Tujikumbushe wahadhiri wababe na kauli zao za kukatisha tamaa

Domaradzka

Senior Member
Apr 19, 2016
135
168
Maisha ya raha tu hayawezi kumfunza mtu. Katika maisha lazima upitie kipindi kigumu walau cha kukupima uwezo wako wa kukabiliana na changamoto. Hata elimu iko katika mkondo huu, kuna wakati chuoni tulipitia magumu katika baadhi ya kozi hata kukata tamaa.

Lakini pia baadhi ya wahadhiri walifanya maisha haya yawe magumu kwa ubabe wao na kauli zao tata. Vijana wakiwa wanajiandaa kwenda vyuoni hebu tujikumbushe hao wahadhiri ambao walitufanya tuone maisha ni magumu.

I will never let my government down. Siwezi nikaruhusu kilaza avuke mwaka na kwenda kuua watanzania-Dr.Thomas Nyambo, Biochemistry MUHAS
 
Maisha ya raha tu hayawezi kumfunza mtu. Katika maisha lazima upitie kipindi kigumu walau cha kukupima uwezo wako wa kukabiliana na changamoto.Hata elimu iko katika mkondo huu, kuna wakati chuoni tulipitia magumu katika baadhi ya kozi hata kukata tamaa. Lakini pia baadhi ya wahadhiri walifanya maisha haya yawe magumu kwa ubabe wao na kauli zao tata. Hebu tujikumbushe hao wahadhiri ambao walitufanya tuone maisha ni magumu.

I will never let my government down. Siwezi nikaruhusu kilaza avuke mwaka na kwenda kuua watanzania-Dr.Thomas Nyambo, Biochemistry MUHAS
Mkuu kumbe una mpata Dr.Nyambo dah..siwezi msahau siku ya oral alivyonikazia.
 
Prof. Mgongo Fimbo na Ebenezer Mshana wa UDSM faculty of law. hao nikikutana nao hata mahakamani huwa nahakikisha nimewagalagaza hadi waonekane wao chekechea kwangu. wanajua walichonifanya, ila nimewasamehe. naona hata magufuli hajawaona hadi leo watastaafu hata mapande wanayopata wenzao wenyewe watasikia tu kwenye television. hadi yule dogo Dr. Longopa aliyefundishwa nao amepewa pande wenyewe wataendelea kusahihisha mitihani hadi wakongoroke.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom