6,328
WanaJF.

Tujikumbukishe maandiko ya Joseph Ludovick masaa machache baadaa ya kushambuliwa na kuumizwa kwa Absalom Kibanda.

"Ndugu,leo usiku yapata saa tano na nusu niliachana na Maggid Mjengwa maeneo ya Shekilango tukitokea Rose Garden.yeye alielekea hotelini. alikofikia,sehemu fulani kariakoo,nami nikasubiri kigari kuelekea nyumbani kwangu.hapo shekilango,magari yalichelewa kidogo,pembeni ilipaki bajaji ikiwa na watu 2 na dereva.ndipo wakaniambia twende tuchangie mia tano tu kwenda ubungo mataa nikakaa katikati ya hao jamaa.

Ghafla wakakata kona na kuanza kuelekea mabibo na wakiulizana kama wako kamili,na mwingine kujibu yuko kamili.nikajua tayari niko mikononi mwa majambazi na sikujua wako kamili namna gani,kwa hiyo nikaamua kuwa mtulivu.Tulipofika relini karibu na mabibo,wakanipokonya begi lakini hawakulifungua.( ndani yake kulikuwa na laptop,toshiba kubwa,na chaja yake,kamera ndogo ya digital na USB yake,modem ya zantel na card reader.).tulipofika maeneo ya loyola sekondari nikawasihi wanishushe ili nirudi mwenyewe,wakaniambia safari ile inaishia jangwani.nikaingiwa na wasiwasi mkubwa na nia yao hasa.maana wameshanipokonya begi,kwa nini wasiniachie? lakini niliendelea kuwa mtulivu ili kutowa provoke.

Tulipovuka kigogo mwisho kwenye giza karibu na msikiti,wakasimama pembeni ya barabara na kuniamuru kushuka.nikashuka na kuanza kuwadai begi langu.ndipo mmoja akasema wamekuwa wastaarabu mimi naanza kuwadharau.Ghafla akanivuta kwa nguvu kunirudisha kwenye kibajaji,akamwambia mwenziye wanisachi kama nina vitu vingine.wakanisachi na kuchukua pesa (nilikuwa na elfu 35) na simu mbili ndogo za nokia.moja yenye line mbili.kisha mmoja akatoa order- nivuliwe nguo.Nikavuliwa viatu,T shirt na suruali.nikabaki na nguo za ndani pekee.wakanishusha na kuniacha hapo.

Kurudi nyuma kama hatua kumi tu ndipo kituo kidogo cha polisi Kigogo.nikaanza kutoa maelezo hapo kwa zaidi kama ya saa 2 nikiwa uchi na nguo za ndani tu.Nikiwa hapo nikasikia polisi wakiwasiliana juu ya tikio la kupigwa vibaya ABSALOM KIBANDA kwenye redio calls.ilikuwa yapata saa nane.baada ya kuchukuliwa maelezo,polisi walinipatia gari nikaelekea hotelini kwa Maggid,ambaye saa kumi aliamshwa na kunichukulia chumba hapa nikapumzika.

Ameniazima nguo zake ndizo nimevaa bado hadi sasa.naelekea kituo cha polisi Magomeni kwenda kupewa mpelelezi wa kesi yangu.namba ya case yangu kigogo ni KIG/RB/318/2013 (WIZI KUTOKA MAUNGONI).

Namshukuru Mungu hawajanijeruhi wala kunipiga.namshukuru Maggid kwa msaada wake hadi sasa

MUNGU NI MWEMA".
Maandishi haya aliyaandika kwenye jukwaa la mabadiliko.

Akaja Manyerere hapa JF na huu uzi: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...u-siri-za-kutekwa-kibanda-hazitajulikana.html
 
Amefanyiwa unyama huo hatua kumi kutoka kituo cha polisi?ama kweli njia ya mwongo ni fupi!
 
Waliomtuma walikuwa wanachukua zile recording original,ili kikinuka asije kuwageuka,na sasa wamemtelekeza kama ile mifuko ya lailon ambayo hutumika sirini,na bado akina Juliana na wasaliti wenzake,wakisha watumia ni kutupa tu,hayo ndiyo maCCm.
 
Waliomtuma walikuwa wanachukua zile recording original,ili kikinuka asije kuwageuka,na sasa wamemtelekeza kama ile mifuko ya lailon ambayo hutumika sirini,na bado akina Juliana na wasaliti wenzake,wakisha watumia ni kutupa tu,hayo ndiyo maCCm.

Hiyo ndio hasara ya kutumika mkuu. Ila amini Mungu haya yana mwisho na mwisho wake hauko mbali.
 
Hiyo ndio hasara ya kutumika mkuu. Ila amini Mungu haya yana mwisho na mwisho wake hauko mbali.

Wamesahau kuwa ukitumika kuua na wewe itabidi ufe,ili waliokutuma wabaki salama,imekula kwake,alitegemea atapewa mamilioni kumbe 50,000/= ndiyo malipo yake na kutelekezwa.
 
CCM wameshindwa kumuwekea dhamana kibaraka wao wakati wana mali zisizohamishika kama jengo la vijana.
Huyu kijana hakujua gharama za kutenda yasiyompendeza Mungu, hata hakuwahi kusoma yale ya YUDA ISKARIOTI na vipande therathini vya fedha alivyopewa kumsaliti Bwana YESU. Hakuweza kuvitumia badala yake akajinyonga hata kabla aliyemsaliti kusulubishwa.
Kijana huyo ni MSHENZI SANA.
 
Hivi ni kwanini Mwigulu hamwekei dhamana mtu wake?

Amuwekee dhamana kwani jamaa anakaa sero?? Mchizi anaishi HOTELINI huyo anakula maisha kuliko sisi tusio na ''kesi''.

Cha kujiuliza ni kama watamlipa hizo milioni 300 walizomuahidi maana ishu ya Ugaidi imebuma vibaya na wananchi tunajua kuwa ilitengenezwa na Mwigulu Nchemba
 
aisee hivi alikuwa anaandika hayo kwa kujishtukia ili asishtukiwe,jamaa kwa kweli ameiweka familia yake kwenye wakati mgumu only beacause of money,too sad,yaani alivyomsaliti Lwakatale kwa kumrekodi hapo ndo alichemsha kweli,just imagine Lwakatale ndo alikuwa kama mzazi kwenye harusi ya Ludo,Ludo alichemsha kweli,hapo alipo anajuta kweli.Hivi kweli hakufikiria matokeo ya mchezo ambao ameejiingiza?
 
aisee hivi alikuwa anaandika hayo kwa kujishtukia ili asishtukiwe,jamaa kwa kweli ameiweka familia yake kwenye wakati mgumu only beacause of money,too sad,yaani alivyomsaliti Lwakatale kwa kumrekodi hapo ndo alichemsha kweli,just imagine Lwakatale ndo alikuwa kama mzazi kwenye harusi ya Ludo,Ludo alichemsha kweli,hapo alipo anajuta kweli.Hivi kweli hakufikiria matokeo ya mchezo ambao ameejiingiza?

Huyu dogo, Lwakatare ni kama baba yake, kama amempa mke na sasa anaishi kama mwanaume and then unamsaliti huyo mtu, laana hakika itamwandama maisha yake yote, labda tu aende kwenye familia ya Lwakatare ajieleze na kutubu wamsamehe au wasimsamehe lakini awe ametubu labda anaweza kupata amani vinginevyo sioni.
Sometimes kumbe mtu akiwa na njaa hata shule hamsaidi kufikiri outcomes ya matendo yake.
 
Hauhitaji kuwa na PHD au hata degree kumjua mhusika mmojawapo wa tukio la Kibaanda ni Ludo akishirikiana na mfadhiri wake wa karibu mwiugulu
Waje FBI au hata Scotland Yard kama watu na hata nchi haijaumbuka!
 
CDM wametega MCC vibaya...kutoa hawawezi kwani dili litaharibika zaidi ....kumwacha ni noma..Watabaki mpa special attendance tuu.ila atakula kifungo, gerazani aua hotelini.
 
Don't just connect the dots! Collect and critically analyse them. You will smell something fishy and see the other side of the story.

Saafi sana...hembu waeleze.Kuwa si tuu wafikrii mara mbili ila ziaid ya mara mbili.....hawajui kuwa clue ya vitu vya mashaka hutumika kujenga hoja ya kufanya upelelezi na kujua wapi pwa kuanzia.Kwa wasio observant hawatoona vitu vingi sana.
 
CHADEMA msaidieni kijana wenu huyo bodyguard wa SLAA mahabusu mahala pabaya sana kule!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom