Tujikumbushe walioishi siku 72 kwa kula maiti baada ya ajali ya ndege

Una maana huyo Mama wa Ethiopia?
Wakati wa vita ya wao kwa wao wengi wao walibahatika kuikimbia vita ingawa wengi walikufa kwa njaa
Ila huyu mama alisikitisha sana maana alikuwa dhaifu sana na alikuwa na kichanga na mtoto alikuwa dhaifu sana kwa kutokupata chochote kwa mda mrefu
Mama hakuwa na maziwa kifuani kwa udhaifu aliokuwa nao
Alipoona mtoto anakaribia kufa kwa njaa akawa anamtemea mate yake ili apompoze njaa mtoto wake
Jamani vita muisikie tu kwani Ina mateso ya kila aina
Mama ashukuriwe kwa kila namna na tuwajali sana hatujui wamepitia mangapi


Sent from my iPhone using Tapatalk
Uwiiiiii uwiiiiiii 😭😭😭
 
Itabidi niiicheki. Ni nzuri kuitazama na demu mpya unaemtokea ili akihofu namkumbatia na kumpoza kwa mahaba.
 
Utakumbuka kisa cha ajali ya ndege iliyotokea mwaka 1972 iliyoanguka Amerika ya Kusini kwenye milima ya barafu ya Andes iliyo Argentina na Chile, kati ya abiria na waendeshaji 50 wakiwemo wachezaji wa mpira wa Rugby kutoka Uruguay walitoka hai abiria 16 tu ambao walipatikana siku ya 72 tangu kutokea kwa ajali hiyo katika umbali na ukubwa wa maelfu ya kilometa za milima ya barafu iliyoungana.

Kipindi ajali inatokea abiria waliotoka hai walikuwa 27 lakini baadaye wengine wachache kupoteza maisha kwa majeraha na baridi kali na wengine 08 zaidi walikufa kwa kufunikwa na maporomoko ya barafu Avalanches.

Siku zote waliishi kwenye mabaki ya ndege hiyo wakiamini wangepatikana na kuokolewa lakini haikuwa hivyo kwani siku chache baadae waliishiwa mabaki ya chakula na kuanza kukata nyama za maiti na kula wakianza na mwili wa rubani.

Wachache walikataa mwanzo lakini baadae hali ilizidi kuwa mbaya na kujiunga kula ili kuongeza siku za kuishi.

Baadae moja aliruhusu mwili wa ndugu yake ukatwe na kuliwa.

Baada ya kuingia mwezi wa pili wawili kati yao walijitoa muhanga kutoka kutembea mamia ya kilometa wakipanda na kushuka milima ya barafu kwa kubahatisha huku wakiwa wamepakia vipande vya nyama ya maiti ili wasife njaa.

Walitembea safari ya kifo mkononi kwa muda wa siku 08 hadi walipoona mto na kuufuata kwa bahati nzuri walikuta mtu akiwa na farasi ng'ambo ya mto huo na kuwasiliana nae kwa kuandika ujumbe kwenye karatasi na kufunguka kwenye jiwe kisha kumrushia.

Hapo ikawa sababu ya kupona kwao na kuokoa wengine waliobaki kwenye tukio baada ya kusambaa habari kuna wahanga wa ajali hiyo wamepatikana hai.

Wanasema sababu ilikuwa ni uzembe wa marubani kujaribu kukatisha 'shortcut' kwenye milima hiyo na kujikuta katika milima iliyochomoza kuliko usawa wa ndege ilipokuwa inapaa na kugonga.

Ni moja katika ajali mbaya iliyosababishwa na makosa ya kibinadamu.
Karatasi walitoa wapi walitumia peni gani pi na bard Kali karatasi lingeloa STORY NZURI ILA IMETUNGWA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni very emotional
Sikulia bali niliwasikitikia sana kwa madhila waliyoyapata. Kama ni matukio ya kweli kwa watu huwa Nina huruma sana ila kwa mimi yakinitokea huwa ninakubali matokeo na kusubiri what next kwa sababu nimeona mengi vitani. Angalia tu ndio unajifundisha hali halisi inayowatokea watu.

Kuna visa dunia hii. Yaani niliposoma comment nimemkumbuka mama mmoja Ethiopia wakati wa vita daa


Sent from my iPhone using Tapatalk
Ndugu ukisoma story vzuri unagundua ni ya kutungwa mfano walikuwa kwenye barafu je karatasi halikulowa? Pia walitumia Nini kuandika ujumbe? Jiulize kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu ukisoma story vzuri unagundua ni ya kutungwa mfano walikuwa kwenye barafu je karatasi halikulowa? Pia walitumia Nini kuandika ujumbe? Jiulize kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni true story inabidi uisome mwenyewe au kuangalia movie yake
Kwa Mimi naamini ni Kweli kwani mpaka waliopatwa na madhila hayo wapo mpaka leo
Kila mmoja wetu ana haki ya kukubali au kukataa
Sikupingi kwa utafiti wako


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Inaitwaje hiyo movie mkuu?
Daa naikumbuka hiyo ajali niliiona documentary yake na movie pia. Yaani walikula kila kitu mpaka pombe zote na mwisho wakaanza Kula mpaka dawa za mswaki, na mwisho kuanza kula nyama za wenzao.

Nakumbuka mmoja wa abiria alimwambia rafiki yake “niahidi nikifa hutakula nyama yangu”
Bahati mbaya mmoja wapo alifariki

Hiki kisa kilinisikitisha sana kuzidi hata vita ya pili ambapo majeshi ya Japan walipokuwa wanawala wenzao baada ya kukosa chakula



Sent from my iPhone using Tapatalk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni true story inabidi uisome mwenyewe au kuangalia movie yake
Kwa Mimi naamini ni Kweli kwani mpaka waliopatwa na madhila hayo wapo mpaka leo
Kila mmoja wetu ana haki ya kukubali au kukataa
Sikupingi kwa utafiti wako


Sent from my iPhone using Tapatalk
Nimejarb tu kufikilia kulikuwa na barafu why karatasi halikulowa? Pia kalamu ya kuandika walitoa wap

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimejarb tu kufikilia kulikuwa na barafu why karatasi halikulowa? Pia kalamu ya kuandika walitoa wap

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimejarb tu kufikilia kulikuwa na barafu why karatasi halikulowa? Pia kalamu ya kuandika walitoa wap

Sent using Jamii Forums mobile app

Waliopata majanga hayo ndio waliohadithia
Waliwaacha wenzao kutafuta msaada ndipo wakakutana na mto na upande wa pili wakaona watu
Anyway walivyosema ni kuwa waliandika kwenye karatasi na kuikunja kwenye jiwe na uzi halafu kumtupia mtu upande wa pili na ndio kuwataarifu police

Adjustments.jpg



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom