Bath Kombwa hajafariki siku nyingi kweli?Kuna mtu anafahamu habari za Barholomew Kombwa?
Take a break, na tujikumbushe enzi zile za RTD, ambapo kulikuwa hakuna FMs rado kama sasa. Hakika kulikuwa na watangazaji, vipindi bomba na hata nyimbo za kutambulisha vipindi zilikuwa makini sana. Hebu ngoja niwakumbushe baadhi ya watangazaji wa wakati huo.
1. Nassoro Nsekeli- alikuwa na sauti kama ya mafua hivi alikuwa mtaalamu wa kipindi cha Majira- ndiye aliyetangaza kifo cha Nico Zengekala
2. Bujago Izengo wa Kadago- Kibesi chake kilikuwa safi sana
3. David Wakati (DG) - kipindi cha Nipe habari- Kwaherini wote, mungu awalinde na mmbaki salama, mungu akipenda..............
4, Khalid Ponera- Zilipendwa
5. Ahmed Kipozi- taarifa ya habari
6. Hassan Mkumba- matangazo ya vifo
7. Siwatu Luwanda
8. Salama Mfamao
9. Mohamed Amani (Mohamed Dahman)
10. Salim Seif Nkamba
12. CHisunga Steven- kipindi cha Ugua pole duu
13. Bathoromeo KOmbwa (bati Kombwa) - WAkati wa Kazi
14. Ahmed Jongo- Mpira
15. Christina Chokunogela
16. Dominic Chilambo- Mpira
17. Edda Sanga
18. Debora Mwenda- Mama na Mwana
19. Aloycea Maneno- Ombi lako, cheichei Shangazi, mama na mwana
Duu nawamiss sana hawa watu tofauti na watangazaji wa sasa
MarehemuRankim Ramadhani: buzuki time
Kitambo sana.
R.I.P hatuko naye duniani alitutoka mwaka juzi nadhaninamkumbuka Ezekiel Malongo wa redio tanzania enzi hizo akiwa mtangazaji wa mpira daaah...
sijui yupo wapi
Sent using Jamii Forums mobile app
jmn..kumbe hatunae huyu dada?Halima mchuka(First lady)RTD akitangaza mpira RIP.