Tujikumbushe Somo Ugonjwa hatari wa kuharisha (Diarrhea)

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Jana nilishindwa kuendelea kujibu maswali kwenye uzi wangu niliouandika ghafra tu baada ya kubanwa na maumivu makali ya tumbo la kuharisha(diarrhea ) na hii ni baada ya kugundua kwamba nilikunywa Supu ya kuku na chapati asubuhi ya kuelekea mchana sehemu flani hivi bila kutazama mazingira ya usafi kama ni salama na rafiki kwa Afya yangu,

Leo nimekuja kutoa somo kidogo jinsi gani ya kuhepuka Ugonjwa huu hatari wa kuharisha(Management ),

-Kwanza kabisa nianze hivi ukiona tu Tumbo linauma mara tu baada ya kutoka kula kitu flani either chakula, Tunda or maji basi ujue ulikula/kunywa kitu kisicho salama yaani kitu kichafu ambacho hakikuandaliwa katika hali ya usafi,

-Popote uendako unapokuta kitu chochote cha kula kabla ya yote hakikisha kwanza kama kimeandaliwa katika hali ya usafi,

--Kama ni chakula angalia mazingira ya pale walipokiandaa na chombo walichokuwekea N.K

--Kama ni tunda hakikisha limeoshwa vizuri tena kwa maji safi na salama,

--Pia kama ni maji ya kunywa basi hakikisha yapo salama yamechemshwa au kuwekwa dawa ya kuulia bakteria eg Water guard,

---kabla ya kula chochote hakikisha mikono yako umenawa vizuri kwa maji ya kutiririka siyo ya kuwekwa kwenye kibeseni, kama sabuni ipo hakikisha unaitumia ili kuondoa bakteria waliopo mkononi,

--Usikubali kula wala kunywa chochote sehemu ambayo unaona hali yake ya usafi haiko salama, kumbuka Afya na maisha yako ndio kila kitu hakuna Replacement,


Ugonjwa wa kuharisha una madhara mengi,(Effect)

--kwanza kabisa unaambatana na maumivu makali ya tumbo,

--pili unamaliza maji mengi mwilini kutokana na ile hali ya kuharisha kinyesi chenye maji mara kwa mara,

-- tatu unanyongonyesha mwili,

--nne unaweza kusababisha kifo kwa sababu ya upungufu wa maji mwilini unaotokea baada ya kuharisha kinyesi ambacho ni kama maji in nature,


Tiba yake(Treatment ),

-Kabla ya kujua tiba ni bora kabisa ukafuata njia za kuukabili(Management) ili usikupate waswahili wanasema kinga ni bora kuliko tiba mi nilipuuzia matokeo yake jana yangu ilikuwa ni balaa, jana niliyopata maumivu makali ya Tumbo,

--kwanza kabisa ukiona tumbo linauma na mara umeanza kuharisha ni vyema ukawahi hospitary iliyo karibu nawe watakufanyia yafuatayo;
----wakiona frequency yako ya kuharisha ni very high watakuwekea drip ya maji LR(linger Ractate) "iv" (intra Venus ) kama sikosei ili kurecover maji yaliyopotea,
Kama frequency yako sio sana utapewa maji safi yaliyochanganywa na Oral suspension lita 1½ utakuwa unakunywa kila wakati ili kurecover maji yaliyopotea wakati unaharisha,

--wataangalia na kupima kama case ni kipindu pindu(chorela),mchafuko wa Tumbo tu au ulikula chakula chenye sumu utapewa tiba kulingana na case yako ilivyo,


kama ugonjwa umekupata na wewe uko mbali na hospitary either Uko shambani or kijijini ambako ni mbali na kituo cha Afya fanya hivi;

--Hakikisha unachukua maji yaliyochemshwa na kupoa weka kwenye jagi au chupa iliyo safi na salama,
chukua chumvi na sukari kidogo changanya then utakuwa unakunywa kidogo kidogo ili kurecover yale maji yaliyopotea wakati unaharisha,
Ukiona hali inazidi kuwa mbaya hakikisha unatafuta msaada mapema ili uwahi hospitary au kituo chochote cha Afya,

Usilete utani wala kuchukulia poa ugonjwa wa kuharisha mara tu pale unapokuanza hakikisha unatoa taarifa mapema kwa ndugu au rafiki zako wa karibu ili kuepuka kuzidiwa na kukosa msaada,

Ugonjwa huu ni mbaya ila wengi wanauchukulia poa tu ukiharisha zaidi ya mara 5 jua kwamba unapoteza maji mengi mwilini na kifo kinakunyemelea usipopata Tiba mapema, wengi wamekufa kama utani kwa kudhani ni hali tu ya mpito,


Note
Somo hili nimelitoa mimi kama mimi Zero IQ, sijacopy mahali sasa wale wa kucopy na kupaste kwenye blog zao wajitahidi kutoa credit kwa mtoa mada.

Nb.
Zero IQ nimenusurika jana kwa huu ugonjwa vinginevyo ningepotea humu jukwaani kama ben saa nane bila yeyote kujua wapi nimeelekea kumbe zamani Zero ningekuwa tayari nimesha R.I.P


Cc Zero IQ
 
safi sana kwa kitu ulicho andika naamini jamii itafaidika na elimu hii uliyotoa leo.
Mungu wa mbinguni akuzidishie pale ulipo
pungukiwa na akupatie kila unachostahili katika huu ulimwengu
 
Asante kwa somo nimeumwa Tumbo hivi karibun diarrhea inakuwa asubuhi. Dawa zenyewe ni chungu flagile hata kama unakunywa maji bado mdomo ni mchungu
 
Tumbo lilishawahi kunisumbua siku 3 naendesha mwanzo mwisho. Haipiti nusu saa bila kwenda chooni, iwe usiku iwe mchana. Daaah, nilikunywa dawa mpaka mwili wote unanuka dawa, mpaka maji nayo unayaona hayana radha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom