Tujikumbushe tulikotoka

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,770
10,660
Shehe Yahya amtabiria JK ushindi 2010
Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 23rd December 2009


MTABIRI maarufu wa Afrika Mashariki, Shehe Yahya Hussein ametabiri kuwa Rais Jakaya Kikwete atashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao na atakayempinga ndani ya chama chake atakufa ghafla.

Sambamba na hilo, atakayeonekana kumshinda nje ya chama chake pia atapoteza maisha vivyo hivyo.

Akitoa utabiri wake jana Dar es Salaam, juu ya uchaguzi mkuu mwakani, Shehe Yahya alisema ushindi wa Rais Kikwete unatokana kurithishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1995 ilipodaiwa kuwa Rais Kikwete alishinda kwenye kura za maoni lakini akamsihi amwachie Benjamin Mkapa.

Alisema ushindi wa Rais Kikwete unatokana na kutanguliwa kwa vifo vya watu waliotokea sehemu moja ambapo mwaka 2005 kabla ya uchaguzi, Mwenyekiti wa CCM Songea alifariki dunia na mwaka huu kabla ya uchaguzi tena kumetokea kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM , Lawrence Gama ambaye anatokea pia Songea.

Alisema ushindi huo utaleta Serikali za mseto Tanzania Bara na Visiwani na kuongeza “kwa mara ya kwanza Waziri Mkuu ajaye atatokea Upinzani na kwa Zanzibar, CUF imeshaonekana kushinda”.

Shehe Yahya alisema upinzani nje na ndani ya CCM utasambaratishwa na baadhi ya viongozi kujiunga na kambi ya Rais Kikwete wakiwamo wa Upinzani.

Mtabiri huyo alisema kutokana na ushindi huo katika uchaguzi wa mwakani kwenda sambamba na vifo, kutatokea kifo cha kiongozi wa zamani wa kitaifa kati ya sasa na Aprili mwakani, kabla ya uchaguzi.

“Kutatokea maandamano makubwa kupinga matokeo ya uchaguzi kuhusu wabunge wa pande zote wa CCM na Upinzani kuhusu wizi wa kura. Maandamano hayo yatasababisha kesi kubwa kupinga matokeo ya ubunge wa pande zote,” alitabiri.

Katika utabiri wake huo wa mwisho wa mwaka huku akiahidi kutoa utabiri mwingine Januari 10 mwakani, Shehe Yahya alisema baadhi ya viongozi wa sasa wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere watajiuzulu kwa aibu itokayowafika kuihusisha taasisi hiyo na siasa ya kumpinga Rais Kikwete, ilhali taasisi hiyo ni ya watu wa pande zote na si ya siasa bali ya kusaidia kila mtu.

Mtabiri huyo ambaye alijitapa kutabiri na matukio kuwa ya kweli ikiwemo ya kiongozi kupigwa kibao ambapo Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi alikumbwa na masahibu hayo, alisema mwakani pia kutatokea ajali nyingi kwa vyombo vya usafiri na pia hali ya uchumi kwa Watanzania itakua.

Awali Msaidizi wa Shehe Yahya ambaye ni mtaalamu wa nyota, Abdulrahman Ally, akitoa utabiri wa nyota wa mwaka 2010 akisema utakuwa wa mabadiliko makubwa kwa watu watakaotawala nchi, huku mashindano makubwa kati ya mataifa yenye nguvu yakiongezeka.

“Marekani itashuka katika wadhifa wake wa kidunia, huku mataifa madogo yanayokua yatakwaruzana na majirani zao, hii inaamanisha mwaka 2010 ni mwaka wa ugomvi kati ya nchi na nchi,” alisema.

Ally alisema watu wa ibada, wanaozingatia uongofu kuliko uoga, wenye mapenzi dhidi ya chuki watakuwa na furaha kubwa mwakani

Source: Habari Leo.

What a crap!
 
Back
Top Bottom