Tujikumbushe Songea Boys {Box 2} | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujikumbushe Songea Boys {Box 2}

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by stanluva, Jul 17, 2009.

 1. stanluva

  stanluva Senior Member

  #1
  Jul 17, 2009
  Joined: Apr 7, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Na kumbuka Mabweni ya Urafiki, umoja, maendeleo, ujamaa na muungano!

  • Nakumbuka shida ya umeme iliyokuwa itokea na kulazimika kutumia chemli!

  • Kama mtakumbuka Kuna kisima cha kupampu a.k.a Shadufu! Aisee kilitoa msaada wa kutosha katika kutupa maji ila ndo kuoga watu ilikuwa issue passport kama kawa!

  • Pia kulikuwa na huduma ya mihogo "mayau/mayao au makaba" ya kuchemsha kila asubuhi wakati wa uji "pola" ya kiuzwa na wamama wa vijijini toka Mletele!
  • Nakumbuka library yetu ilivyokuwa imechoka ukiingia utakuta vitabu vya hadithi za Abunuasi na adili na nduguze! Vitabu vya taaluma iliku vya enzi zile za 67! Dah ilikuwa shughuli kama kulikuwa na assignment!
  • Kwa wale wapenzi wa disco mnawakumbuka tamsala/ Tamso "Songea Girls" Mwanangu ilikuwa lazima Uoge na Pafyum!

  • Nakumbuka mitaa ya Ulokoni {vijijini} kulikuwa na mama mmoja maarufu kama binti bull huyo mama dah ni noma kila service unapata chakula na vingine pia!

  • Bila kusahau Kuchunga Ng'ombe wa shule na kulima mashamba ya shule dah ilikuwa kazi kwelikweli kwa sisi watoto wa ocean road jembe hatukuwahi kulishika zaidi ya kusomakwenye vitabu!
  • Namkumbuka mwl. mmoja muhohela vijana walikuwa awakimwita maps da alikuwa ni noma ni zaidi ya Feudal wa Tosa Huyu alikuwa capability ya ajabu ya kukutambua akiwa umempa mgongo kisha ukiwa na bifu naye duu utajuta!
  • Bila kusahau umbali uliopo toka mjini hadi shule {4KM} lakini dah wazee tulikuwa tunachapa kwa mguu unaweza kwenda na kurudi mara mbili au zaidi! Lakini leo tunapanda gari fire na kushukia bahkresa kariakoo!
  Naomba kama unakumbuka vingine usisite kuchangia napenda kuwasilisha wakuu!
   
 2. R

  Rayase Member

  #2
  Jul 18, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mmmmh! inapendeza! mzee ni long sana! kwa kweli ni zamani kidogo! Nimefurahi! Umesau mambo ya punga siku ya j1! au mbogamboga kwa mama jeni na wengine! Kwa kweli inapendeza siku ya jumatatu wakati wa weekly report! food supply, water supply, social affairs zote was normal! Ni matamu sama yale maisha! Kwa kweli kile chuo cha mafunzo ni balaa!
   
 3. t

  tishekwavb Member

  #3
  Jul 18, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 8
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umenikumbusha mbali ila umesahau small mbufu unakula kama hujakutana na jiwe utakutana na snail. Zile mbufu zilizokaa muda mrefu na kuwa na wadudu. Umesahau magoti, baadhi ya maneno kama mlonda kwa maana ya mlinzi, umemsahau mwalimu wa nidhamu Mpalile. Marehemu mkuu wa shule Mwalimu Mkoba anatembea ananyata kwa umardadi amepiga perfume kilometa moja unaisikia, na kile kivokswagen chake (Chura). Katika mayao husisahau vilevile mandondo
   
 4. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Haaa my beloved box 2,jamani sijui lile grunding lipo kwani ule wakati tukidance na wana Tamso mambo yalikuwa kama sukari,jamani enzi zetu pale box 2 wakati ule kulikuwa hakuna ukimwi na sijui yale mashamba ya mahindi yapo au ndo mafisadi wameshafisadi,nakumbuka dangron kwenye mihogo ya nuru na kwa mzee Toinyo kwenye maembe,na bugo la Mwanaume Mavere sijui yuko wapo, pia RIP Eddy,Dudu and others .Na wengine akina Yusuph Mdoe,Yahya ,Smasher,KaiKai,Elias John washington(mtukutu)Hanse mwandemelela.Na wote tuliojenga uwanja wa majimaji,
  Wana box 2 wa mwaka 1981.
   
 5. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mhh mzee box tuu ya mwaka 1981 long time hiyo! heshima mbele mkuu Mfianchi. Nakumbuka mandazi ya Gawaza pale kijijini Ruhira.

  Kuna hadithi moja niliipata nikiwa Box 2,kuna mtu mmoja alikuwa na wake kama wanne maeneo yale na wake zake walikuwa wanauza mayao wote.Nafikiri wawili kati yao walikuwa hawana umri mkubwa na vijana walikuwa wanawatamani lakini inasemakana Mume wao alikuwa kafanya mambo ya kimazingara ukienda nao kufanya mambo kila ukitaka kuchomoa ''Mpini'' unatoka na vidagaa vidagaa vinaunganika na ukeni mpaka aje awafumanie ndiyo mnaweza kutenganishwa.
   
 6. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mfianch heshima kwako 81 nilikuwa na miaka mi 2! Ila Rayase najua ni PCB member mwenza ingawa haujaongelea hata mama wa biology na mwalimu wetu wa physics kama unakumbuka hii " you take this thing here you place this thing here then you do some manuva n' this is the answer"
  Umenikuna sana hapa kwa bint bulu huduma kotekote we acha tu.Vp bado unataarifa zake mkuu?
  Na pale juu ya bint bulu Mikinda kwa yule dada mke wa mkubwa pia palikuwa ni poa sana.Hii ndo Box2!
   
 7. R

  Rayase Member

  #7
  Aug 19, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kuna tetesi et kafariki! si unajua mambo ya ukame vijana walikuwa wanapona kiana!
   
 8. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ha ha ha haaaa, unakumbuka ugomvi wa Tamsala na box 2. Tamsala walikuwa wanamind kaigo (kigonsela) kwa sana. nakumbuka miaka ya 88-89 box 2 waliwachapa tamsala kwenye sikukuu ya kumbux2 ya mashujaa.

  kisa tamsala waliandika barua chafu kwa box 2, sitaki kukumbuka hiii... chafu sanaaa.
   
 9. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Rayase una maanisha binti bulu ndo kapoteza? Mbona tutawakosa vijana wengi sana! Mkuu chamtu Tamso si tuliona hawana issue tukawa tuna import toka Peruu! Vp mliwachapa Tamsa kwa kutumia fimbo ipi?
   
 10. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu sisi ndo tuliwachapa Tamsala miaka hiyo alikuja Aboud jumbe wakati huo ni kigogo sasa tuliambiwa eti sisi ni NATO kwa wana box 2 nafikiri mnajua manake tulikasirika sana na tukawaburuza kwa sana,mwenzangu mmoja kwa kuhofia kufukuzwa akasema haendi atakuwa mlinzi wa bweni pale Uhuru loo ,so lilipo ibuka la kutaja watu waliowapiga hao tamsala naye akatajwa ilihali hakuenda maskini wa mungu kwa hasira akamtukana mwalimu pale parade na akafukuzwa ,huyu jamaa alikuwa ni kati ya watu wachache ambao Mungu aliwajaria kwa kuwa bright,na tulitegemea angefika mbali,kwa sasa nasikia ameishia kunywa mataputapu,inasikitisha.NIGWISAI LELO ,OH MAMA KADODA ANALIA NA MSUKUMANO na mimi hizi ngoma tulikuwa tunatoroka usiku kwenda ulokoni
   
 11. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Agagangiii,

  mfiachi kumbe umo! kwa kweli ilisikitisha sana. ndo maisha hayo.
   
 12. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Agagangi, mfiachi kumbe upo!
   
 13. R

  Rayase Member

  #13
  Sep 16, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mmmmH! Kwanza heshima yenu wakubwa zangu na wewe Mpcb mambo vp? kweli inapendeza kwani nakumbuka hata pale ambapo tuliwasusa tamsala na wao wakaamua kwenda kaigo eti kutukomoa! kama kawaida waboys wakazamia! Mzee mfinachi, hivyo vichapo vilitokea pia na ttc !Ni balaa! tuliwatandika ttc baada ya kumchoma kisu mboys mwenzetu mpaka wakaruhusiwa kuvaa 'civil' town kwan tukiwakuta ni kichapo! uli ugomvi nao ni balaa et nasikia unaendelea mpaka leo!
   
 14. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ila siku hizi nasikia camp limebadilika sana usafiri si kama zile enzi zetu toka town hadi xkul unakanyaga.
  Ila leo nimeyakumbuka kidogo yale mayao bandugu...na vichwa vya samaki...
  Rayase tupo pamoja kaka ila sijakuona kitambo pale uso wa kitabu...
   
 15. stanluva

  stanluva Senior Member

  #15
  Nov 10, 2009
  Joined: Apr 7, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kaka mkubwa nakubaliana nawe, huwezi amini sasa usafiri toka Deluxe hadi boys karibu na msikitini au karibu na kilabu kimoja cha pombe kwa mzee komba! Hivi kaka hatuna organization hivi kakuweza kusaidia pale box 2?
   
 16. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Ah, mwaka wetu tulimgomea H/Master Mbao na wapambe zake akina Mwachombe na Ndimbo. Hali ilikuwa mbaya mpaka wakafukuzwa wanafunzi kadhaa wakati tunaelekea kwenye mtihani. halafu tulikuwepo tuliokoswakoswa tukaitwa vikambale vilivyokoswa na kokoro! Lakini miaka kadhaa baadaye tulikutana na Mwachome na Mzee Mbao wakiwa kwenye mkutano. Tukakaa pamoja tukapiga kinywaji na tukakumbushana. Mzee Mbao alikiri kwamba hali ilikuwa ngumu upande wake na isingekuwa urafiki wake na Katibu wa Wizara ya elimu alikuwa atimuliwe kazi. Ila kwa uswahiba huo, kibao kiligeuzwa kwa wanafunzi!
  Anasema bado hilo ni tukio ambalo hata wao walimu huwa wanalijadili ili kujikumbusha wajibu kwa wanafunzi. So if we decide we can al;so make a change to our country, just be determined.
  Ah, mmenikumbusha mbali sana....
   
 17. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #17
  Nov 11, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Duh, Wana JF, nyie mlitutangulia. Bifu lenu na tamso lilisababisha tucheze disco mchana kweupeee.. hiyo ni 1991 -93. Dispensary alikuwepo mzee Kidato...(Clinical officer). Nakumbuka ligi ya mabweni, Azimio tuliibuka mabingwa na kuzawadiwa mbuzi. Vijana wa Tunduru (mawia) walikula mpaka ngozi ya mbuzi. Ukiwa na appointment na tamso lazima utunge ugonjwa mkubwa ili uende hospital ya mkoa ukajihudhurishe.

  Duh, jamaa kanikummbusha shamba, nusu ya shamba tulikuwa tunalima marejea, hiyo kazi sikuipenda kabisa.. Nilichokipenda ni soft diet kwa sisi mabingwa wa kufoji.

  Kiranja wa starehe alikuwa maarufu kuliko kaka mkuu, hasa kwa upande wa Tamso.

  Nakumbuka dogo mmoja (form three) tulimkamata darini usiku akiwa Uchi. Hakujua vijana wa kwa Pinda tulikuwa fiti..
   
 18. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  [​IMG]


  Nakumbkua "LUILA NEWS pale assmbly"...Ulokoni, Mawia, Kabwela, Mapsi, Ndimbo, Mahinya (R.I.P), Tamso, TCC Matogoro (Wale Mashemeji zetu)..Ulanzi na komoni..shimoni. Wale wa Azimio1 na Uhuru...mambo ya kuficha madishi ya "Bondo" chini ya uvungu wa kitanda, chingazi haziingii class kwa ajili ya kuwahi "poligi" na "lea"(utandu wa mafuta kwenye dishi la maharagwe". ...Ndi ezi zile za vurugu za LUILA na TCC Matogoro pale Mjimaji, TCC wakachapwa mpka usiku ...ni Enzi za vijana toka Tambaza alipopoteza umaarufu kabisa baada ya kuletwa LUILA ..

  Enzi za suali za "BIOACT", mashati ya "NINO, TOMATO, na viatu mokasini na laba za plastic za "BENQ ..siku za kwanja kule TAMSO chinga anakuja kukuazima suluali na viatu akiondoka kapotea navyo ulokoni ...

  Kula ulokoni kulikua na mabinti kama hawa:
  [​IMG]


  Utawala wa HP Mjenga O!.
   
 19. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Heh heh vijana wangu mmenikumusha mbaliii mpaka machozi yananitoka,nakumbuka tukitoka likizo tulikuwa hatuingii mesi bana,kwani tulikuwa tukija na vijisenti (Tsh 200) kwa hiyo kuanzia asubuhi tulikuwa hatunywi mataputapu(uji usio na sukari),jioni mbufu walikuwa wanamwaga,baada ya siku tatu tu vijisent vikiisha hata mataputapu yalionekana lulu.Kiti muhimu ni kuwa box 2 kwenye taaluma tulikiwa tunakuwa nambari wani pamoja na matatizo yote,vijana wangu matatizo box 2 hayakuanza leo wala jana ni longi sisi tulikuwa tukioga mtoni na kujisaidia kwenye mahindi kwani vyoo vilikuwa vimechoka ile mbaya,pia hakuna kitu kilikuwa kinatuudhi kama kuchunga ng'ombe kwani maziwa walikuwa wanakunywa waalimu pekee nasi tukipata mara chache,jamaa wakaona na isiwe taabu wakachukua mifuko ya lambo ikapakwa chumvi na wakapewa ng'ombe basi baada ya muda ng'ombe mmoja baada ya mwingine wakaanza tangulia mbele ya haki.
   
 20. Njaa

  Njaa JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2010
  Joined: Dec 6, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 60
  Wakuu mmenikumbusha mbali sana leo, nilikuwa sijaiona hii threat! Kuna vijana nimeweza kuwatambua kwa lugha zao kama kama mvina (pcb) Rayes (pcb), stanluva na wengineo, hawa nilikuwa nao pamoja ingawa humu hatutambuani, Mvina binti bull katangulia, niliogopa kukuambia maana najua ulikuwa unapumzika pale mkuu!!! Rayes nakumbuka uliweka bill kabisa ya mihogo!

  Tamsala nimewamisi kwa sana, nakumbuka Mviana ulikuwa na Jeans lako linavaliwa siku ya Tamso pekee! Halafu kuna wale wenzangu na mimi tulikuwa tunaenda ulokoni kuangalia zile movies chafu!!!! Halafu ukirudi kama kawa bafuni. Wale waliokuwepo enzi za binti bull wanamkumbuka yule shoga jirani na bweni la ujamaa 3?? Bado yupo?? au na yeye ndio hivyo tena kasogea??

  Ugomvi na ttc hauwezi kuisha pale! ule ni wa kihistoria! Maps yupo?? Wale wa songea watupe data. Asante kwa hii picha ya songea Mkuu
   
Loading...