Tujikumbushe ushauri wa Rais mstaafu Kikwete katika enzi zake kuhusu nchi yako

lunganzira

Member
Nov 9, 2018
58
28

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha kukerwa na tabia ya baadhi ya Watanzania wanaotumia muda wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii Blogs kuiponda nchi yao, Akizungumza na Watanzania waishio nchini Poland alisema kwamba, "Teteeni nchi badala ya kuiponda kwenye mablogu", Rais Kikwete alisema wajibu mkuu wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi ni kuisemea vizuri, kuihangaikia na kuitetea nchi badala ya kushinda kwenye mablogu wakiiponda, kuibeza na kulalamika.

Aidha, Rais Kikwete alisema kuwa kuishi kwa Watanzania nje ya nchi kutaonekana jambo la maana zaidi ikiwa watatumia rasilimali na fursa wanazozipata ugenini kusaidia kubadilisha hali na maisha ya ndugu zao waliobakia Tanzania. Rais Kikwete pia aliwaonya Watanzania hao wasije kuchanganyikiwa na kujichanganya wenyewe kwa kuiga tamaduni za kigeni kupita kiasi. Rais Kikwete alikuwa anazungumza na Watanzania waishio nchini Poland, Novemba 21, 2013, kwenye Hoteli ya Bristol mjini Warsaw ambako alifikia wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku nne.

Aliwaambia Watanzania hao na familia zao: “Matumaini na matarajio yetu sisi tuliobakia nyumbani ni kwamba mtaisemea vizuri nchi yetu, mtaitetea nchi yenu, mtaihangaikia nchi na kuleta faida nyumbani. Ni jambo haliingii akilini kuwa baadhi yenu mnaweza kuishi hapa na kazi yenu ikawa ni kushinda kwenye mablogu mkilaumu nchi yenu wenyewe. Nchi mbaya, viongozi hawafai..mnapata faida gani? Mnazo nchi ngapi?” Rais Jakaya Kikwete akitafakari jambo juu ya utawala wake.

Aliongeza Rais Kikwete: “Kuhangaikia nchi yetu ni wajibu wenu ambao hamwezi kuukwepa. Matumaini yetu ni kwamba mtasukuma mbele maslahi ya nchi yenu, mtatetea ustawi wa nchi yenu na ndugu zenu.

Fursa zilizoko hapa mnazijua wenyewe, sisi hatuzijui. Nyie ndio mnaishi hapa, sisi tuko mbali na hatuwezi sisi kutegemewa na kutarajiwa tufanye mambo ya hapa ambayo hatuyajui.”

Alisisitiza Rais Kikwete: “Mbona kazi za ma-Ngo’s mnazifanya vizuri bila kusukumwa ama kushawishiwa lakini kazi za kusaidia ndugu zenu hamfanyi? Kama hata hamwezi kusaidia ndugu zenu mnachangia nini nchi yenu?
 
Back
Top Bottom