Tujikumbushe vitabu vya zamani

duh...hivi vitabu bwana usipime....

wakati huo kipindi cha mama na mwana kilikuwa kinasimulia hadithi zake zikirushwa na RTD, mida ya saa nane, nakumbuka hadhithi chache kama ua jekundu, binti chura, akajasembamba, kina bibi aga, na kuna kitabu kingine kilikuwa kinaitwa 'adili na nduguze' mambo ya mji wa mawe n.k.....

kweli watoto wa siku hizi hawafaidi kabisa
 
alfu lela ulela elfu mia na moja
amina anakula wali kwa sindano
man umenirudisha,bali sana
Nimevisoma vyote hivyo. Vilikuwa vinanitia hamasa sana ya kusoma.Halafu kulikuwa na vipindi vya radio kujifunza Kiingereza, 'A Thousand Miles to Tanga'. Siku hiyo mwalimu akileta radio darasani ni furaha tupu!
 
Bulucheka na kabila la wagagagigigogo!

du! mkuu enzi za kaptula ya kaki na shati jeupe, ukivaa stocking na raba mtoni unaonekana bonge la mshua!
Ni WAGAGAGIGIKOKO, na vitabu "original "vya ALFU LELA U LELA vinapatikana , vimerudufiwa na Mkuki na Nyota na kimoja ni 8000, vipo namba moja mpaka namba saba,
 
Ama kweli nyinyi ni vijana wa zamani, kukumbuka vitabu vyote hivyo vya akina Bulicheka na mkewe Lizabeti, Bibi Tarabushi na Kalume Kenge alipokataa kwenda shule!

Ni kweli nilikutana na baadhi ya vitabu vya Alfu lela u lela pale mtaa wa Samora. Nilivinunua vol 1 mpaka 3 nitatafuta vyengine.

Munakumbuka hadithi ya chura aliyekuwa akisema "my name is Shokolokobangoshei" na binti hawezi kutamka neno hilo. Sikujua kumbe lile neno ni la Kisukuma?

Ooooooooh the good old days, leo ni siasa siasa siasa hata kwa watoto wadogo jamani dunia yetu inakwenda wapi?
 
Ama kweli nyinyi ni vijana wa zamani, kukumbuka vitabu vyote hivyo vya akina Bulicheka na mkewe Lizabeti, Bibi Tarabushi na Kalume Kenge alipokataa kwenda shule!

Ni kweli nilikutana na baadhi ya vitabu vya Alfu lela u lela pale mtaa wa Samora. Nilivinunua vol 1 mpaka 3 nitatafuta vyengine.

Munakumbuka hadithi ya chura aliyekuwa akisema "my name is Shokolokobangoshei" na binti hawezi kutamka neno hilo. Sikujua kumbe lile neno ni la Kisukuma?

Ooooooooh the good old days, leo ni siasa siasa siasa hata kwa watoto wadogo jamani dunia yetu inakwenda wapi?
Umenena kweli. Kwa mfano mimi nilianza darasa la kwanza mwaka 1962. Mpo?
 
duh...hivi vitabu bwana usipime....wakati huo kipindi cha mama na mwana kilikuwa kinasimulia hadithi zake zikirushwa na RTD, mida ya saa nane, nakumbuka hadhithi chache kama ua jekundu, binti chura, akajasembamba, kina bibi aga, na kuna kitabu kingine kilikuwa kinaitwa 'adili na nduguze' mambo ya mji wa mawe n.k.....kweli watoto wa siku hizi hawafaidi kabisa

Mnanitoa machozi. Watoto siku hizi hawafaidi Preta. Hawafaidi. Namwomba Mungu anipe nguvu, nina mpango wa kurudisha nguvu za Adili na Nduguze, baadaye after few years nitafanya kwa vitendo. Let's pray.
 
Ni WAGAGAGIGIKOKO, na vitabu "original "vya ALFU LELA U LELA vinapatikana , vimerudufiwa na Mkuki na Nyota na kimoja ni 8000, vipo namba moja mpaka namba saba,
Hao wanatafuta hela tu, vitabu vyenyewe haswa ni kuanzia namba 1-4.
 
Bulucheka na kabila la wagagagigigogo!

du! mkuu enzi za kaptula ya kaki na shati jeupe, ukivaa stocking na raba mtoni unaonekana bonge la mshua!

mkuu ni WAGAGAGIGIKOKO halafu na mfalme wao ni HUHIHUIHUI pia yupo mzee mmoja anitwa MZEE MIRAJI.
 
Msisahau kitabu cha safari za Allan Quterman akina Msolopagazi,kibibi Gagula,wajivuni,n.k :A S 39:

Awww hichi kitabu cha umslopogaas (sp) nilikisoma kikiwa kimeshararukararuka sana yaani enzii hizoo umenikumbusha mbali nyuki dume, nakumbuka nilikuwa nanunua willy gamba series na hela za tuition, plus vitabu vyooooote vya Shafii Adam, kosa la bwana Msa..what I won't give to relish reading them again! Oh time !
 
kweli kabisa those were the days nadhani mambo yalianza kwenda downhill baada ya vitabu kama kandanda kitandani kuanza kutungwa
 
wadau... nakumbuka sana kitabu kikiitwa KISA CHA HASSAN BASRI NA MUHAMMED SIHIRI, kulikuwako VISA VYA ABDULI, hakika ni vitabu vikimpa mtu uelewa wa mambo na kutanua FIKRA.:smile-big: Je vingaliko pia?
 
Hadithi za Allan Quatermain

X-Paster said:
Bwana Balozi wa Lamu:

Mtu huyo mrefu, ambaye hadithi zake nyingi zilisimuliwa katika nchi ya wazulu, na ambaye katika watu wake huitwa "Gogota," na "Mchinjaji" alishtuka, na shoka lake la vita lenye kipini kirefu lilikuwa karibu kumponyoka kwa mshangao na mara ile alinitambua akawa ananiamkia.

Mkuu, mkuu wa zamani, mkuu, mkuu! Baba! Makumazahn, mzee mwindaji, mwuaji wa tembo! mla simba, mwerevu! akeshaye! hodari! mwepesi! ambaye risasi zake kabisa hazikosi shabaha, apigaye shabaha ya kweli, rafiki mwaminifu. Mkuu! Baba! Ile methali ya kikwetu isemayo 'Milima haikutani lakini wanadamu ukutana,' ni ya kweli kabisa na yenye busara. Tazama! tarishi alikuja toka Natal, akalia, 'Makumazahn amefariki! Nchi haitamwona Makumazahn tena.' Haya yalitokea zamani sana. Na sasa, tazama hapa katika nchi ngeni ya harufu mbaya namwona tena Makumazahn, rafiki yangu. Ndiye bila shaka. Manyoya ya mzee bweha yameingia mvi; lakini macho yake na meno yake ni makali kama zamani. Ha! Ha! Makumazahn, unakumbuka namna ulivyoipeleka risasi katika jicho nyati aliyekuwa akishambulia... unakumbuka..."

Basi, nilikuwa nirnemwacha aendelee hivyo, kwa sababu niliona ya kuwa wale Wakazi watano walionekana kwamba wanaweza kufahamu maneno mengine katika yale aliyoyasema, tena yanawatia fikira; lakini sasa niliona inafaa kumkomesha, maana hakuna kitu kinachonichukiza kuliko desturi ile ya Wazulu iitwayo kubonga, yaani kusifu kupita kiasi. Nikasema, "Nyamaza! Ala, maneno yako yenye kelele yamezibwa tokea tulipoachana, na hii ndiyo sababu yanabubujika na kutugharikisha hivi? Unafanya nini hapa pamoja na watu hawa, wewe ambaye tulipoachana ulikuwa mfalme katika nchi ya Wazulu? Umekujaje hapa katika nchi iliyo mbali na kwenu, na kukaa pamoja na wageni?"

Umslopogaas aliliegemea shoka lake refu la vita, ambalo kipini chake ni kipande kizuri cha pembe ya kifaru, na uso wake ulikuwa umejaa huzuni, kisha akawatazama wale wakazi, akasema, "Baba yangu, ninazo habari nitakazo kuambia, lakini siwezi kusema mbele ya watu wanyone hawa, maneno yangu ni baina ya mimi na wewe tu.

Mwanamke alinihaini mautini, akalifunika jina langu kwa aibu, ndiyo, mke wangu mwenyewe, mwanamwali mwenye uso kama mwezi, alinihaini, lakini niliokoka na mauti;
ndipo rnlipoponyoka katika mikono ya wale waliokuja kuniua. Nilipiga mapigo matatu tu kwa shoka langu hili Inkosikazi- hakika baba yangu atalikumbuka moja upande wa kuume, moja upande wa kushoto, na moja mbele yangu, na hata hivyo niliwaacha watu watatu wamekufa. Kisha, nilikimbia, na kama baba yangu ajuavyo, ingawa mimi ni mzee, lakini miguu yangu ni myepesi kwenda mbio kama ile ya paa, wala hapana anaye weza kunigusa tena niishapo kutoka mbavuni pake. Mbele nilikimbia na matarishi wa mauti waliniandama nyuma, na sauti zao zilikuwa kama sauti za mbwa wanaowinda, Kutoka nyumbani kwangu nilikimbia; nikampita yule aliyenihaini alikuwa akiteka maji kisimani. Nilimpita upesi kama kivuli cha mauti, na nilipokuwa nikipita nilimpiga dharuba moja kwa shoka langu, tahamaki! kichwa chake kilimtoka, kikaangukia kisimani. Kisha, nilikimbilia kaskazini. Siku baada ya siku nilisafiri; kwa miezi mitatu nilisafiri, nisipumzike, nisisimame, ila nilizidi kukimbilia kwenye usahaulifu, mpaka nilipoonana na safari ya yule mwindaji mweupe aliyekwisha kufa, nami nimekuja hapa pamoja na watumishi wake. Wala sikuleta kitu pamoja nami. Mimi niliye mtoto wa watu, ndiyo, wa damu ya mfalme mkuu Chaka, mimi niliye mkuu mwenyewe, jemadari katika kikosi cha Nkomabakosi, sasa mimi ni mgaagaa, mtu asiye na nyumba. Wala sikuleta kitu pamoja name ila shoka ili langu; kwa nguvu zake ambazo kwazo nilitawalawatu wangu.

Wamewagawanya ng'ombe zangu; wamewatwaa wake zangu; na watoto wangu hawautambui uso wangu tena. Hata hivyo, kwa shoka lili hili nitakata njia nyingine nifike mpaka kwenye ustawi. Nimesema!" Basi, akalizungusha shoka lake kichwani likalialia lilipokuwa likiikata hewa.
 
Nadhili ya Umslopogaas
amri hii ilimchukiza sana yule mzee mzulu. Kwa muda wa dakika kumi alikuwa amesimama kama kwamba anatamani kumpiga yule mjivuni, hapo basi hakuweza kustahimili zaidi, akauweka mkono wake mrefu juu ya bega la yule mjivuni, akamvuta kwa nguvu hata kumgeuza na kumfanya amtazame usoni. Kisha, aliupeleka uso wake mkali katika uso wenye duara ya manyoya wa yule mjivuni, akasema kwa sauti iliyonguruma: Waniona?"

yule mjivuni akajibu, "ndiyo, nakuona kitwana."
umslopogaas akasema, "waliona hili?" akaweka inkosikazi mbeie ya macho yake. Yule mjivuni akasema, "ndiyo, kitwana, nauona ‘mchezo' wako; ya nini?"
umslopogaas akasema, "wewe mjivuni mbwa, wewe mpayapaya, wewe mjivunaji, wewe mkamata watoto wanawake; kwa 'mchezo' huu nitavikongoa viungo vyako. Ni vyema ya kuwa u tarishi, ama sivyo, ningevitawanya tawanya viungo vyako chini katika majani.'

yule mjivuni akautikisa mkuki wake mrefu, akacheka sana kwa muda mrefu, akajibu, "laiti tungeweza kushindana mimi na wewe peke yetu, ningekuonyesha mambo."
ageuka aende zake huku anacheka. Umslopogaas akajibu, na sauti yake ingali ikinguruma, "usiwe na shaka, tutashindana peke yetu mimi na wewe. Utashindana uso kwa uso na umslopogaas, wa damu ya chaka, wa kabila la wazulu, mkuu wa jeshi la nkomabakosi, kama wengi wengine walivyofanya; nawe utajiinamisha mbeie ya inkosikazi kama walivyofanya wengi wengine. Ndiyo, cheka, cheka! Usiku wa kesho fisi watakuwa wanacheka na huku wanavunja na kuzitafuna mbavu zako."

uk 45, hadithi za allan quatermain
 
ama kweli nyinyi ni vijana wa zamani, kukumbuka vitabu vyote hivyo vya akina bulicheka na mkewe lizabeti, bibi tarabushi na kalume kenge alipokataa kwenda shule!

Ni kweli nilikutana na baadhi ya vitabu vya alfu lela u lela pale mtaa wa samora. Nilivinunua vol 1 mpaka 3 nitatafuta vyengine.

Munakumbuka hadithi ya chura aliyekuwa akisema "my name is shokolokobangoshei" na binti hawezi kutamka neno hilo. Sikujua kumbe lile neno ni la kisukuma?

ooooooooh the good old days, leo ni siasa siasa siasa hata kwa watoto wadogo jamani dunia yetu inakwenda wapi?

ni siasa tu kwa kuwa ndiyo kuna short cut ya utajiri - ufisadi.
 
mkuu ni WAGAGAGIGIKOKO halafu na mfalme wao ni HUHIHUIHUI pia yupo mzee mmoja anitwa MZEE MIRAJI.

Bila kumsahau Mpiga Filimbi wa Hamelin - I think ni kama chama fulani cha siasa hapa nchini kwa sasa. Kina makelele kibao ya ahadi lakini kinawapeleka wananchi kwenye maisha magumu kila kukicha
 
Msimsahau ABUNUWAS ambaye aliazima sufuria kwa rafiki yake akarudisha na kasufuria kadogo ndani yake na kumwambia mwenyewe kuwa sufuria yake imezaa na yeye siyo mwizi hivyo anamrudishia sufuria yake na katoto kake. Alipokwenda siku nyingine kuazima sufuria hiyohiyo mwenyewe akajisemea nyumba ya Abunuwasi ina baraka, hivyo akamwazima kwa roho safii. Safari hii sufuria haikurudi hadi mwenyewe alipoifuata na Abunuwasi akamwambia kwa vile sufuria ilizaa safari imekufa, kila kizaacho lazima kife. Abunuwasi alikuwa mwamuzi mzru sana wa kesi wakati Harun Rashid
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom